Makundi ya setilaiti: Wanajimu waonya kwamba huenda ikawa hatari kuutazama muonekano wa dunia

Starlink satellite trail

Chanzo cha picha, Marco Langbroek/SatTrackCam Leiden

Maelezo ya picha,

Wana anga wana wasiwasi kwamba setilaiti zinazonga'aa kupita kiasi huenda zikaathiri utafiti

Wanajibu wanaonya kwamba huenda mtizamo wao wa dunia ukaathirika.

Kuanzia wiki ijayo, kampeni ya kurusha maelfu ya satelaiti mpya itaanza na kutoa fursa ya kuongezeka kwa kazi ya mtandao kutoka kwenye anga ya juu.

Lakini vyombo vya angani za juu kwanza ambavyo tayari vimesharushwa kwenye mzunguko wa dunia na kampuni ya moja ya anga za juu ya Marekani kunaathiri muonekano wa anga la usiku.

Muonekano wa anga hilo unajitokeza ukiwa na mistari ya rangi nyeupe, weupe wake unang'aa sana kiasi cha kushindana na nyota.

Wanasayansi wana wasiwasi kwamba kundi la nyota la setilaiti linaweza kuficha picha zinazoonekana kupitia darubini na kuingiliana na uangalizi wa kupitia astronomia ya redio.

Daktari Dave Clements, mwanafizikia wa anga kutoka chuo cha Imperial College London, ameiambia BBC kwamba: "Anga la usiku ni raslimali na kile kinachoendelea ni tishio kwa raslimali hii."

Kampuni zenye kuhusika zimesema kwamba zinashirikiana na wana anga kupunguza athari za setilaiti.

Kwanini setilaiti nyingi zinarushwa kwenye anga?

Sababu kuu ni kuongeza kasi ya mtandao.

Badala ya kutimia nyaya na setilaiti inawezesha upatikanaji wa mtandao duniani kutoka kwenye anga la juu.

Na iwapo kutakuwa na setilaiti nyingi kwenye mzunguko wa dunia, inamaanisha kwamba hata maeneo ya vijijini yanaweza kupata mtandao.

Chanzo cha picha, ONEWEBB

Maelezo ya picha,

kundi la setilaiti zilizonaswa na kampuni ya OneWeb kwa umbali wa kilomita 1,200 juu ya dunia

Nikufahamishe tu kwamba kwa sasa hivi kuna setilaiti 2,200 kwenye anga la dunia.

Lakini kufikia wiki ijayo, kundi la setilaiti - mradi wa kampuni ya anga za juu ya Marekani itaanza kutuma makundi ya setilaiti 60 kwenye mzungumzo wa dunia kila baada ya wiki kadhaa. Hii itamaanisha kwamba karibia setilaiti 1,500 zitakuwa zimerushwa kwenye anga ifikapo mwaka ujao, na kufikia katikati ya miaka ya 2020, huenda kukawa na kundi la setilaiti 12,000.

Kampuni moja ya Uingereza ya OneWeb inalenga kurusha setilaiti 650 - lakini idadi hii huenda ikaongezeka hadi 2,000 iwapo kutakuwa na wateja wengi.

Wakati tayari Amazon imepanga kurusha kundi la setilaiti 3,200 kwenye anga la dunia.

Kwanini wana anga wana wasiwasi?

Mei na Novemba, kampuni ya anga za juu ya Marekani ya Starlink, ilituma setilaiti 120 kwenye mzunguko wa dunia chini ya kilomita 500.

Lakini wataalam wa mambo ya angani walikuwa na wasiwasi baada ya chombo cha angani kuonekana kikiwa kinang'aa mnoo kwa miale meupe kupitia darubini.

Chanzo cha picha, Gemini Observatory/ NSF

Maelezo ya picha,

Kituo cha uangalizi wa nyota cha Gemini kilinasa kundi la nyota

Dhara Patel, mwana anga wa Royal Observatory Greenwich alisema: " Setilaiti zina ukubwa sawa na meza lakini zinaweza kuakisi na paneli zake zinaakisi mwanga mwingi wa jua, kumaanisha kwamba tunaweza kuona nyota kwa muonekano wa picha zinazotazamwa kupitia darubini."

"Setilaiti hizi pia zinatumia sana mawimbi ya redio ... na hilo lina maanisha kuwa zinaweza kuingiliana na mawimbi yanayotumiwa na wana anga. Hivyo basi pia kunaathiri astronomia ya redio."

Patel, anaonya kwamba tatizo hilo litazidi kadiri setilaiti zitakavyoongezeka kwenye mzunguko wa dunia.

Je hili lina maanisha nini kwa watafiti?

Dakta Clements anaamini kwamba kunaweza kuwa na athari kwa wana anga.

"Wanawakilisha eneo lililo karibu kati ya kile tunachoona kutoka duniani na kwengine ulimwenguni. Kwa hiyo wanaingilia kila kitu.

"Na utakosa kuona kile kilicho nyuma yao, ama iwe nyota ndogo hatari au kwasari ya mbali kabisa duniani."

Dr. Clement anasema kwamba itakuwa tatizo kubwa kabisa kwa darubini zinazoangalia mandhari kubwa ya angani kama ile iliyotumika Chile.

Anaelezea: "Kile tunachotaka kufanya ni kwa darubini kutazama anga kubwa na nyenginezo na kupata picha zenye uhalisia wa namna anga inayobadilika...

"Lakini kwa sasa tuna setelaiti hizi ambazo zinaingiliana na utazamaji wa anga sasa hivi ni kama mtu anatembea akiwasha globu yenye kuwaka kama radi kila wakati."

Unaweza pia kusoma:

Lakini Profesa Martin Barstow, mwanafizikia wa anga kutoka Chuo Kikuu cha Leicester anasema baadhi ya matatizo yanaweza kutatuliwa.

"Idadi ya setilaiti hutoa sauti za kuogofya lakini ukweli ni kwamba anga ni kubwa - kwa hiyo unazirusha moja juu ya nyengine kwenye anga, uzito wake hautakuwa mkubwa," anasema.

"Itakuwa kazi nyingikwa wana anga na nguvu kubwa itatumika lakini ni jambo ambalo linaweza kufanyika."

Hata hivyo kwa astronomia ya redio, kundi la nyota linaweza kuwa tatizo - hasa kwa darubini mpya kama vile ile ya Square Kilometre Array (SKA).

Redio inaashiria kwamba matumizi ya setilaiti yatakuwa tofauti ikilinganishwa na yale yanayotafutwa na wana anga lakini pia yanaweza kuingilia shughuli hiyo, Profesa Barstow amesema.

Je kampuni husika zinasema nini?

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kampuni ya SpaceX inalenga kuunda setilaiti zisizo na mwanga mwingi