Wanawake wachukua nafasi muhimu katika Baraza jipya la Mawaziri

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya aUhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri. Katika hotuba yake ya kwanza katika mwaka wa 2020 aliyoitoa kwenye Ikulu ya Rais Mombasa.

Katika mabadiliko hayo, wanawake wameonekana kuchukua nafasi muhimu ambapo Monica Juma ambaye awalikuwa waziri wa mambo ya nje amechukua wadhifa wa waziri wa ulinzi huku Raychelle Omamo aliyekuwa waziri wa ulinzi akiwa waziri wa mambo ya nje.

Ukur Yatani amedumisha wadhifa wake wa waziri wa fedha, Mutahi Kagwe ambaye aliwahi kuhudumu katika serikali ya Kenyatta amerejeshwa tena kama waziri wa Afya.

Betty Maina ambaye ametoka sekta ya biashara ameteuliwa kuwa waziri wa viwanda na Sicily Kariuki aliyekuwa waziri wa afya akiwa waziri wa maji.

Esther Koimett waziri wa habari na mawasiliano naye Simon Chelugui ni waziri wa Leba.

Peter Munya ndio Waziri wa kilimo huku Mwangi Kiunjuri akipigwa kalamu na wengineo.

Wakati wa hotuba yake Rais amesema kwamba wanaweka mipango ya kukwamua uchumi na kuweka wazi kuwa asilimia 70 ya madeni yamelipwa.

Huwezi kusikiliza tena
Maisha Pokot Magharibi baada ya maporomoko ya udongo

Pia ameweka kipau mbele katika biashara na kusema kuwa juhudi zinafanywa kusaidia biashara ndogo ndogo. Pia ametaka nchi kutoa umuhimu kwa uchumi badala ya siasa.

Aidha, rais amesema kwamba anaamini hakuka utawala ambao umekabiliana na ufisadi kama alivyofanyika kwenye utawala wake.

''Kuanzia mawaziri mpaka magavana, maafisa wakuserikali, maafisa wa ununuzi, nimekuwa mstari wa mbele. Rais Uhuru ameonyesha imani kuwa ufisadi umeogopesha wezi wa mali ya umma na kuacha mpira kwa mfumo wa mahakama akiitaka iwajibike kuhakikisha kuwa nchi inashinda vita dhidi ya ufisadi.

Miongoni mwa aliyoyazungumzia ni utoaji wa fedha za ujenzi wa viwanda viwili vya maziwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii