Mkusanyiko wa picha bora duniani mwaka 2019

Mkusanyiko wa picha za zilizozua hisia duniani mwaka 2019.

Mkulima awalisha kondoo wake kwa mabuu, Australia, mwezi Februari. Sehemu kubwa ya Mashariki mwa Australia ilikabiliwa na ukame mbaya kwa miezi kadhaa, kulemaza shughuli za kilimo na jamii kwa ujumla. Haki miliki ya picha Mark Evans / Getty Images
Image caption Mkulima aliwalisha kondoo wake kwa mabuu, Australia, mwezi Februari. Sehemu kubwa ya Mashariki mwa Australia ilikabiliwa na ukame mbaya kwa miezi kadhaa, kulemaza shughuli za kilimo na jamii kwa ujumla.
Waumini wamwaga bizari katika tukio la kutoa sadaka kwa kwa miungu wa Khandoba wakati washerehe ya Somvati Amavasya, katika hekalu moja mjini Jejuri, India, mwezi Februari 2019. Haki miliki ya picha Danish Siddiqui / reuters
Image caption Waumini wamwaga bizari katika tukio la kutoa sadaka kwa kwa miungu wa Khandoba wakati washerehe ya Somvati Amavasya, katika hekalu moja mjini Jejuri, India, mwezi Februari 2019.
Enia Joaquin Luis, 11, aamka kando ya dada yake wa miaka sita, wakiwa wamejifunika mfuko wa plastiki kujikinga na mvua ,katika makazi ya muda ya Buzi. Hii ni baada ya kimbunga Idai kupiga pwani ya Msumbiji mwezi Machi 14 na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa. Umoja wa Mataifa ulisema watu milioni 1.7 waliishi kwenye njia ya kimbunga hicho huku watu wengine 920,000 wakiathiriwa nchini Malawi na maelfu ya wengine nchini Zimbabwe. Haki miliki ya picha Yasuyoshi Chiba / AFP
Image caption Enia Joaquin Luis, 11, aamka kando ya dada yake wa miaka sita, wakiwa wamejifunika mfuko wa plastiki kujikinga na mvua ,katika makazi ya muda ya Buzi. Hii ni baada ya kimbunga Idai kupiga pwani ya Msumbiji mwezi Machi 14 na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa. Umoja wa Mataifa ulisema watu milioni 1.7 waliishi kwenye njia ya kimbunga hicho huku watu wengine 920,000 wakiathiriwa nchini Malawi na maelfu ya wengine nchini Zimbabwe.
Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, amkumbatia mwanamke katika msikiti wa Kilbirnie, mjini Wellington,kufuatia shambulio la Christ church. Watu 50 waliuawa mwezi Machi 15 baada ya mhalifu kushambulia misikiti miwili akionesha tukio hilo moja kwa moja katika mtandao wa Facebook. Haki miliki ya picha Hagen Hopkins / Getty Images
Image caption Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, amkumbatia mwanamke katika msikiti wa Kilbirnie,mjini Wellington,kufuatia shambulio la Christ church. Watu 50 waliuawa mwezi Machi 15 baada ya mhalifu kushambulia misikiti miwili akionesha tukio hilo moja kwa moja katika mtandao wa Facebook.
Familia ya Wakurdi zilisherehekea katika mji wa Nowruz, eneo lenye milima karibu na Iraq. Tamasha hilo la, mwezi Machi, linaadhimisha mwaka mpya wa Kiajemi na pia husherehekewa na jamii tofauti katika maeneo nya magharibi na kati ya bara Asia. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Familia ya Wakurdi zilisherehekea katika mji wa Nowruz, eneo lenye milima karibu na Iraq. Tamasha hilo la mwezi Machi, linaadhimisha mwaka mpya wa Kiajemi na pia husherehekewa na jamii tofauti katika maeneo nya magharibi na kati ya bara Asia.
Mwenyekiti wa zamani wa Nissan Carlos Ghosn akipelekwa katika jumba la kuzuia wafungwa la Tokyo mwezi Aprili baada ya kuachiliwa kwa dhamana katika kesi kadhaa za ufujaji wa fedha. Mawakili wa Ghosn wameikosoa serikali ya Japan kwa kumhujumu wakishirikiana na waendesha mashitaka na wasimamizi wakuu wa kampuni ya Nissan. Haki miliki ya picha Behrouz Mehri / AFP
Image caption Mwenyekiti wa zamani wa Nissan Carlos Ghosn, akipelekwa katika jumba la kuzuia wafungwa la Tokyo mwezi Aprili baada ya kuachiliwa kwa dhamana katika kesi kadhaa za ufujaji wa fedha. Mawakili wa Ghosn wameikosoa serikali ya Japan kwa kumhujumu wakishirikiana na waendesha mashitaka na wasimamizi wakuu wa kampuni ya Nissan.
