Kenya yanasa mali ya mamililioni ya dola kutokana na kesi za rushwa
Huwezi kusikiliza tena

Lakini kwanini hakuna aliyehukumiwa

Mkurugenzi mkuu wa mashitaka ya umma chini Kenya, Noordin Haji amesema kuwa serikali ya nchi hiyo imekusanya mali zenye thamani ya dola milioni 20 zilizokua zimekusanywa kutoka katika kesi mbalimbali za rushwa.

Hata hivyo hiyo ni asilimia moja tu ya pesa za umma zinazokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni mbili zikihusisha kesi za watu mashuhuri.

Katika miaka ya hivi karibuni wanasiasa wenye vyeo vya juu na watumishi wa umma wamekamatwa na kushitakiwa kwa rushwa.

Lakini kwanini hakuna aliyehukumiwa? Ni swali ambalo mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi amemuuliza Bw. Noordin Haji.

Mada zinazohusiana