Kundi la Islamic State nchini Nigeria 'limewakata vichwa mateka Wakristo'

Screen grab from previous Iswap video (2015)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Baadhi ya wafuasi wa kundi la Kiislamu la Boko Haram kwa sasa wanaendesha harakati zao chini ya kikundi kinachoitwa "Islamic State West Africa Province"

Kundi la Islamic State limetoa video linayodai inaonyesha mauji ya Wakristo 11 nchini Nigeria.

IS linasema kuwa mauji hayo ni sehemu ya kampeni yao ya hivi karibuni ya "kulipiza kisasi cha mauaji ya kiongozi wake na msemaji nchini Syria.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuwahusu wahanga, ambao wote walikua ni wanaume, lakini inasema walikua "wamekamatwa katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita" katika jimbo la kaskazini-mashariki mwa Nigeria la Borno.

Video hiyo ya dakika 56-ilitolewa na ''shirika la habari ''la IS Amaq.

Video hiyo imetolewa tarehe 26 Disemba na wachambuzi wanasema ni wazi imetolewa kwa makusudi katika kuambatana na sherehe za Christmas.

Picha ilichukuliwa katika eneo la wazi lisilojulikana.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

IS wamedai kuwa mauaji ya Wakristo 11 yanalenga kulipiza kisasi cha kifo cha kiongozi wao- Abu bakr al Baghdadi nchini Syria

Mmoja wa mateka aliyekua katikati anaonekana akipigwa risasi na kufa huku wengine 10 wakisukumwa ardhini na kukatwa vichwa.

Viongozi wa IS na msemaji alieuawa Abu Bakr al-Baghdadi na Abul-Hasan Al-Muhajir waliuawa nchini Syria mwishoni mwa mwezi wa Oktoba...Je Abu Bakr al-Baghdadi alikuwa nani?

Unaweza pia kusoma:

Awali IS ilitoa video ambayo mwandishi wa habari wa Nigeria Ahmad Salkida, anaamini ilikua na uhusiano na nyingine tofauti ya wapiganaji wa jihadi iliyoripotiwa kutolewa na kiongozi wa Boko haram Abubakar Shekau alidai 'Yesu sio mtoto wa mungu'. Shekau kwa mara nyingine tena aliripotiwa kuwatishia Waislamu na Wakristo wanaounga mkono mawazo huru.

Karibu miezi miwli baadae, tarehe 22 Disemba IS ilitangaza kampeni mpya ya wanamgambo hao "kulipiza kisasi " cha mauaji yao na tangu walkati huo wamedai kuendesha mashambulio katika nchi mbali mbali chini ya kampeni hiyo.

Tawi moja la kundi hilo la wanamgambo wa Boko Haram kwa sasa wa apigana chini ya jina "Jimbo la Kiislamu la Afrika Magharibi " (Iswap).Mwaka jana Iswap liliwauwa wakunga wawili ambao lilikua limewateka nyara.