Fahamu hasara ya mgogoro wa Marekani na China uliodumu kwa miaka karibu miwili

A Chinese factory worker examines products at the production line. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mfanyakazi wa kampuni ya China akitathmini uzalishaji

Kumekuwa na majibizano makali, majadiliano ambayo hayakupata ufumbuzi na ahadi za tena na tena za kusitisha mapigano lakini hatimaye Marekani na China zinatia saini makubalino ya kibiashara Januari 15.

Licha ya matokeo, vita vya kibiashara vimekuwa na mchango mkubwa wa kufikiria tena kuhusu uhusiano wa China na Marekani, pamoja na uchumi wa dunia.

Kwa hiyo nini kilichobadilika katika kipindi cha miaka miwili ya mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili?

Nakisi ya kibiashara imepungua

Rais Donald Trump anatumia nakisi ya kibiashara kutathimini mafanikio na inaaminika kwamba kuendeleza mzozo wa kodi kunaweza kupunguza nakisi ya kibiashara ya nchi hiyo na China.

Ndio, nakisi ya kibiashara ya Marekani kwa bidhaa imepungua tangu kuanza kwa vita vya kibiashara lakini iko juu.

Katika kipindi cha miezi 12 hadi Novemba, 2019, nakisi ilipungua kwa bilioni 60 za marekani ikilinganishwa na mwaka uliotangulia na kusalia kuwa karibu bilioni 360 za marekani.

Lakini kupunguza nakisi huko kulikuwa na gharama yake - biashara kati ya nchi hizo mbili ilipungua kwa zaidi ya bilioni 100 za marekani.

Mauzo ya mazao ya Marekani yamepungua

China ilijibu hatua ya Trump kuongeza kodi kwa bidhaa zake zinazouzwa China na wakulima wa Marekani ndio walioathirika zaidi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mazao ya kilimo ya Marekani yanayouzwa China, kama maharagwe ya soya yamepungua kwa kiasi kikubwa kwasababu ya vita vya kibiashara

Mazuo ya kilimo ya Marekani nje ya nchi ya kila mwaka kwa China yalipungua kwa karibia bilioni 25 hadi bilioni 7, ikiwa ni kiwango cha chini zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Lakini kuna uwezekano mdogo wa hatua ya kuongeza kodi mazao ya kilimo ya China kuwa na athari kubwa katika uchumi wa Marekani, kwasababu wakulima wa Marekani ni karibia asilimia 1 pekee ya idadi ya watu nchini humo na Marekani imetoa ruzuku ya kiasi cha juu tu kwa kilimo ili kukabiliana na athari zinazotarajiwa.

Uwekezaji wa China ulishuka

Japo uwekezaji wa Marekani nchini China bado umesalia imara wakati wa vita vya kibiashara, uwekezaji wa China nchini Marekani umepungua kwa kiasi kikubwa.

Kulingana na jopo la washauri la American Enterprise Institute lenye makao yake Washington, uwekezaji wa China ulipungua kutoka bilioni 54 za marekani mwaka 2016 hadi bilioni 9.7 in 2018.

Katika kipindi cha nusu mwaka ya kwanza 2019, bilioni 2.5 pekee ndizo zilizowekezwa nchini Marekani na kampuni za China.

Kampuni za China zilisita kuwekeza nchini Marekani kwa madai ya wasiwasi kuhusiana na mzozo wa kibiashara pamoja na masharti makali ya uwekezaji na Marekani na uthibiti wa mtaji nchini China.

Mazingira ya kibiashara yenye kutia hofu

Japo bado uwekezaji unaendelea, kampuni za Marekani zenye kuendesha shughuli zake China zinasema kuwa mzozo wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili ni moja kile kinachowapa wasiwasi mkubwa.

Kulingana na Baraza la Kibiashara la Marekani na China, 2019, asilimia 81 ya kampuni za Marekani zenye kuendesha shughuli zake China, zilisema kuwa vita vya kibiashara vilikuwa na athari hasi katika biashara zao ambayo ni ongezeko la asilimia 8 ikilinganishwa na 2018.

Mwaka 2017, asilimia 45 ya kampuni za Marekani zilikuwa na wasiwasi wa suala hilo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uchumi wa China unakua polepole

Pigo kubwa kwa uchumi wa China na Marekani

Marekani inatarajiwa kutofikia matarajio yake ya kiuchumi kwa asilimia 3, kwasababu ya vita vya kibiashara na China. Wachambuzi wanasema inaweza kuchukua miaka miaka kadhaa kushuhudia athari kamili ya mvutano wa kodi kati ya Marekani na China.

Aidha, uchumi wa China unakua kwa mwendo wa polepole. Benki ya Dunia inakadiria kwamba uchumi wa China utakua chini ya asilimia 6 mwaka 2020, na kuwa kasi ya chini zaidi katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Vita vya kibiashara kati ya nchi hizo zenye uchumi mkubwa duniani bila shaka unaathiri uchumi wa dunia. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani Kristalina Georgieva amesema, "Katika vita vya kibiashara, kila mmoja hupata hasara."

Kando na kufanya mazungumzo ya kibiashara na China, Marekani pia inajadiliana na washirika wengine wa kibiashara kupitia tena makubaliano yao ya kibiashara. Kwasababu ya mgogoro wa kibiashara uliotokea, Shirika la Fedha Duniani lilipunguza makadiro ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka 2019 hadi asimilia 3, ikiwa ni makadiria ya chini zaidi tangu wakati wa mgogoro wa kifedha.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii