Mwana wa Bruce Lee aushtaki mgahawa kwa kutumia picha ya babake

Watu wanatembea nje ya mgahawa huo wa Real Kungfu ama Zhen Gongfu , unaondeshwa na mgahawa wa Kungfu Catering Management mjini Beijing.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Watu wanatembea nje ya mgahawa huo wa Real Kungfu ama Zhen Gongfu , unaondeshwa na mgahawa wa Kungfu Catering Management mjini Beijing.

Kampuni inayosimamiwa na mwana wa kike wa Bruce Lee imeushtaki mgahawa mmoja maarufu nchini China kwa kutumia picha ya nyota huyo wa karate.

Kampuni hiyo kwa jina Bruce Lee Enterprises inadai kwamba Real Kungfu ilitumia picha hiyo katika nembo yake bila ruhusa.

Kampuni hiyo inataka mgahawa huo kuondoa picha hiyo mara moja na inataka kulipwa fidia ya

$30m.

Hatahivyo mgahawa huo unahoji kwamba serikali ya mitaa ya eneo hilo iliidhinisha utumizi wa nembo hiyo.

Picha hiyo ina mwanamume mwenye nywele nyeusi akiwa amesimama.

''Nembo ya mgahawa huo wa Real Kungfu ni nembo ambayo kampuni hiyo iliwasilisha ombi na kupatiwa baada ya ukaguzi wa kiwango cha juu uliofanywa na shirika la utoaji nembo, tumekuwa tukiitumia kwa takriban miaka 15 kufikia sasa'', kampuni hiyo ilisema katika taarifa yake iliochapishwa katika mtandao wa kijamii wa Weibo.

''Tumeshangaa kwamba baada ya miaka mingi sasa tunashtakiwa, tunaisoma kesi hii kwa nguvu na kuandaa kutoa jibu let''.

Mgahawa huo wa chakula uliopo katika mji wa Guangzhou unaojulikana kama Zhen Gongfu kwa lugha ya Mandarin ulianzishwa 1990 na sasa una zaidi ya matawi 600 nchini China.

Kampuni ya Bruce Lee Enterprises inasimamia biashara na haki za picha ya Bruce Lee.

Katika taarifa katika tovuti yake , kampuni hiyo ilisema imechukua jukumu la kuendeleza sanaa na filosofia ya Bruce Lee ili kushinikiza ukuaji wake na maelewano duniani kwa lengo la kuendeleza mafanikio ya nyota huyo.

Kampuni ya Bruce Lee Enterprises haikutoa tamko lolote ilipotakiwa kufanya hivyo.

Kesi hiyo huenda ikafuatiliwa kwa karibu baada ya serikali ya China kuahidi kulinda haki miliki