Ole Gunnar Solskjaer: Manchester United bado haijafikia matarajio yangu

Ole Gunnar Solskjaer

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Ole Gunnar Solskjaer alianza vyema akiwa kocha wa muda, lakini mambo yakawa magumu alipopewa mkataba wa moja kwa moja.

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kuwa klabu hiyo bado iko nyuma kinyume na matarajio aliyokuwa nayo katika kipindi kama hiki cha msimu.

United, ambayyo itakuwa mwenyeji wa Newcastle siku ya Boxing Day, inashikilia nafasi ya nane katika Ligi ya Primia na iko nyuma kwa pointi saba kuufikia mstari wa timu bora nne za juu.

Solskjaer amekuwa mkufunzi wa timu hiyo kwa mwaka mmoja lakini anasema anatumia msimu huu kuunda kikosi cha msimu ujao.

"Tulijua kwamba msimu huu utakuwa na panda shuka nyingi," anasema.

"Msimu huu utatumika kusuka kikosi cha msimu ujao, lakini ni matumaini yetu kwamba tutafanikiwa kuharakisha kwa kupata matokeo bora.

"Natarajia kwamba tutaendeleza matokeo bora, kupata tajriba zaidi na pia tunaendelea kujifunza kutokana na changamoto zote.

"Kwa sasa tuko nyuma kiasi kuliiko vile nilivyokuwa nikitarajia."

Kiungo nyota Paul Pogba, ambaye majeraha yamekuwa yakimuandama toka Septemba aliingia kama mchezaji wa akiba wakati United ilipochapwa mabao 2 na Watford siku ya Jumapili.

Solskjaer anasema kwamba Pogba ndio kiungo bora zaidi duniani na huenda akashiriki katika mechi ya United dhidi ya Newcastle Alhamisi hii.

"Anaweza kucheza popote. Anaweza kukaba na kushambulia a anaweza kuhamisha uwanja kwa pasi ndefu," ameongeza mkufunzi huyo raia wa Norway.

"Bila shaka hayo ni mazungumzo kumhusu Pogba ambayo yataendelea. Na ni vizuri kuona kwamba amerejea."

Pia unaweza kusoma: