Polisi wamekanusha kupiga risasi waandamanaji wenye ghadhabu

Huwezi kusikiliza tena
Waandamanaji wanaopinga serikali wakipaza sauti na kusema 'Kifo kwa dikteta' karibu na uwanja wa Azadi

Polisi nchini Iran katika mji mkuu Tehran, wamekanusha kutumia silaha dhidi ya waandamanaji walioghadhabishwa na kudunguliwa kwa ndege ya Ukraine.

Maafisa wa polisi walikuwa wamepata maagizo ya kuonyesha kwamba wao imara, mkuu wa polisi amesema.

Video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii Jumapili, zilirekodi kile kilichoonekana kama maafisa wakifyatua risasi pamoja na mwanamke aliyejeruhiwa akibebwa.

Maandamano yalianza Jumatatu baada ya Iran kukubali kwamba ilirusha kombora kimakosa dhidi ya ndege ya abiria ya Ukraine na kuanguka karibu na Tehran.

Watu wote 179 waliokuwa kwenye ndege hiyo PS752, wengi wao wakiwa raia wa Iran na Canada walikufa.

Siku tatu za kwanza baada ya kutokea kwa ajali, Iran ilikanusha kwamba vikosi vyake vimedungua ndege hiyo na kusema kwamba ilipata matatizo ya kiufundi.

Hata hivyo, ilikubali kudungua ndege hiyo baada ya video kuonyesha kombora likipiga ndege hiyo, na kusababisha hasira kote nchini Iran.

Unaweza kusoma:

Awali, raia wa Iran walikuwa wameungana kuomboleza kifo cha Jenerali Qasem Soleimani, ambaye alikuwa wa pili mwenye madaraka makubwa nchini humo, baada ya kushambuliwa na ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani nchini Iraq.

Taarifa za hivi karibuni zinaonesha uwezekano wa kutokea kwa maandamano zaidi sawa na yaliyoshuhudiwa Novemba mwaka jana dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta. Makundi ya haki za binadamu yanasema mamia ya watu waliuawa.

Nini kilitokea katika maandamano ya wikiendi?

Maandamano yaliyotokea Jumapili yaliendelea hadi usiku wa manane huku watu wakiendelea kupandwa na ghadhabu dhidi ya serikali ya Iran na vikosi vya ulinzi vilivyodungua ndege ya Ukraine.

Video iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii inaonesha waandamanji wakiipiga mateke na kuangusha bango kubwa la Soleimani.

Kuna taarifa kwamba watu kadhaa walijeruhiwa wakati vikosi vya usalama vilipoingilia maandamano yaliyofanyika kwenye uwanja wa Azadi mjini Tehran ambapo watuwalikuwa wakipaza sauti na kusema "kifo kwa dikteta" - wakiashiria kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei.

Video moja iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha jeshi la Basij Resistance, ambalo mara nyingi hutumiwa kukabiliana na ghasia likivamia waandamanaji, Kile kinachokisiwa kuwa milio ya risasi inasikika.

Video nyengine inamuonesha mwanamke alijeruhiwa akibebwa na watu waliokuwa wakisema kwa sauti ya juu kuwa amepigwa risasi ya mguu. Damu imeonekana ikitapakaa ardhini.

Mtu aliyekuwa kiandamana ameiambia BBC kwamba: "Walianza kuja na fimbo, wakaanza kutupiga. Tulianza kupiga kelele tukisema maneno ya kupinga serikali na wao wakaanza kurushia risasi."

Hata hivyo licha ya madai yote hayo, mkuu wa polisi Jenerali Hossein Rahimi amekanusha kwamba maafisa wao walitumia silaha kukabiliana na waandamanaji.

"Polisi walikabiliana na waandamanaji waliokuwa wamekusanyika kwa utulivu," amesema, kabla ya kutoa onyo kwamba wale wenye nia ya kusema maneno ya uongo, watakabiliwa.

Wakati huohuo, msemaji wa serikali ya Iran Ali Rabiei alitupilia alikejeli kile alichokiita machozi ya mamba wakati anazungumzia hatua ya Rais Trump ya kuunga mkono waandamanji.

Maandamano yalianza tena Jumatatu mchana nje ya vyuo vikuu vya Tehran na mji wa Isfahan.

Ndege iliyoanguka ya PS752?

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Vadym Prystaiko, ameiambia BBC kuwa rais wa Iran Hassan Rouhani alikuwa ameiahidi serikali ya Ukraine kwamba kila aliyehusika atakabiliwa na mkono wa sheria katika mazungumzo kwa njia ya simu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bango lililopo mji wa Tehran lililoandikwa: "Sote tuna machungu na tunaomboleza."

Bwana Prystaiko aliongeza kuwa nchi 5 ambazo raia wake walikuwa kwenye ndege hiyo - Ukraine, Canada, Sweden, Ujerumani na Uingereza - zitakutana London Alhamisi hii kujadiliana kuhusu hatua ya kisheria itakayochukuliwa.

Alisema, nchi zinazoomboleza, zitashirikiana kama nchi binafsi na kwa pamoja kuhakikisha wote waliohusika na ajali hiyo wanachukuliwa hatua za kisheria na vile familia za walioathirika zinaweza kufidiwa.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau pia ameambia watu waliokusanyika katika ibada maalum ya raia 57 wa Canada kwamba nchi hiyo itahakikisha haki imetenda.

Hata hivyo serikali ya Iran imekanusha madai kuwa imekuwa ikijaribu kuficha ukweli.

Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria zaidi ya 170 ilianguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Ndege namba PS752 hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Awali, ubalozi wa Tehran ulisema kuwa injini ya ndege iliharibika na hakuna uhusiano wowote wa kigaidi na pia ilisema kuwa haitakabidhi kisanduku cha kunakili safari ya ndege ama ''Black box'' ya ndege ya Ukraine iliyopata ajali na kuua watu 176, kwa kiwanda kilichotengeneza ndege hiyo au kwa Marekani.

Ajali hiyo imetokea wakati ambapo kuna mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran, muda mfupi baada ya Iran kushambulia kwa makombora kambi mbili za kijeshi za Marekani zilizopo Iraq.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii