Sadio Mane: Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal atajwa kuwa mchezaji bora 2019

Sadio Mane Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sadio Mane alifunga magoli 15 kwa mwaka 2019-20 kwa timu ya Liverpool

Shirikisho la soka barani Afrika wamemtaja mwanasoka bora wa mwaka kuwa ni Sadio Mane ambaye anachezea timu ya Liverpool.

Walioshiriki kinyang'anyiro cha tuzo hizo ni mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool -na wenzie walioshiriki kinyang'anyiro hicho ni mchezaji wa Misri Mohamed Salah na mchezaji wa Manchester City pamoja na winga wa Algerian Riyad Mahrez.

Mane ambaye ana umbaye ana umri wa miaka 27, aliweza kuisaidia Reds katika ligi ya mwaka 2018-2019 na kufunga magoli 30 katika msimu uliopita.

Aliweza kufunga magoli 15 mpaka sasa kwa mwaka 2019 mpaka 2020, na kuisaidia Liverpool kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 13.

"Nina furaha sana na ninajivunia kuwa mshindi. Kandanda ni ajira yangu ambayo ninaipenda," alisema Mane.

"Ninapenda kuwashukuru familia yangu, taifa langu , timu yangu ya taifa , wachezaji wenzangu, shirikisho na klabu ya Liverpool.Hii ni siku kubwa kwangu."

Mane alichukua tuzo yake katika sherehe zilizofanyika huko Hurghada, Misri.

Lakini si Salah, ambaye alishinda tuzo hiyo mara mbili katika miaka miwili iliyopita wala Mahrez wali.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sadio Mane ameifungia Liverpool magoli 15 kwa mwaka 2019-20

Mane alimaliza katika nafasi tatu za juu katika tuzo hizo katika miaka mitatu iliyopita.

Na ilikuwa ni ndoto yake kushinda tuzo hiyo ili kufikia mafanikio ya shujaa wake El Hadji Diouf, ambaye alishinda mwaka 2002.

Premia ligi imewakilishwa vyema katika kikosi bora cha Afrika na tuzo nyingine

Mahrez alishinda tuzo moja - Goli bora la Afrika ambalo alilifunga kwenye mchezo wa nusu fainali Afcon kati ya Algeria na Nigeria .

Salah, Mane na Mahrez wote wameingia katika kikosi cha wachezaji 11 bora pamoja na beki wa kati wa Liverpool, Joel Matip na beki wa kulia wa Tottenham Serge Aurier na mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang.

Wachezaji bora 11 wa Afrika: Andre Onana (Ajax/Cameroon), Achraf Hakimi (Borussia Dortmund/Morocco), Kalidou Koulibaly (Napoli/Senegal), Joel Matip (Liverpool/Cameroon), Serge Aurier (Tottenham/Ivory Coast), Riyad Mahrez (Manchester City/Algeria), Idrissa Gana Gueye (Paris St-Germain/Senegal), Hakim Ziyech (Ajax/Morocco), Mohamed Salah (Liverpool/Egypt), Sadio Mane (Liverpool/Senegal), Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal/Gabon)

Beki wa kulia wa Morocco,Achraf Hakimi mwenye miaka 21,ambaye anachezea Borussia Dortmund kwa mkopo akitokea Real Madrid, ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.

Mshambuliaji wa Nigeria na Barcelona Asisat Oshoala ametajwa kuwa mchezaji bora kwa upande wa wanawake akiwapiku mshambuliaji wa Cameroon Ajara Nchout na nyota wa Beijing BG Phoenix na Afrika Kusini Thembi Kgatlana.

Cameroon, waliopoteza mbele ya England kwa 3-0 kwenye hatua 16 bora ya fainali za kombe kwa wanawake mwaka 2019 wameshinda tuzo ya kuwa timu bora ya taifa kwa upande wa wanawake.

Djamel Belmadi, aliyeiongoza Algeria kushinda ubingwa wa Afcon ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume, na kocha wa Afrika ya kusini Diseree Ellis, akishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii