Kesi inayomkabili Trump: Seneta wa Republican akerwa na msimamo wa wenzake

Lisa Murkowski

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Lisa Murkowski ametaja ksi hiyo kama 'ilioharakishwa'

Seneta wa Republican Lisa Murkowski amesema kwamba amekerwa na msimnmo wa chama chake kabla ya kesi inayomkabili rais Donald Trump kuwasilishwa katika bunge la seneti nchini humo.

Rais Trump alishtakiwa katika bunge la uwakilishi linalotawaliwa na wabunge wa Democrat kwa utumizi mbaya wa mamlaka na kulizuia bunge la Congress.

Kwa sasa anakabiliwa na kesi hiyo katika bunge la seneti linalotawaliwa na wanachama wengi wa chama cha Republican - ambao wanatakiwa kutopendelea upande mmoja.

Hatahivyo seneta wa walio wengi katika bunge hilo la seneta Mitch McConnel ameahidi kushirikiana na ikulu ya Whitihouse.

Bwana Trump , ni rais wa tatu kushtakiwa katika mabunge hayo , hatahivyo hakuna uwezekano wa kumuondoa madarakani kutokana na wingi wa Republicans katika bunge hilo.

Rais huyo ametaja mchakato wa kesi hiyo kama uwindaji wa kisiasa.

Je bi Murkowski alisemaje?

Bi Murkowski aliambia chombo cha habari cha Alaska KTUU kwamba hafurahii jinsi bwana McConnel anavyotoa matamshi ya ushirikiano na Ikulu ya Whitehouse.

''Niliposikia hilo nilikerwa sana'', alisema.

Seneta huyo pia alisema kwamba kunahitajika kuwepo na uwazi na kutoshirikiana kati ya bunge la seneti na Ikulu ya Whitehouse kuhusu jinsi kesi hiyo itakavyoandaliwa.

''Kwangu mimi inamaanisha kwamba tunahitaji kurudi nyuma na kutopendelea upande unaojitetea'', alisema. Hatahivyo aliutaja mchakato wote wa kesi hiyo kama ule ulioharakishwa.

Bi Murkowski , mwanachama wa Republican mwenye msimamo wa kadri , amemkosoa Trump kuhusu sera kadhaa. Mwezi Oktoba 2018, aliamua kutounga mkono uteuzi wa Trump wa mahakama ya kilele , kufuatia madai ya unyanyasaji wa kingono.

Jukumu la McConnel ni lipi?

Bwana McConnel atachukua jukumu muhimu katika kesi hiyo- ambayo inatarajiwa kutopendelewa -wakati itakapofanywa.

Lakini alisema wazi wiki iliopita kwamba yeye sioi jaji asiyependelea katika mchakato huo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mitch McConnell ana matumai kwamba rais Trump ataondolewa mashtaka s confident that President Trump will be acquitted

"Huu ni mchakato wa kisiasa. hakuna kinachohusisha mahakama ndani yake . kesi ya kutaka kumuondoa raisi ni uamuzi wa kisiasa'', alisema.

Bwana McConnel pia alisema kwamba alikuwa na matumaini kwamba rais Trump ataondolewa mashtaka hayo katika bunge la seneti linalodhibitiwa na wanachama wa Republican.

''Tutakuwa na matokeo yatakayopendelea upande mmoja'', alisema.

Viongozi wa Republican na wenzao wa Democrat katika bunge le seneti mara kwa mara wamezozana kuhusu kanuni za kesi hiyo.

Democrats wanataka hakikisho na stakhabadhi kuruhusiwa ili kuwezesha kile wanachokitaka kuwa kesi ya haki.

Bwana McConell amekataa kuwasilishwa kwa mashahidi ili kutoa ushahidi wakati wa kesi hiyo.

Je Trump alisema nini?

Katika msururu wa jumbe za twitter, rais aliwashutumu wabunge wa Democrats kwa kukataa kuendelea na kesi hiyo kwa kuwa ''kesi yao ilikuwa mbaya''.

Alituma ujumbe wa twitter akisema; Baada ya Democrats kukataa kunipa haki yangu bungeni, bila kuwa na wakili bila mashahidi, sasa wanataka kuliambia bunge la seneti jinsi ya kuendesha kesi hiyo.

''Kwa kweli hawana thibitisho la chochote, Na pia hawatakuwepo .Nataka kesi hiyo kufanyika sasa hivi!''

Kwa nini kuna mkwamo kuhusu kuanza kwa kesi hiyo?

Ili kesi hiyo kuanza bunge la uwakilishi linalodhibitiwa na Democrats ni sharti liwasilishe nakala za kesi hiyo kwa bunge la seneti.

Lakini spika wa bunge la uwakilishi Nancy Pelosi amekataa kufanya hivyo hadi pale sheria za kesi hiyo za seneti zitakapokubaliwa na Democrats.

Maelezo ya picha,

Ili kesi hiyo kuanza bunge la uwakilishi linalodhibitiwa na Democrats ni sharti liwasilishe nakala za kesi hiyo kwa bunge la seneti. Lakini spika wa bunge la uwakilishi Nancy Pelosi amekataa kufanya hivyo hadi pale sheria za kesi hiyo za seneti zitakapokubaliwa na Democrats.

Kiongozi wa Republican katika bunge la seneti Mitch McConnell, ataamua masharti ya kesi hiyo na Democrats wanamtaka kutoa maelezo kuhusu mashahidi na ushahidi utakaoruhusiwa.

Bwana McConnel amekataa kukubaliana na Democrats: Tunasalia katika mkwamo, alisema, baada ya mkutano mfupi na kiongozi wa walio wachache wa Democrats Chuck Schumer.

Bwana McConnel ana idadi kubwa ya wabunge wa Republican katika bunge hilo.

Kuna wabunge 53 wa Republican katika bunge hilo lenye viti 100 na kwa kura hiyo kumuondoa madarakani.

Trump anakabiliwa na shutuma gani?

Kama matokeo ya uchunguzi yatapatikana, chama cha Democratic kinasema Bw Trump alitoa misaada miwili ya kijeshi yenye thamani ya dola milioni 400 za Kimarekani ambazo tayari zilikuwa zimeshapangwa na bunge, na mkutano na rais Volodymyr Zelensky.

Chama cha Democrat kinasema shinikizo hili kwa mshirika wa Marekani linaonesha matumizi mabaya ya madaraka.

Uchunguzi wa kwanza ambao BwTrump aliutaka kutoka kwa Ukraine ulikuwa unahusu makamu wa rais mstaafu Joe Biden, ambaye ni mpinzani wake mkubwa kutoka chama cha Democratic na mtoto wake Hunter.

Hunter Biden alijiunga na baraza la kampuni ya nishati la Ukraine, pale baba yake alipokuwa makamu wa rais mstaafu Barack Obama.

Kitu cha pili ambacho Trump alitaka ni Ukraine kujaribu kurekebisha njama zinaonyesha kuwa Ukraine na sio Urusi ndio walioingilia uchaguzi mkuu uliopita wa Marekani.

Nadharia hii ilikuwa dhaifu, na vyombo vya uchunguzi nchini Marekani vimeficha kusema kuwa Moscow ndio waliofanya udukuzi wa barua pepe mwaka wa 2016.

Je kuna namna yoyote ambayo rais atapatwa na hatia?

Ni viongozi wachache wa Marekani ndio walifikia katika hatua ya namna hii. Kwa kuwa chama cha upinzani cha Democratic kina wingi wa wawabunge, kuna uwezekano kuwa Trump ataondolewa mashtaka.

Democratic wanataka kura hiyo ipigwe kabla ya mwisho wa mwaka.