Kesi inayomkabili Trump: Viongozi wa Democrat na Republican walumbana

McConnell

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Democrats na Republicans walumbana kuhusu kesi ya Donald Trump

Viongozi wa Republican na Democrats katika bunge la seneti nchini Marekani wamelumbana kuhusiana na kanuni zitakazofuatwa katika kesi inayomkabili rais Donald Trump.

Democrats wanataka hakikisho kwamba mashahidi na baadhi ya stakabadhi muhimu zitaruhusiwa ili kuruhusu kile ambacho wanakitaja kuwa kesi ya haki.

Kiongozi wa Democrats Chuck Schumer anasema kwamba ufichuzi wa barua pepe kuhusu msaada wa Ukraine ni kumbusho kuhusu kwa nini uwazi unahitajika.

Lakini hakukosa kukubaliana kuhusu iwapo mashahidi wataruhusiwa kutoa ushahidi wao wakati wa kesi hiyo.

Rais Trump alipigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika bunge la uwakilishi wiki iliopita kwa matumizi mabaya ya mamlaka na kulizuia bunge la uwakilishi.

Ni rais wa tatu katika historia ya Marekani kushtakiwa.

Hatahivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba hataondolewa afisini kwa kuwa chama chake cha Republican kina maseneta wengi katika bunge hilo ambapo kesi hiyo itafanywa kama ilivyo kulingana na katiba.

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi ujao baada ya likizo kukamilika. Lakini wana Democrats kufikia sasa wamekataa kutoa stakhabadi za kesi hiyo iliopigiwa kura na bunge la uwakilishi na sasa itarajiwa kuwasilishwa katikab bunge la seneti.

Wanataka hakikisho kutoka kwa bwana McConnell kwamba mashahidi wao waliowachagua - karibia wanne wakiwa wafanyakazi wa sasa na wa zamani wa Ikulu wakiwa na ufahamu kuhusu kilichotokea Ukraine -wataruhusiwa kutoa ushahidi.

Bwana Trump anatuhumiwa kwa kumshinikiza rais wa Ukraine kuanza uchunguzi dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa , mgombea wa chama cha Democrat Joe Biden.

Bwana Trump ameshutumiwa kwa kuzuia msaada wa Ukraine

Je McConnell alisemaje?

Hatujakataa mashahidi , bwana McConnell aliambia kitengo cha habari cha Fox News siku ya Jumtatu.

Alisema kwamba atasimamia kesi kama ile iliomkumba aliyekuwa rais wa wa Marekani Bill Clinto 1999, ambapo maseneta waliamua ni mashahidi gani watakaoitwa baada ya kufungua mjadala na maswali.

Bwana McConell alimshutumu spika wa bunge la uwakilishi Nancy Pelosi kwa kushikilia nafasi na kusema kwamba anajaribu kutueleza jinsi ya kuendesha kesi hiyo katika bunge la seneti.

Democrats wanasemaje?

Maelezo ya picha,

Kiongozi wa Democrats Chuck Schumer anasema kwamba mashahidi ni sharti wasikilizwe

Walisisitiza kuletwa kwa mashahidi wikendi baada ya barua kufichuliwa ikisema kwamba Ikulu ya Whitehouse ilijaribu kukatiza msaada kwa Ukraine dakika 91 pekee baada ya rais Trump kuzungumza na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa simu mnamo mwezi Julai.

Simu hiyo ambayo ipo katikati ya madai dhidi ya Trump - ambayo rais huyo amekana.

Chuck Schumer alisema kwamba yeye na mwenzake wa Republican wapo katika mkwamo baada ya kufanya mkutano muhimu siku ya Alhamisi ili kuzungumzia sheria za kesi hiyo.

Wakati wa mkutano na wanahabari nyumbani kwake huko New York siku ya Jumapili , bwana Schumer alisema kwamba Republicans hawajatoa sababu muhimu kwa nini hakupaswi kuwepo kwa mashahidi na kwa nini stakhabadhi hazifai kutolewa