Tetesi za soka Ulaya Jumatano 25.12.2019: Werner, Pogba, Neymar, Haaland, Alonso, Cavani

Chanzo cha picha, Reuters
Barcelona itarjariubu kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar
Barcelona itajaribu kumsaini mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 27, katika dirisha dogo la mwezi Januari. (Goal)
Chelsea inafikiria uhamisho wa mwezi Januari wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23. (Express)
Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26, anataka kuondoka katika klabu hiyo na kurudi katika klabu yake ya zamani Juventus. (Calicomercato - in Italian)
Chanzo cha picha, Reuters
Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba, 26, anataka kuondoka katika klabu hiyo na kurudi katika klabu yake ya zamani Juventus.
Mario Mandzukic amemaliza uvumi uliokuwa ukienea baada ya kukamilisha uhamisho wake katika klabu ya Qatari ya Al-Duhail licha ya Man United kuonyesha hamu ya kumsajili kutoka Manchester United. (Mail)
Manchester United inajiandaa kumpatia mshambuliaji wa Norway Erling Haaland mshahara wa £200,000 kwa wiki ili kujiunga nao kutoka Red Bull Salzburg. (Sun)
Beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, analengwa na klabu ya Inter Milan. (Calciomercato)
Beki wa Chelsea na Uhispania Marcos Alonso, 28, analengwa na klabu ya Inter Milan. (Calciomercato)
Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, anakaribia kukamilisha uhamisho wa mwezi Januari kuelekea Atletico Madrid. (Marca)
Arsenal inatarajiwa kumuuza mmoja ya washambuliaji wake na kumnunua mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele. (Le10Sport - in French)
Everton na Atletico Madrid wanapigania kumsaini mshambuliaji wa River Plate na Colombia Rafael Santos Borre, 24. (AS)
Arsenal inatarajiwa kumuuza mmoja ya washambuliaji wake na kumnunua mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele.
Beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, anataka kusalia Roma wakati makubaliano yake ya mkopo yatakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Roma Press)
AC Milan ina matumaini ya kuafikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, katika klabu hiyo mwezi Januari. (Mail)
West Ham inafikiria kumsaini beki wakati wa Uhispania Unai Nunez, 22, kutoka Athletic Bilbao. (AS in Spanish)
Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham inafikiria kumsaini beki wakati wa Uhispania Unai Nunez, 22, kutoka Athletic Bilbao. (AS in Spanish)
Juan Sebastian Veron anasema kwamba kuna mazungumzo kati ya Estudiantes na kiungo wa kati wa Vissel Kobe Andres Iniesta kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 wa Uhispania kujiunga na klabu hiyo ya Argentine . (La Oral Deportivo, via Marca)
Mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo amewapatia wachezaji wake likizo ya siku ya Krismasi kwenda kujumuika na familia zao kabla ya mechi ya siku ya Ijumaa dhidi ya Man. (FourFourTwo)
TETESI ZA SOKA JUMANNE
Chanzo cha picha, Reuters
Kiungo wa kati wa man United paul Pogba
Real Madrid wamemwambia ajenti wa Paul Pogba Mino Raiola kwamba hawatomsaini kiungo huyo wa kati mwezi Januari.. (Mail)
Chelsea wamepewa fursa ya kumsaini Isco mwenye umri wa miaka 27 kwa dau la £44m na Real Madrid, hatua itakayotoa fursa kwa mabingwa hao wa Uhispania kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham Christian. (Mirror)
Beki wa Arsenal na Bosnia-Herzegovina Sead Kolasinac, 26, analengwa na Napoli pamoja na Roma. (Sky Sports)
Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wamepewa fursa ya kumsaini Isco mwenye umri wa miaka 27 kwa dau la £44m na Real Madrid
Mkufunzi mkuu wa RB Leipzig Oliver Mintzlaff amefichua kwamba wanapata shida kushindana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsaini mshambuliaji wa Norway Erling Haaland kutoka Salzburg. (Mail)
Tottenham watahitaji kulipa dau la £50m kumsaini beki wa Ufaransa Issa Diop mwenye umi wa miaka ,22, kutoka West Ham. (Express)
Spurs inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Lille Boubakary Soumare . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 pia analengwa na Manchester United. (L'Equipe - via Football 365)
Borussia Dortmund haitazuia uuzaji wa winga wa England Jadon Sancho, 19, mwezi Januari. (Bild)
Borussia Dortmund haitazuia uuzaji wa winga wa England Jadon Sancho, 19, mwezi Januari . (Bild)
AC Milan wameweka dau la £26m kwa kiungo wake wa kati Franck Kessie, huku Wolves ikifikiria kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 mwezi Januari.. (Calciomercato - in Italian)
Lyon inamnyatia kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24,. (L'Equipe - in French)
Atletico wameafikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa PSG na Uruguay Edinson Cavani, 32. (Star)
Chanzo cha picha, Reuters
Atletico wameafikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji wa PSG na Uruguay Edinson Cavani, 32. (Star)
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameungwa mkono kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, 33, kwa makubaliano ya muda mfupi. (Express)
Everton wameshauriwa kumsaini mshambuliaji wa Wolves na Mexico Raul Jimenez, 28, pamoja na mshambuliaji wa Southampton Danny Ings, 27. (Talksport - via Star)
Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anasema beki wa Croatia Filip Benkovic, 23, huenda akaondoka kwa mkopo mwezi Januari huku klabu ya Derby County. (Leicester Mercury)

Paul Pogba: Ole Gunnar Solskjaer amesema kiungo wa Manchester United haendi popote mwezi ujao
Maneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema Paul Pogba "hautauzwa Januari" na pia amekanusha madai kwamba alikutana na mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland.