Ni jambo gani unatamani wazazi wako wangekufanyia ?

Binti wa Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati tunawakuza watoto wetu, jambo muhimu ambalo huwa tunaangalia na kuvutiwa nalo ni wazazi wetu. Hii ina maana, huwa tunataka kuwakuza watoto wetu kama jinsi tulivyokuzwa na wazazi wetu.

Kitabu cha hivi karibuni kilichoandikwa na mwanasaikolojia Philippa Perry ambacho kimetoa muongozo wa malezi, kitabu kinaitwa 'The Book You Wish Your Parents Had Read'.

Kitabu hiki kimeeleza namna wazazi wanaweza kuwalea watoto na kuwapa msingi bora.

Mambo muhimu ambayo mzazi anapaswa kuzingatia ni pamoja na:

1. Kuweka mipaka

Huwa si jambo rahisi kwa sababu unampenda mtoto wako na unataka umpatie kila kitu, lakini inafikia wakati ambao kuna kikomo.

Hata kama unahisi kuwa wewe ni mzazi ambaye una kila kitu unakihitaji duniani, bado unahitaji kuweka mipaka.

Ni namna gani unaweza kuweka mipaka kwa njia ya upendo? Jibu ni, kujijibu wewe mwenyewe wakati unasema sentensi yako na sio kusema kuwa wewe mtoto unapaswa kufanya nini?

Hii ikiwa ina maana kwamba , "Ninajua unataka kupanda basi kwenda mjini usiku lakini siwezi kukuruhusu kufanya hivyo."

Badala ya kusema: "Hapana wewe una miaka 13, bado mdogo sana."

Hakuna mtu ambaye anapenda kuelezewa , hivyo unapaswa kujieleza nafsi yako mwenyewe na sio mtoto.

Maelezo ya picha,

Kuweka mipaka ni jambo muhimu

2.Unapaswa kuelewa tabia zote ambazo mtoto wako huwa nazo

Tatizo huwa linakuja kwa wazazi ni kuwa tunataka watoto wetu wawe na furaha kila wakati.

Hiii ni kutokana na mapenzi tulionayo kwao kupita kiasi, huwa hatupendi kuwaona wanasikitika , hivyo huwa tunasema : "Usikasirike."

Lakini ni muhimu sana kuwapa mwanya kujisikia vyovyote na kuelewa hali waliokuwa nayo kwa wakati husika.

Tunapaswa kuelewa kuwa wana hisia ya kufurahi na kukasirika wanapopata hasira.

3. Kumbuka kuwa wewe ni kioo cha mtoto wako

Kumbuka kuwa wewe ni kama kioo cha mtoto wako. Namna ambavyo tunawajibu watoto wetu ndio namna tunavyowajenga.

Kama mara nyingi huwa unawaongelesha kwa hasira, hivyo wataona sura yako ikiwa imekasirika na wao kuiga.

Hivyo unapaswa kujua namna gani unaweza kuzungumza vizuri na mwanao.

Jaribu kuwa mkarimu kwao.

Maelezo ya picha,

Hata kama mtoto wako amekosea , sio lazima kumuonyesha mtoto wako sura ya hasira

4. Tabia zote ni mawasiliano

Kama mtoto wako ana tabia ya ukorofi kumbuka kuwa : Tabia zote ni mawasiliano.

Kile ambacho mtoto wako anafanya ni kujaribu kuwasiliana namna nzuri ambayo anaifahamu.

Hivyo unapaswa kufahamu sababu zinazomfanya mwanao kuwa na tabia hizo na namna gani unaweza kumsaidia kuachana na tabia hizo ambazo hazipendezi , kwa kumueleza kwa namna nzuri.

Tunapaswa kuzikubali hisia zote , hata kama tunaziona kuwa hazieleweki.

Tunapaswa kuwasaidia watoto wetu kuwa waangalifu na hisia zao na kama mtu mwingine akifanya hivyo kwao watajisikiaje.

Kila mtu yuko tofauti.

Maelezo ya picha,

Kumbuka kuwa kila mtu yuko tofauti

5.Mtoto wako sio mradi au kazi

Kama nikikwambia kitu kimoja, itakuwa hivi: "Mtoto wako sio kazi ambayo umepewa unapaswa kuimaliza, sio mradi ambao unapaswa kuwa mzuri.

Mtoto wako ni mtu ambaye una uhusiano naye."

Kama mtoto wako ni mwembamba au kibonge, bado ni mtu.