Mnara wa kanisa kongwe la Ufaransa maarufu la Notre-Dame de Paris likianguka baada ya moto kuchoma jengo la kanisa hilo, Aprili 15. Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yaliteketezwa na moto huku mwingine ukifanikiwa kuzimwa katika minara miwili ya kengele. Rais Emmanuel Macron alitoa ahadi ya miaka mitano ya kufanyia ukarabati kanisa hilo. Haki miliki ya picha Geoffroy Van Der Hasselt / AFP
Image caption Mnara wa kanisa kongwe la Ufaransa maarufu la Notre-Dame de Paris likianguka baada ya moto kuchoma jengo la kanisa hilo, Aprili 15. Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yaliteketezwa na moto huku mwingine ukifanikiwa kuzimwa katika minara miwili ya kengele. Rais Emmanuel Macron alitoa ahadi ya miaka mitano ya kufanyia ukarabati kanisa hilo.
Majeneza yakibebwa wakati wa mazishi ya pamoja ya wahanga wa shambulio la kanisha la St Sebastian Aprili 23 mjini Negombo, Sri Lanka. Haki miliki ya picha Carl Court / Getty Images
Image caption Majeneza yakibebwa wakati wa mazishi ya pamoja ya wahanga wa shambulio la kanisha la St Sebastian Aprili 23 mjini Negombo, Sri Lanka. Msururu wa mashambuio ya mabomu yaliolenga makanisa na mahoteli ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 250 na wengine wengi kujeruhiwa. Walipuaji walifanya shambulio hilo Jumapili ya Pasaka katika miji ya Colombo, Negombo na Batticaloa.
Mwanafunzi Alaa Salah, 22, alipewa jina la ''The Nubian Queen'' baada ya video aliyokuwa akiongoza mkutano wa kupinga utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir kuvuma mitandaoni mwezi Aprili akimshinikiza ang'atuke madarakani. Haki miliki ya picha Courtesy Lana H Haroun
Image caption Mwanafunzi Alaa Salah, 22, alipewa jina la ''The Nubian Queen'' baada ya video aliyokuwa akiongoza mkutano wa kupinga utawala wa rais wa Sudan Omar al-Bashir kuvuma mitandaoni mwezi Aprili akimshinikiza ang'atuke madarakani.
Rais wa Marekani Donald Trump alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, katika mpaka wa kati ya Korea Kaskazini na Kusini Juni 30. Haki miliki ya picha Kevin Lamarque / Reuters
Image caption Rais wa Marekani Donald Trump alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, katika mpaka wa kati ya Korea Kaskazini na Kusini Juni 30. Viongozi hao walisalimiana huku bwana Kim akisema hakutarajia kukutana na rais katika eneo hilo. Bwana Trump kisha alivuka mpaka na kuingia Korea Kasakazini na kuwa rais wa kwanza wa Marekani kufanya hivyo.
Watu wakishiriki pigano la kila mwaka la tomato Haki miliki ya picha Diana Sanchez / AFP
Image caption Tamasha la kila mwaka laTomatina lilifanyika katika mji wa Sutamarchan, Colombia mwezi Juni. Katika tamasha hilo washiriki hupigana kwa tomato, kuadhimisha mwisho wa mavuno ya tomato.
Wanajeshi wakiwaangalia wenzao 280 wakishiriki zoezi la kushuka kwa parachuti katika uwanja wa Sannerville, France. Wakongwe, familia, wageni na wanajeshi walikusanyika Juni 6 kuadhimisha kumbukizi ya 75 ya Normandy landings, ambayo ilichangia vikosi vya muungano kuelekea Ujerumani na kushinda Ulaya miezi 11 baadae. Haki miliki ya picha Christopher Furlong / Getty Images
Image caption Wanajeshi wakiwaangalia wenzao 280 wakishiriki zoezi la kushuka kwa parachuti katika uwanja wa Sannerville, France. Wakongwe, familia, wageni na wanajeshi walikusanyika Juni 6 kuadhimisha kumbukizi ya 75 ya Normandy landings, ambayo ilichangia vikosi vya muungano kuelekea Ujerumani na kushinda Ulaya miezi 11 baadae.
Wabunge Rashida Tlaib, Ilhan Omar, Alexandria Ocasio-Cortez na Ayanna Pressley wazungumzia suala hilo katika mjini Washington, DC, USA. 15 Julai 2019. Haki miliki ya picha Jim Lo Scalzo / EPA
Image caption Bunge la wawakilishi nchini Marekani lilipiga kura kulaani kitendo cha rais Donald Trump, katika msururu wa ujumbe wa Twitter mwezi Julai, aliposema wabunge wanawake Rashida Tlaib, Ilhan Omar, Alexandria Ocasio-Cortez na Ayanna Pressley "wanatokea nchi ambazo serikali zao zimesambaratika" na kuwataka "warudi".
Wanaharakati wa mazingira wa Uswidi Greta Thunberg na Ivy-Fleur Boileau, Virgile Mouquet, Adelaide Charlier na Alicia Arquetoux, kutoka vugu vugu la mazingira la vijana, wakihudhuria kikao cha maswali wa serikali katika Bunge la kitaifa mjini Paris, mwezi Julai 2019. Haki miliki ya picha Philippe Wojazer / Reuters
Image caption Wanaharakati wa mazingira wa Uswidi Greta Thunberg na Ivy-Fleur Boileau, Virgile Mouquet, Adelaide Charlier na Alicia Arquetoux, kutoka vugu vugu la mazingira la vijana, wakihudhuria kikao cha maswali wa serikali katika Bunge la kitaifa mjini Paris, mwezi Julai. BI Thunberg baadae aliytangazwa na Jarida la Time kuwa kijana mdogo wa mwaka magazine.
