Polisi Brazil inachunguza Bomu lilorushwa ofisi iliyotengeneza filamu ya Yesu mwenye mahusiano ya jinsia moja

kundi la waigizaji Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kundi hili la waigizaji wamewahi kushinda tuzo za filamu za emmy

polisi nchini Brazili wanachunguza mkasa wa ofisi ya uzalishaji wa filamu iliyolipuliwa kwa bomu mjini Rio de Janeiro kwa sababu ya filamu yake inamuhusisha Yesu na uhusiano wa jinsia moja.

Filamu hiyo yenye utata ilioneshwa maalum siku ya krisimasi kupitia kampuni ya Netflix.

kipindi hiko cha filamu kimechezwa na kundi la waigizaji wa vichekesho Porta dos Fundos, inaonesha Yesu kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, katika moja ya onesho Yesu anaonekana akimleta mchumba wake wa kiume kumtambulisha kwa familia.

Unaweza pia kusoma:

Zaidi ya watu milioni 2.3 wamesaini waraka wa mtandao ili filamu hiyo iondolewe na isioneshwe kabisa kwenye televisheni.

Video inayosambaa mtandaoni inaonesha kundi la watetezi wa kidini wakifanya shambulio katika ofisi iliyotengenezewa fiamu hiyo.

Katika video hiyo kundi linalojiita wanaharakati wa kidini wameonekana wakivamia ofisi za uzalishaji wa filamu hiyo na kuanza kurusha mabomu.

Kiongozi wa kundi hilo alitoa hotuba mara baada ya shambulio na kusema kuwa filamu hiyo ni kinyume na maadili lakini pia alikosoa kampuni ya kuonesha filamu ya Netflix.

Video hiyo ilisambaa siku ya krisimasi na baada ya siku moja shambulio hilo likafanyika katika ofisi ya kundi la Porta dos Fundos ambapo ndipo ilipotengenezwa.

Hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa , walinzi walifanikiwa kuzima moto kwa haraka.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zaidi ya watu milioni 2 wameitaka Netflix kuondoa filamu hiyo

katika ujumbe wa twitter kundi hilo limesema kuwa watapambana katika kipindi hiki cha chuki na watafikisha upendo kupitia uhuru wa kujieleza.

Filamu yao fupi ya dakika 46 iliogizwa katika lugha ya kireno inayiotwa 'The First Temptation of Christ' imezua ghazabu kali na kukosolewa na makundi ya kidini tangu kuachiwa kwake mwezi huu wa disemba.

Unaweza pia kusoma:

kundi hili la waigizaji wa vichekesho wamewahi kushinda tuzo ya Emmy kwa filamu yao nyingine ya krisimasi.

Waumini wengi wa Kikatoliki duniani wapo Brazil na pia kundi kubwa sasa linakua la waevanjalisti wanaomuunga mkono rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro .

Mtoto wa rais Jair Bolsonaro ni miongoni mwa waliokosoa vikali filamu hiyo na pia Netflix ya nchini Brazil.

Kupitia mtandao wa Twitter, Juliano Medeiros, kiongozi wa upinzani amesema shambulio hilo ni la hatari hivyo mamlaka zinapaswa kuchukua hatua.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii