Je, Rais wa Urusi Vladimir Putin anapanga 'mchezo' gani wa kisiasa?

Russian President Vladimir Putin (R, back to camera) and Russian Prime Minister Dmitry Medvedev (L, back to camera) leave after a meeting with Cabinet members at Government headquarters in Moscow, Russia, 15 January 2020 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Medvedev (kushoto) amekuwa mshirika wa karibu wa rais lakini kwa sasa atasalia nyuma ya pazia

Bila shaka ni jambo ambalo limeshtua wengi. Hata mawaziri katika serikali ya Urusi hawakuona uwezekano wa wao kujiuzulu serikalini.

Je lilikuwa suala la mwaka mpya wa kazi - kuachana na wazama na kujumuisha wapya?

Hungeweza kubisha kwamba Vladimir Putin, 67, amebadili mawazo yake. Akiwa amesalia na miaka minne kabla ya kuondoka madarakani, wakati tayari amekuwa katika kiti cha urais kwa miaka 20, ilijitokeza wazi kwamba anapanga ya baadaye.

Serikai mpya inayoongozwa na Mikhail Mishustin, mwenye ujuzi na aliyefanikiwa kubadilisha mfumo wa kodi wa Urusi uliokuwa unachukiwa na wengi na kuwa wenye kupendwa mno pamoja na aliyefanyakazi kwa ushikrikiano wa karibu na Bwana Putin tangu alipokuwa rais.

Dmitry Medvedev aliwahi hata kuwa rais kwa miaka minne, kwasababu kulingana na katiba ya Urusi haingewezekana kwa Putin kuendelea.

Bwana Medvedev, kiongozi wa chama tawala cha Urusi asiye na ushawishi mkubwa, bado yupo lakini majukumu yake mapya kama naibu wa baraza la usalama la Urusi huwa hayaangaziwi sana na umma.

"Kwake ni kama kupata dhahabu. Hii inamaanisha kwamba kuwekwa katika baraza la usalama ni sawa na kuwa mtu wa karibu na Putin - serikali yake ndogo," amesema Alexander Baunov kutoka jopo la ushauri wa sera za ndani na nje ya nchi.

Bwana Putin anafikia pale alipokuwa baada ya kipindi chake cha pili madarakani, wakati ambapo Dmitry Medvedev alikuwa makamu wake. Lakini wakati huu, rais hatakuwa kimya tu akiangalia kama waziri mkuu. Kwa sasa inaonekana kana kwamba muhula wa nne wa Putin madarakani kama rais utakuwa wa mwisho.

Kwa hiyo nini anachotaka?

Kwa nje, inamaanisha kwamba bunge litakuwa na nguvu zaidi - kuchagua waziri mkuu na kuidhinisha baraza la mawaziri. Lakini hilo halitatokea sasa. Bwana Putin amemchagua mrithi wa Medvedev na bunge litahitajika kumuidhinisha.

Kwa suala la bunge kuwa na nguvu zaidi, hilo bado halijajitokeza wazi. "Wabunge watakuwa walewale, siyo mengi yatakayobadilika," amesema Sergei Goryashko wa BBC Urusi.

Wakati Rais Putin anapendekeza kuwa na kura maoni katika mabadiliko ya katiba - kura ya kwanza ya aina hiyo tangu mwaka 1993.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia walihisi mabadiliko wakati Putin anatoa hotuba yake kwa mabunge yote mawili Jumatano asubuhi

Moja ya pendekezo linalopendwa na wengi ni kubadilisha Baraza la Taifa kuwa shirika rasmi la serikali litakalojumuishwa kwenye katiba.

Kwa wakati huu ni bodi ya ushuri yenye kujuisha magavana 85 wa eneo na maafisa wengine wakiwemo viongozi wa kidini. Bodi hiyo ni kubwa kiasi kwamba siku ya kufanya mikutano inabidi wakutane kwenye jumba la serikali lililopo Kremlin.

Bwana Putin ameweka hatma ya Baraza hilo wazi. Moja ni kwamba anaweza kuwa kiongozi mpya mwenye nguvu wa Baraza la Taifa.

"Ukweli wa kwamba ameanza mazungumzo kuhusiana na Baraza hilo la Taifa na huenda anajaribu kuunda nyadhifa nyengine itakayokuwa na nguvu zaidi, ambapo anaweza kuwa juu ya wadhifa wa rais," Bwana Baunov amesema.

Bwana Putin anataka kusalia madarakani lakini swali ni je hilo linawezana vipi? amesema Sergei Goryashko. Kwa wakati huu tunakaribia kuwa na uhakika wa kwamba Putin hataendelea kuwa rais baada ya 2024, lakini majukumu atakayochukua baada ya hapo. Huenda hata ikawa jukumu alilonalo sasa hivi la kiongozi wa baraza la taifa.

Sam Greene, Mkuu wa Taasisi ya Urusi iliyopo King's College London, anaamini kwamba viongozi wanaotafakari hatma yao baada ya 2024, kwa sasa watahitajika kucheza karata zao vizuri zaidi - ukiangazia majukumu ya bunge, Baraza la Taifa na Putin mwenyewe.

Kwa kutumia ulinganifu sawa na huo, mchambuzi Konstantin Eggert amesema kile kilichoundwa kuigiza mabadiliko ndiyo kile kile kilichokuwepo awali.

Watu wamepokeaje hatua hii?

Kwa Alexei Navalny, mpinzani ambaye ndo tishio kubwa kwa Putin, mabadiliko ya sasa ni mwanzo wa kurejea kwa siasa za mfumo wa kisovieti na kura yoyote ya kupendekeza mabadiliko kwenye katiba itakuwa ulaghai.

Mwanaharakati Lyubov Sobol pia alikuwa anashtumu: "Kubadilisha wezi na wezi wengine hakuwezi kuwa mabadiliko wala mageuzi."

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mikhail Mishustin amepongezwa kwa kubadilisha mfumo wa kodi lakini hafahamiki sana na raia wengi wa Urusi

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii