Rais wa Urusi Vradimir Putin aikemea Poland

Russian President Vladimir Putin (C) and Russian Defence Minister Sergei Shoigu (L) take part in the annual meeting of the Defence Ministry board,

Chanzo cha picha, Sputnik/AFP

Maelezo ya picha,

Kiongozi wa Urusi ameikemea Poland katika kauli zake za hivi karibuni

Wakati maafisa wa ngazi ya juu wa Urusi walipokua wakitathmini kwa ufupi matokeo ya mafanikio ya 2019, mada moja ilijitokeza katika matangazo ya rais Vladimir Putin: Poland na nafasi yake katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Katika kipindi cha siku saba, alitaja sio chini ya mara tano suala hili katika mikutano muhimu - baadhi yake ikiwa hata haihusiani na historia au hata sera ya kigeni.

Katika hatua ambayo haikua ya kawaida alipokua akihutubia bodi ya wizara ya ulinzi tarehe 24 Disemba alimuelezea balozi wa Poland kwa Wanazi wa Ujerumani kama "kashfa na nguruwe anayepinga wayahudi".

Saa mbili baadae, akazungumzia mada hiyo tena katika mkutano na viongozi wa bunge. Spika wa bunge la Urusi (Duma) Vyacheslav Volodin alimshukuru rais Putin na akadai Poland iombe msamaha kwa Urusi.

Unaweza pia kusoma:

Siku iliyofuata, rais Putin alifanya mkutano wa mwisho wa mwaka na wafanyabiashara muhimu wa Urusi. Kwa mujibu wa jarida la Forbes la lugha ya Kirusi, ''pia alimshangaza kila mmoja kwa namna alivyojikita katika masuala ya kihistoria yanayohusiana na Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na mahusiano na Poland.''

Pia anapanga kuandika taarifa juu ya suala hili.

Lakini ni kwanini amekuwa na hasira hii ya ghafla na Poland?.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mkutano na viongozi wa biashara ulifanyika katika ofisi ya Waziri Mkuu - Kremlin

Ukosoaji wa Poland wa Putin unafuatia azimio la bunge la Muungano wa Ulaya lililolaumu kwa pamoja Muungano wa Usovieti na Wanazi wa Ujerumani kwa kusababisha Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Kwa mujibu wa rais wa Urusi, kujumuisha pande hizo mbili ni " mtizamo mbaya wa hali ya juu", na kwa mara nyingine tena alitoa kauli ambayo wakosoaji wake wanaiita "ukosoaji usio na msingi " ambapo alijaribu kuigeuzia lawama Poland.

Mara nyingi Muungano wa Usoviet umekua ukishutumiwa kwa kuihusisha Poland na Wanazi wa Ujerumani kutokana na mkataba waliousaini na Hitler wa kutochokozana (unaofahamika kama mkataba wa Molotov-Ribbentrop ).

Lakini ni kwanini Putin anakasirishwa na shutuma dhidi ya nchi ambayo haipo tena?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mkataba kati ya Ujerumani na Muungano wa Usovieti ulisainiwa mwaka 1939

Ushindi wa USSR katika Vita vikuu vya Dunia ni moja ya mihimili mikuu miwili ya fikra za taifa, na zaidi ya miaka 70 baada ya vita hivyo bado unasherehekewa kwa sherehe fupi kila mwaka .

Pia ni njia muhimu ya rais Puntin ya kujihalalisha na kupanua zaidi sera yake ya kigeni kama mrithi wa ufalme wa Usovieti.

Kwa hiyo utawala wa Kremlin unaona ukosoaji wowote wa kile kinachofahamika nchini Urusi kama Ushindi Mkubwa kama shambulio dhidi yake.

Katika yote haya , hakuna sababu ya kutosha kwa Poland kukubali shutuma ambazo imezielezea kama '' simulizi za uongo''

Ni mada inayochukuliwa kwa umakini sana nchini Poland, ambayo ilikana kushiriki katika vita vya uhalifu vya Nazi mwaka 2018. Kufuatia malalamiko, sheria ililainishwa ili kuifanya iwe sheria ya kiraia na sio kosa la jinai.