Maisha baada ya kifo: Simulizi ya watoto saba walioganda mpaka 'kufa' na 'kufufuka'

Maisha baada ya kifo: Simulizi ya watoto saba walioganda mpaka 'kufa' na 'kufufuka'

Mwaka 2011, ziara ya kimasomo ya watoto wa shule moja nchini Denmark iliingia mkosi. Kundi la watoto lilitumbukia kwenye maji yaliyoganda na 'kufa'. Mioyo yao iliacha kudunda kwa saa kadhaa. Hiki ni kisa kikubwa cha aina yake kinachofahamika ambapo watoto wote hao saba walirejea kutoka 'kuzimu'.