Mpango wa nyuklia wa Iran: Viongozi wa Ulaya waanzisha mchakato wa kujiondoa

nuklia Haki miliki ya picha AFP

Viongozi wa Ulaya wameanzisha mchakato wa kuingiza kwenye mzozo mpango wa nyukilia wa Iran, baada ya nchi hiyo kulegeza msimamo wake kuhusu mpango huo.

Iran ilijiondoa katika masharti yaliyofikiwa katika mkataba huo yanayodhibiti viwango vya uzalishaji madini ya urani, ambayo inaweza kutumiwa kuunda silaha za nyuklia.

Inasema ilifanya hivyo kujibu vikwazo vipya ya Marekani dhidi yake ilipojiondoa katika mkataba wa nyukli mwaka 2018.

Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimesema hazijaridhishwa na hoja ya Iran.

Mkataba wa nyuklia ulifanya Iran, ambayo inasisistiza mpango wake wa nyuklia ni salama, kukubali kupunguza viwango vya urutubishaji wa madini yake ya urani na kukubali wachunguzi kufuatilia mipango hiyo ili kulegezewa vikwazo vya kiuchumi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Awali iliafikiwa kuwa madini ya uranium ya Iran yatapunguzwa kwa 98% hadi kilo 300 baada ya miaka 15

Rais wa Marekani Donald Trump aliiwekea upya vikwazo hivyo ili kuishurutisha Iran kujadili makubaliano mapya katika juhudi za kudhibiti mpango wake wa nyuklia na hali kadhalika uundaji wa makombora ya masafa ya mbali. Katua ambayo bado haijakubaliana nayo.

Kwanini viongozi wa Ulaya wanachukua hatua sasa?

Washirika wengine katika mkataba huo- ambao ni Ufaransa, Ujerumani na Uingereza pamoja na China Urusi- walijaribu kudumisha mkataba huo.

Lakini vikwazo hivyo vimefanya biashara ya uuzaji nje wa mafuta ya Iran kuporomoka na kudorora kwa thamani ya sarafu yake hali ambayo imeongeza mfumko wa bei.

Katika taarifa ya pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza walielezea kusikitishwa kwao na hatua ya Marekani kujiondoa katika mkataba huo na kusisitiza kuwa walitaka kudumisha makubaliano hayo.

Mawaziri hao kutoka mataifa ya Ulaya-yanayofahamika kama E3 -yalifanya juhudi za kuhakikisha Iran inazingatia mkataba huo kupitia njia za kidiplomasia ili kukomesha mzozo kati ya nchi hiyo na Marekani kwa kuwaleata pamoja katika meza ya mazungumzo.

Iran kukiuka mashariti

"Mataifa ya E3 yamejitolea katika mchakato huuu wa kidiplomasia na yako tayari kundelea na mchakato huo hali ikiruhusu," iliongeza taarifa hiyo.

"Hata hivyo Iran imeendelea kukiuka mashariti yaliyofikiwa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia, JCPoA. Hatua ya Iran kuhusu masuala ya nyuklia imekuwa na athari mbaya."

"Hatukubaliani na hoja kuwa Iran inaweza kupunguza utekelezaji wa mashariti katika mkataba wa JCPoA."

Walisema hatua ya Iran ya Januari 5 ya kujiondoa katika masharti yanayodhibiti viwango vya urutubishaji wa madini ya urani - iliwafanya kusalia na hatua kutangaza mzozo kwa mujibu wa kanuni za mkataba uliopo ikiwa ni pamoja na mchakato wa kukabiliana na mzozo.

"Tunafanya hivi kwa nia njema ya kufikia lengo la kudumisha mkataba wa pamoja wa kimatifa wa nyuklia JCPoA na matumaini ya kupata ufumbuzi wa mzozo huu kubitia majadiliano ya kidiplomasia kwa kuzingatia kanuni zilizopo ndani ya mkataba wenyewe."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii