Tiba ya saratani: Je ni nini haswa kilichogunduliwa?

Seli za saratani ya matiti Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Mbinu hiyo mpya inaweza kuuwa idadi kubwa ya seli za saratani, ikiwemo ile ya matiti na ile ya tezi dume

Ugunduzi wa mfumo mpya wa kinga unaweza kutumika kutibu aina zote za saratani, wanasema wanasayansi.

Kundi hilo kutoka chuo kikuu cha Cardiff liligundua mtindo wa kutibu saratani ya tezi dume, ile ya matiti ya mapafu na aina nyengine za saratani katika vipimo vya maabara.

Matokeo yake yaliochapishwa katika jaradi la kinga asli ,hayajajaribiwa miongoni mwa wagonjwa lakini wanasayansi hao wanasema yana uwezo mkubwa.

Wataalam wanasema kwamba ijapokuwa kazi hiyo ilikuwa hatua za kwanza ilikuwa inafurahisha.

Ni nini walichogundua?

Mfumo wetu wa kinga ni jinsi mwili wetu unavyoweza kujilinda dhidi ya maambukizi lakini pia unashambulia seli zilizo na saratani.

Wanasayansi hao walikuwa wakitafuta njia ambazo hazijagunduliwa kuhusu jinsi mfumo wetu wa kinga unavyoshambulia uvimbe unaosababisha saratani.

Kile walichogundua ni seli aina T ndani ya damu. Hii ni seli katika kinga ambayo inaweza kupima iwapo kuna tishio mwilini ambalo linafaa kuondolewa.

Tofauti yake ni kwamba seli hiyo inaweza kushambulia aina tofauti za saratani.

Kuna fursa hapa ya kutibu kila mgonjwa, mtafiti profesa Andrew Sewell aliambia BBC.

Aliongozea: Awali hakuna aliyeamini kwamba hili linaweza kufanyika. Inatoa fursa ya tiba moja kutibu saratani zote, seli moja aina ya T inayoweza kuharibu aina tofauti ya saratani miongoni mwa waathiriwa.

Je inafanya kazi vipi?

Seli aina ya T zina uwezo wa kubaini kiwango cha kemikali mwilini.

Kundi hilo la Cardif liligundua seli aina ya T na receptor yake ambayo inaweza kugundua na kuuwa idadi kubwa ya seli za saratani katika maabara ikiwemo katika mapafu, ngozi, damu, koloni, matiti, tezi dume, mayai na shingo ya uzazi.

Kitu muhimu ni kwamba iliwacha tishu muhimu bila kuathiriwa.

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption T-cells hushambulia seli za saratani

Jinsi seli hiyo inavyoweza kufanya kazi hiyo ndio swala ambalo bado linakanganya.

Seli hiyo inashirikiana na molekuli kwa jina MR1, ambayo ipo katika sakafu ya kila seli ndani ya mwili wa binadamu.

Imedaiwa kwamba MR1 uharibu metaboli inayoendelea ndani ya seli ya saratani katika mfumo wa kinga.

''Sisi ndio watu wa kwanza kuelezea seli aina ya T ambayo hugundua MR1 katika seli zilizo na saratani- hilo halijawahi kufanyika - hii ni mara ya kwanza'' , mtafiti Garry Dolton aliambia BBC.

Kwanini ni muhimu?

Tiba ya saratani ya seli ya T tayari ipo na hatua ya chanjo ya saratani yamekuwa moja ya ugunduzi wa kufurahisha zaidi katika ugonjwa wa saratani.

Mfano maarufu ni ule wa CAR-T - dawa ya jeni ilioundwa kushinikiza seli ya T kushambulia ama kuharibu seli za saratani mwilini

CAR-T inaweza kuwa na matokeo ya kushangaza ambayo huwafanya baadhi ya wagonjwa kuwa wagonjwa zaidi na kusalimu amri.

Hatahivyo mtazamo huo ni wa aina yake na unafanya kazi katika aina chache za saratani ambapo lengo kuu ni kuzifunza kutafuta seli za saratani.

Na imeshindwa kuwa na mafanikio yoyote katika saratani kama vile zile zinazosababisha uvimbe badala ya zile za damu kama vile saratani ya damu.

Watafiti wanasema kwamba seli aina ya T inaweza kusababisha tiba ya saratani duniani.

Je itafanya kazi vipi iwapo itaanza kutumiwa?

Lengo ni kwamba sampuli za damu zitachukuliwa kutoka kwa mgonjwa anayeugua saratani. Seli zake aina ya T zitatolewa na baadaye kuwekwa jeni ili kuzifanya kuweza kubaini seli za saratani.

Seli hizo zitakuzwa ili kuongezeka kwa wingi katika maabara na baadaye kurudishwa katika mwili wa mwanadamu .

Ni mbinu kama hiyo inayotumiwa kutengeneza tiba ya CAR T.

Hatahivyo utafiti huo umefanyiwa majaribio katika wanyama pekee na katika seli za maabara, na vipimo salama vitahitajika kufanywa kabla ya matumizi ya mwanadamu.

Je wataalam wanasemaje?

Lucia Mori na Gennaro De Libero, kutoka chuo kikuu cha Basel nchini Switzerland, wanasema kwamba utafiti huo una fursa kubwa lakini ni mapema mno kusema kwamba utafanikiwa kufanyakazi katika saratani zote.

''Tunafurahi sana kuhusu kazi ya seli hiyo ya kinga na matumizi ya TCRs katika tiba ya uvimbe'' ,alisema.

Daniel Davis, ambaye ni profesa wa kinga katika chuo kikuu cha Manchester, alisema: Huu ni utafiti wa msingi na hauko karibu kupata tiba ya saratani.

''Ni wazi kwamba ni ugunduzi mzuri, utakaoendeleza maarifa yetu ya kimsingi kuhusu mfumo wa kinga na uwezekano wa dawa mpya za baadaye."

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii