Familia ya kifalme yajadili suala la mwanamfalme Harry na Meghan

Familia ya kifalme kuwa na kikao cha pamoja Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Familia ya kifalme kuwa na kikao cha pamoja

Mwanamfalme Harry na mwanamfalme William wamekanusa taarifa ya uongo iliyoandikwa katika gazeti la Uingereza kuhusu mahusiano yao.

Maelezo yaliyotolewa kwa niaba ya mwanamfalme Harry na William ameelezea taarifa hiyo kuwa ya kizushi na iliyotumia lugha ya kichochezi.

Taarifa hiyo imekuja baada ya chanzo cha taarifa kuliambia gazeti la Times kuwa mwanamfalme Harry alipata msukumo wa kuondoka katika shughuli za kifalme kutokana na tabia za unyanyasaji za William.

Ndugu hawa watakutana na malkia pamoja na wakuu wa familia kifalme huko Sandringham kujadili majukumu ya baadae ya mwanamfalme Harry na mkewe Meghan.

Mwanamfalme Harry, kaka yake mwanamfalme William na baba yao mwanamfalme Charles watahudhuria kikao hicho, huku Meghan anatarajiwa kujumuika kwa njia ya simu akiwa Canada.

Mwanamfalme Harry na mkewe wanapanga kujihudhuru na majukumuku ya kifalme.

Mwandishi wa masuala ya kifalme wa BBC, Jonny Dymond ameelezea mkutano huo kuwa ni mkutano wa kihistoria katika familia ya kifalme.

Kikao hicho kinaleta matumaini kuwa mazungumzo hayo yataweza kuwapa mwanya wapenzi hao wapya katika familia ya kifalme kupiga hatua na vilevile malkia kupata suluhu kuhusu suala lao.

Hata hivyo mwandishi wetu alisema kuwa majadiliano hayo yatachukua muda kufikia makubaliano na kuanza kufanyiwa kazi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Malkia akiwa anatoka kanisani siku ya jumapili

Miongoni mwa masuala ambayo yanatarajiwa kuzungumzwa ni namna mwanamfalme Harry na mkewe wataweza kupata ufadhili, na kama wataendelea kubaki na wadhifa wao wa kifalme au la.

Malkia ,mwanamfalme Charles, William na Harry wanatarajiwa kuhakiki majukumu yao ya kifalme na kupanga jinsi shughuli za kifalme zitaweza kuendelea bila uwepo wa mwanamfalme Harry na mkewe.

Leo hii itakuwa ni ya kwanza kwa malkia kufanya mazungumzo na mwanamfalme Harry na mkewe tangu watangazwe nia yao.

Mwanamfalmee Charles amerejea kutoka Oman ambapo alihudhuria mazishi ya sultani Qaboos.

Huwezi kusikiliza tena
Mwanamfalme Harry na Meghan warudi kutoka Canada

Magazeti yameripoti kupendekeza wapenzi hao kuweza kufanya mahojiano ya televisheni , kama watakuwa hawajafurahia matokeo ya majadiliano hayo.

Mtangazaji na rafiki wa wapenzi hao, Tom Bradby - aliyefanya makala kuhusu wao mwaka jana - aliandika katika gazeti la Sunday Times: "Nina wazo la nini kinachoweza kutangazwa kwa ujumla, sidhani kama kukaa kufanya majuano ni jambo zuri kwa sasa."

Huko Sandringham hapo baadae wataweza kuchagua namna nzuri.

Hii itazingatia na malengo ya mwanamfalme Harry na mkewe Meghan.

Ukiachilia mbali mkanganyiko huu, maelezo ya zaidi yanahitajika , ili kuweza kuweka usawa katika malengo yao ambayo yanaleta utofauti na kuonekana kuwa wanaomba jambo gumu.

Fedha ni suala kubwa.

Labda suala ili linaweza kuzungumziwa jumatatu, jumanne au jumatano.

Lakini majadiliano ya kupata huduma yanahitaji ufikiwa mapatano fulani.

Kama Mwanamfalme Harry na Meghan wataendelea kuwa katika shughuli za kifalme basi hakuna kitakachobadilika.

Lakini wapenzi hao watakubali vizuizi watakavyopewa ili wapate huduma?

Suala lao linaweza kukwepeshwa ingawa uelekeo unaweza kuwa wa njia moja. Mwanamfalme Harry na Meghan wanatafuta namna ya kujiondoa.

Harry na Meghan wanataka nini?

Katika maelezo yao kupitia mtandao wa Instagram, wapenzi hao walisema wanataka kuachana na shughuli za kifalme na kuwa huru kiuchumi.

Vilevile walisema wamepanga kugawa muda wao wa kuishi Uingereza na kaskazini Marekani, huku wakiendeea kumtumikia malkia.

Tumefikaje hapo?

Meghan akiwa Canada akiwa na mtoto wake wa miezi nane Archie walienda huku wakati majadiliano yakiendelea, ambapo watahusisha serikali ya Uingereza na Canada.

Yeye na mwanamfalme Harry walikuwa Canada wakati wa krismasi kabla ya kurejea Uingereza kwa ajili ya majukumu ya kifalme.

Mwezi oktoba, Mwanamfalme Harry na Meghan walibainisha jinsi wanavyokwazika na kufuatiliwa na vyombo vya habari.

Wapenzi hao walikuwa wanajiandaa kuanzisha asasi yao ya misaada baada ya kujitoa katika shughuli za kifalme.


Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii