Mafunzo ya kusherehekea Krisimasi njema

Two young women looking cross

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuanzia usiku wa kuamkia Krismasi, familia huwa zina hekaheka nyingi kufikia sikukuu ya Krismasi.

Na mara nyingine ndugu wanaweza hata kutofautiana kwa kile wanachokitaka kwa siku hiyo, mfano rimoti ya televisheni ya kipi wanataka kuangalia.

Krismasi ikipangiliwa vizuri basi inakuwa siukuu nzuri zaidi, haswa unapozingatia yafuatayo:

1. Upendo wakati wa Krismasi

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwenda nyumbani ulipozaliwa ni jambo zuri sana -lakini unapofika je utalala katika kitanda chako cha utoto pamoja na watoto wako?

"Hata kama tuna kazi nyingi au tuko nyumbani, kuna wakati huwa tunapata wa kukaa peke yetu.

Lakini sikukuu ya Krismasi huwa inawalazimisha watu mara zote kuwa wengi katika sehemu moja".

"Kama una ndugu , lazima huwa kuna jambo la kufanya kutaka kuwa na mtu fulani kuongea naye.

"Watoto walikuwa wamezoea kukaa na wazazi wao, lakini wazazi wamekuwa wakiwapuuzia kutokana na tamthilia na kukataa kucheza nao".

Ni vyema kuthamini watu walio karibu yako na kutenga muda kwa ajili yao na kufanya familia iwe na furaha siku ya Krismasi na haimaanishi kuwa mnapaswa kuwa pamoja saa 24.

Badala ya kutarajia kila mtu kujumuika sikukuu ya krismasi , labda watu wanapaswa kukubaliana muda wa kufungua zawadi, muda wa kula chakula cha mchana au mtu kuendana na mazingira yaliyopo.

2. Sio sikukuu ya upishi peke yake

Chanzo cha picha, Getty Images

Mapishi siku ya Krismasi huwa ni shughuli kubwa.

Kuna mambo mengi ambayo , mara nyingi watu huwa wanatumia ujuzi wao wote kupika mapochopocho na hekaheka kuwa nyingi.

Kama mmepanga kupika, si jambo baya kuomba msaada kwa watu ili mpike pamoja.

"Hakikisha kuwa umeweka ratiba ili kila mtu aweze kusaidia katika upishi."

Ni muhimu kwa kila mmoja awe anajukumu katika shughuli hiyo, kama kupika nyumbani ni changamoto basi ni vyema kuagiza.

3. Krismasi ni sherehe ya nani?

Chanzo cha picha, Getty Images

Mara nyingi watu wanaiona sikukuu hii ni kwa ajili ya watoto na mara nyingine wengine huona kama ya watu wazima na wakati mwingine ni ya familia.

Kadri miaka inavyozidi kuna tofauti sana ya mtazamo wa sikukuu hii.

Watoto huwa wanafurahia kupata zawadi wakati , watu wazima wanafurahi kunywa pombe kabla ya usiku haujafika na kubishana siasa.

Kikubwa ni kuwa familia huwa zimeweka utamaduni wa kujumuika kwa pamoja.

4. Maelewano wakati wa Krismasi

Ni vyema kukubaliana kufuata utaratibu fulani katika siku kuuu ya krismasi.

Ni wazo zuri ili watu waweze kuheshimiana na kufurahi kwa pamoja bila kubishana.

Kama mtu amekuudhi basi ni vyema kukubali kupuuzia.

5. Teknolojia

Chanzo cha picha, Getty Images

Kumbuka kuwa kuna televisheni moja na watu ni wengi hivyo inabidi kukubaliane cha kuangalia?

Licha ya kwamba siku hizi simu zimechukua nafasi kubwa zaidi, lakini vyema kuweka mbali teknolojia na kuwa karibu na walio karibu yako.

6. Kuimba wakati wa Krismasi?

Chanzo cha picha, Getty Images

Muziki huwa ni namna nzuri ya kufurahia sikukuu hii na kuleta familia karibu na kumfanya kila mmoja afurahie siku hii.

Unaweza kutumia mtindo wa kila mmoja kuimba ili kuwafanya wajumuike kwa ukaribu zaidi.

7. Umakini wa bajeti yako

Kuna mambo mengi ya kununua wakati huu wa krismasi lakini kumbuka kuna mwezi unaofuata ambao una majukumu mengi zaidi.

Januari huwa ni mwezi mgumu sana, majukumu huwa mengi. Ni vyema kuwa na kikomo katika bajeti yako.

8.Krismasi inataka watu wafurahi

Krismasi ni wakati wa furaha. Migogoro na ugomvi sio wakati wake hivyo ni vyema watu kuwa na amani na furaha katika siku hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images