Kwa nini Marekani imekataa kuwapeleka mbwa wake Jordan na Misri

Mbwa wa kunusa vipilipuzi

Chanzo cha picha, Press Association

Maelezo ya picha,

Mbwa wa kunusa vilipuzi hutumika katika mataifa mengi kukabiliana na ugaidi

Marekani imekataa kuwapeleka mbwa wake wa kufichua vilipuzi katika mataifa ya Jordan na Misri kufuatia vifo vya baadhi ya wanyama hao kutokana na uzembe.

Kifo chochote cha mbwa ni kitu cha huzuni, alisema msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani.

Mnamo mwezi Septemba, ripoti ya Marekani iliangazia visa vya uzembe katika zaidi ya mbwa 100 waliopelekwa Jordan na Misri na mataifa mengine manane katika miaka ya hivi karibuni.

Pia unaweza kusoma:

Mbwa hao wa Marekani walio na mafunzo walipelekwa katika mataifa hayo ikiwa ni mpango wa vita dhidi ya ugaidi.

Jordan na Misri kufikia sasa hazijatoa tamko lolote.

Marekani ilitangaza marufuku yake ya muda siku ya Jumatatu. Wizara ya maswala ya kige ni nchini humo ilisema kwamba hatua hiyo inalenga kuzuia maelezo zaidi.

Chanzo cha picha, Canine Validation Center

Maelezo ya picha,

Wawili kati ya mbwa waliokosa lishe bora wapatiikana nchini Jordan

''Mbwa hao wana jukumu muhimu katika vita dhidi ya ugaidi katika juhudi zetu ughaibuni kuokoa maisha ya raia wa Marekani'' , maafisa hao walisema.

Maafisa hao hatahivyo walisema kwamba mbwa waliopelekwa nchini Jordan na Misri watasalia katika mataifa hayo kwa sasa.

Ripoti hiyo ya wizara ya maswala ya kigeni ofisi ya inspekta jenerali ilisema kwamba mbwa mmoja alifariki Jordan 2017 kutokana na joto jingi.

Mbwa wengine wawili walirudishwa nchini Marekani wakiwa katika hali mbaya , ilisema taarifa.

Maafisa wa Marekani walisema kwamba waliamua kumuua mbwa mmoja kabla ya kumsaidia aliyesalia kuimarisha afya yake kwa kuwa alikuwa na uzani mdogo.

Mbwa wote watatu walikuwa ni wale wa Belgian Malinois.

Ripoti iliofuatia mwezi huu ilifichua kwamba mbwa wengine wawili waliotumwa Jordan walifariki kutokana visa visivyo vya kawaida : moja wao kutokana na joto kali na mwengine kutokana na dawa ya kuua wadudu ilionyunyizwa na maafisa wa polisi kulingana na AFP.

Jordan ndio imekuwa ikichukua mbwa wengi kutoka Marekani huku mbwa 100 wakitumwa katika falme za mashariki ya kati.

Ripoti hiyo ya Marekani pia ilisema kwamba watatu kati ya mbwa 10 waliopelekwa Misri walifariki kutokana na matatizo ya saratani ya mapafu, kupasuka kwa vibofu vya mikojo na joto kali 2018-19.