Papa Francis: Mungu anawapenda hata wale wabaya kati yetu

Papa Francis

Papa Francis amefanya ibada ya kuziombea kulainika "nyoyo ngumu na zilizojaa ubinafsi" ili kusaidia kuondosha dhuuma duniani.

Hayo ameyasema katika hotuba yake ya Krismasi ama maarufu kama "Urbi et Orbi" ("Kwa Jiji na kwa Dunia") ambayo ameitoa moja kwa moja kutoka kwenye dirisha la Kanisa Mtakatifu Petro, Basilica jijini Vatican.

Papa amezungumzia juu ya kuta za tofauti ambazo watu wanajengewa na kuombea amani katika mataifa yaliyokumbwa na mabaa ya vita, mazingira na magonjwa.

Pia unaweza kusoma:

Katika hotuba hiyo ameyalenga mataifa ya Afrika ambayo Wakristo wamekuwa wakishambuliwa.

"Nawaombea ustahamilivu na amani wale wote wanashambuliwa kutokana na imani zao, hususani wamishenari na waumini ambao wametekwa na kwa wahanga wa mashambulio ya makundi yenye msimamo mkali, hasa katika nchi za Burkina Faso, Mali, Niger na Nigeria".

Shambulio la mkesha wa Krismasi nchini Burkina Faso limesababisha vifo vya watu 35 wengi wao wakiwa wanawake. Mamia ya watu wameuawa katika nchi hiyo katika miaka michache iliyopita, wakilengwa na makundi ya kijihadi.

Papa pia ameyataja maeneo mengine ambayo yameendelea kukabiliwa na machafuko kama Syria, Lebanon, Yemeni, Iraq, Venezuela, Ukraine na Palestina.

Kwa mabadiliko mema kutokea, amesema, watu inawapasa wawe na huruma.

"Namuomba [Mungu] alainishe nyoyo zetu ambazo kwa nyakati nyingi huwa ngumu na zilizojaa ubinafsi, na atengeneze njia za mapenzi yake. Na atujaalie tabasamu lake kweye sura zetu fakiri, kwa watoto wote wa dunia: wale ambao wametelekezwa na wale ambao wanateseka kwenye magomvi," amesema.

Je, Papa awali alisema nini?

Papa awali alikaribisha siku kuu ya Krisimasi kwa kusema kwamba Mungu anapenda kila mtu hadi wale wabaya kati yetu .

Alikuwa akizungumza na maelfu ya watu wakati wa mkesha wa siku kuu ya Krisimasi katika kanisa la St Peters Basilica mjini wa Vatican.

''Munaweza kuwa na mawazo ya finyu , unaweza kuwa umefanya mambo mabaya lakini Mungu anaendelea kukupenda'' , alisema.

Matamshi yake huenda yakachukuliwa na wengi kama yale yanayolenga kashfa zinazokumba kanisa hilo , ikiwemo visa vya unyanyasaji wa kingono , kulingana na mwandishi wa BBC.

Miongoni mwa wale wanaoshiriki katika ibada hiyo ni watoto waliochaguliwa kutoka mataifa kama vile Venezuela, Iraq, na Uganda.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Papa Francisi wikendi iliopita alizindua mabadiliko makuu katika eneo hilo ikiwemo kuondoa kiapo cha siri

Mwandishi wa BBC wa Rome Mark Lowen amesema kwamba hiyo ni ishara ya wazi kutoka kwa kiongozi huyo wa kanisa lenye takriban wafuasi bilioni 1.3 kote duniani ambao huzingatia matatizo yanayowakumba wahamiaji na waathiriwa wa vita mbali na kuwafikia wale walio pembeni.

"Krismasi inatukumbusha kwamba Mungu anaendelea kutupenda sisi sote licha ya kwamba kuna waliofanya mabaya kati yetu, anasema.

''Nawapenda na nitaendelea kuwapenda kwa kuwa ninyi muna thamani kubwa mbele ya macho yangu'' , alisema kiongozi huuyo wa dini akiwa na umri wa miaka 83.

''Mungu hakupendi kwa sababu unafikiria na kufanya kile anachotaka . Anakupenda vile ulivyo. Mapenzi yake kwenu hayana masharti na hayategemei ulivyo''.

Papa pia alizungumzia kuhusu kashfa za kifedha na unyanyasaji unaokumba kanisa hilo.

''Chochote tunachokosea katika maisha yetu , chochote ambacho hakifanyiki vyema katika kanisa , matatizo yoyote yaliopo duniani hayatatumiwa kama sababu''.

Je alinaamisha nini?

Kutoka katika miji ya Australia hadi katika shule na Marekani kote, kanisa katoliki limekumbwa na msururu wa unyanysaji dhidi ya watoto katika miongo kadhaa iliopita.

Kesi za kiwango cha juu na ushahidi uliotolewa katika uchunguzi unaofanywa umeendelea kuweka swala hilo katika vichwa vya vyombo vya habari.

Maelezo ya picha,

George Pell ni miongoni mwa viongozi wakuu wa kanisa hilo waliohukumiwa kwa unyanysaji wa watoto

Katika visa vya hivi karibuni Kadinali George Pell alihukumiwa kwa kuwanyanyasa wavulana wawili wa kwaya mjini Melbourne mwaka 1999

Ni kiongozi wa hadhi ya juu nchini Australia kutoka katika kanisa hilo na awali alikuwa mweka hazina wa Vatican ikimaanisha kwamba alikuwa akionekana katika kanisa hilo kama afisa mkuu wa tatu kwa hadhi.

Wiki iliopita , Papa alianzisha mabadiliko muhimu ili kuondoa kiapo cha siri katika kanisa hilo ambacho kimeingilia unyanyasaji wa watoto.

Kanisa hilo lilikuwa likiangazia kesi za unyanyasaji wa kingono kwa siri kubwa , katika kile ilichosema zilikuwa juhudi za kulinda faragha za waathiriwa na sifa za watuhumiwa.

Lakini stakhabadhi mpya za papa huyo zimeondoa masharti hayo kwa wale wanaoripoti unyanyasaji huo