Wanaharakati wa kupigania demokrasia wakijikinga dhidi ya maji ya mwasho kutoka kwa magari polisi wa kizima ghasia Hong Kong mwezi Septemba 15, 2019. Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanaharakati wa kupigania demokrasia wakijikinga dhidi ya maji ya mwasho kutoka kwa magari polisi wa kizima ghasia Hong Kong mwezi Septemba. Maandamano yalianza mwezi Juni kupinga mswada wa kuhamishwa kwa wahalifu kushtakiwa nje ya Hong Kong. Maandamano hayo yanatarajiwa kuendelea kwa zaidi ya miezi sita.
Rai wa Afghanistan wakisikiliza hotuba ya mwisho ya kampein ya mgombea urais Abdullah Abdullah mjini Bamiyan. Haki miliki ya picha Paula Bronstein / Getty Images
Image caption Rai wa Afghanistan wakisikiliza hotuba ya mwisho ya kampein ya mgombea urais Abdullah Abdullah mjini Bamiyan. Watu wachache waliripotiwa kupiga kura katika uchaguzi huo wa urais kwa sababu wapiga kura wengi walihofia usalama wao kufuatia vitisho kutoka kwa wanamgambo wa Taliban.
Nyumba iliyoharibiwa na kimbunga Dorian katika mji wa bandari wa Marsh eneo la Great Abaco, Bahamas, Septemba 8, 2019. Haki miliki ya picha LOREN ELLIOTT / Reuters
Image caption Nyumba iliyoharibiwa na kimbunga Dorian katika mji wa bandari wa Marsh eneo la Great Abaco, Bahamas. Kimbunga hicho kikali katika historia kiligonga Bahamas kiliacha uharibifu mkubwa. Watu karibu 43 walifariki na wengine wengi hawajulikani waliko mpaka sasa siku kadhaa baada ya kimbunga kutua mwezi Septemba.
Mtu aliyejificha nyuma ya sing'enge ahudhuria maandamano mjini Srinagar mwezi Oktobar, baada serikali ya India kufuta uhuru wa jimbo la Kashmir Haki miliki ya picha Danish Ismail / Reuters
Image caption Mtu aliyejificha nyuma ya sing'enge ahudhuria maandamano mjini Srinagar mwezi Oktoba, baada serikali ya India kufuta uhuru wa jimbo la Kashmir
Wazima moto wakikabiliana na moto mkali uliozuka mjini Santa Paula, California, mwezi Novemba. Haki miliki ya picha Josh Edelson / AFP
Image caption Wazima moto wakikabiliana na moto mkali uliozuka mjini Santa Paula, California, mwezi Novemba. Karibu hekari 100,000 ziliteketezwa na moto huo wa nyika ambao uliwalazimu maelfu ya watu kuhama makaazi yao.
Mwanamume kutoka jamii ya Uajajara - ambaye ni mwanachama wa ulinzi wa msitu, kundi lililobuniwa kukabiliana na ukataji miti katika eneo hilo Haki miliki ya picha Ueslei Marcelino / REUTERS
Image caption Mwanamume kutoka jamii ya Uajajara - ambaye ni mwanachama wa ulinzi wa msitu, kundi lililobuniwa kukabiliana na ukataji miti katika eneo hilo - akishika doria karibu na mji wa Amarante, jimbo la Maranhao. Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amekosolewa vikali ndani na nje ya nchi kwa kushindwa kutoa ulinzi kwa maeneo ya mashariki ya msitu wa Amazon.
Mwanamke afunika uso wake karibu na barabra ya kuelekea mji wa Ras al-Ain nchi Syria unaokaliwa na Wakuridi, katika mpaka wa nchi hiyo na Uturuki. Haki miliki ya picha Delil Souleiman/AFP
Image caption Mwanamke afunika uso wake karibu na barabra ya kuelekea mji wa Ras al-Ain nchi Syria unaokaliwa na Wakuridi, katika mpaka wa Uturuki. Nyuma yake, magurudumu ya gari yamewashwa moto ili kuzuia ndege za kivita za Uturuki kuonekana. Mwezi Oktoba, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alivamia kijeshi vikosi vya Kikurdi baada ya rais Donald Trump kutangaza kuondoa vikosi vya Marekani katika eneo la mpaka wa Syria.
Mtoto wa mwaka mmoja akiwa mbele ya Gateway International Bridge mjini Matamoros, Mexico Haki miliki ya picha Veronica G. Cardenas / Reuters
Image caption Mtoto wa mwaka mmoja raia wa Mexico akisubiri nafasi yake ya kuomba hifahi nchini Marekani akiwa na mama yake alionekana mbele ya lango la daraja la kimataifa la Gateway mjini Matamoros.

Picha zote zina haki miliki ya wapiga picha waliotajwa pamoja na mashirika