Sherehe za Krismasi duniani kwa picha

Kutoka barani Afrika hadi Australia, misa na sherehe mbalimbali zimekuwa zikifanyika kuadhimisha moja ya siku takatifu katika kalenda za dini ya kikristo. Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa sehemu mbali mbali duniani.

Kenya

Chanzo cha picha, Reuters

Jijini Mombasa misa ilifanyika usiku wa manane katika eneo maarufu la Fort Jesus.

Jijini Nairobi mchana watu wakajitokeza kwenye viwanja vya bustani ya Uhuru kusherehekea na familia zao.

Pia ilikuwa fursa nzuri kwa wafanyabiashara kwenye eneo hilo.

Khartoum, Sudani

Chanzo cha picha, EPA

Misa ya krismasi ikisherehekewa katika kanisa kuu la mtakatifu Mathayo ndani ya mji mkuu wa Sudani.

Colombo, Sri Lanka

Chanzo cha picha, EPA

Watoto wa kikatoliki nchini Sri Lanka wakiwa wamevaa kama malaika katika kanisa la mtakatifu Anthony. Katika Jumapili ya pasaka, kanisa hilo lilikuwa la tatu kulengwa na watu waliovaa mabomu ya kujitoa muhanga, watu 54 walifariki dunia hapa, na zaidi ya watu 300 katika sehemu nyingine za nchi hiyo.

Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu

Chanzo cha picha, EPA

Muumini akiwasha mshumaa katika kanisa kuu la mtakatifu Joseph. Falme za Kiarabu ina jamii imayokua ya kikatoliki, huku Wafilipino wakiwa ni asilimia tano ya idadi ya watu wote.

Hanoi, Vietnam

Chanzo cha picha, AFP

Mwanamke mmoja akijipiga picha nje ya kanisa kuu la mtakatifu Joseph katika mji mkuu wa Vietnam.

Paris, Ufaransa

Chanzo cha picha, EPA

Askofu Pilippe Marsset akiendesha misa ya usiku katika kanisa la mtakatika Germain l'Auxrrois. Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 200, Misa ya krismasi haikufanyika katika kanisa kuu la Notre-Dame baada ya moto mkali kutokea mwezi Aprili mwaka huu.

Bethlehem, Palestina

Chanzo cha picha, EPA

Misa ya usiku ikiendelea katika mji wa Magharibi wa Bank ambako Biblia inasema ndipo Yesu alipozaliwa.

Mji wa Vatican

Chanzo cha picha, AFP

Katika misa yake ya saba ya krismasi, Papa Francis amesema Mungu aliwapenda hata wale walio wabaya kati yetu, ujumbe unaoweza kutafsiriwa kuwa unahusu matatizo ya kanisa.

Aleppo, Syria

Chanzo cha picha, AFP

Misa ya krismasi ya asubuhi ikiendelea katika kanisa la orthodox katika mji wa vita wa Aleppo nchini Syria. Jamii ya kikristo nchini humo ni moja jamii za zamani duniani, ukiridu nyuma hadi milenia mbili. watu wa wengi jamii hii hutokea katika madhehebu ya mashariki. Kanisa la Orthodox la Kigiriki, Kanisa la kitume la Kiarmenia na kanisa la Orthodox la Syria.

Baghdad, Iraqi

Chanzo cha picha, EPA

Nchini Iraqi, wakristo wamehudhuria misa ya krismasi katika kanisa la kianglikana la mtakatifu George, wakati huo huo maandamano yanayoipinga serikali, yaliyoanza mwezi Oktoba yakiendelea. Baadhi wanakadiria kuwa jamii ya kikristo nchini humo imepungua kutoka milioni 1.5 mwaka 2013, hadi kufikia 250,000.

Sydney, Australia

Chanzo cha picha, EPA

Katika siku kuu za krismasi picha hii imeonekana mjini Sydney ikimkashifu waziri mkuu Scott Morrison kwa kuchukua likizo ya kwenda Hawaii wakati nchi hiyo ikipambana na moto wa msituni.

Picha zote zina hatimiliki