Wakristo wanaolazimika kuadhimisha Krismasi msituni

Wakristo wanaolazimika kuadhimisha Krismasi msituni

Wakristo wa Jimbo la Aceh, Indonesia wanaadhimisha Krismasi kwenye mahema katikati ya msitu.

Makanisa yao yalishambuliwa na kuvunjwa mwaka 2015 na makundi ya waislamu na mamlaka za eneo hilo. Mamlaka hizo pia zinadai wakristo hao hawana kibali cha kujenga upya nyumba zao za ibada.

Indonesia ndiyo taifa lenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani, taifa hilo lina katiba inayoruhusu uwepo wa dini mbalimbali. Lakini hata hivyo, stahmilivu na masikilizano ya kidini yamekuwa ni ya kuzorota katika miaka ya hivi karibuni.