Misri, Ethiopia, Sudan zakubaliana matumizi ya mto Nile

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Makubaliano ya awali hayazungumzii kasi ya kujaza maji katika bawa

Misri, Ethiopia na Sudan wamefikia makuabliano ya awali ya kujaza maji na shughuli nyengine kwenye bawa kubwa linalojengwa mto Nile

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi tatu, pamoja na Marekani na Benki ya Dunia, imesema kwamba washiriki wanaojadiliana wamekubaliana kujaza bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia wakati wa msimu mvua kati ya miezi ya Julai na Agosti.

Hata hivyo taarifa hiyo haikusema lolote kuhusu masuala ya msingi yanayozunguka mgogoro huo ambayo ni kasi ya kujaza bwawa hilo.

Ethiopia inataka kujaza bawa la Grand Renaissance kwa miaka 6 lakini Misri imependekeza angalau mradi huo uchukue kipindi cha miaka 10 - kwa kuhofia kwamba kuchukua kipindi kifupi kutaathiri mtiririko wa maji ya mto Nile ambayo inategemea asilimia 90 ya maji ya mto huo.

Makubaliano ya mwisho yatatiwa saini Januari 28-29, wakati ambapo mawaziri kutoka nchi tatu watakuwa wanakutana Washington.

Haki miliki ya picha Reuters

Makubaliano ya awali ambayo yalifikiwa na waziri wa fedha wa Marekani na Rais wa benki ya Dunia, yanatilia maanani mahitaji ya Ethiopia ya kuanza uzalishaji wa umeme mapema, lakini pia yanazungumzia hatua za kupunguza athari kwa Misri na Sudan iwapo kutakuwa na vipindi virefu vya kiangazi katika nchi hizo zilizopo kwenye mkondo wa maji ya mto Nile.

Kufikiwa kwa makubaliano hayo kunapunguza wasiwasi uliokuwepo kati ya Ethiopia na Misri ambazo zimekuwa zikizozana tangu Ethiopia ilipoanza kujenga bawa hilo mwaka 2011.

Ujenzi wa Bwawa la Grand Renaissance linalojengwa Ethiopia ukishamalizika, mradi huo unaogharimu kima cha bilioni 5 za marekani, litakuwa ndio bawa kubwa zaidi la uzalishaji umeme barani Afrika lenye uwezo wa 6,000MW.

Pia unaweza kusoma:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii