China yathibitisha virusi vya Corona vinaweza kusambazwa
China yathibitisha virusi vya Corona vinaweza kusambazwa
Virusi vipya vya Corona vimesambaa kutoka mji wa Wuhan nchini Uchina hadi sehemu zingine, pamoja na Marekani, Japan, Taiwan, Thailand na Korea Kusini.
Mamlaka imehamasisha watu wasisafiri nje na ndani ya mji wa Wuhan wakati ambapo idadi ya waliokufa imezidi 6. Imethibitishwa kwamba virusi hivyo vinaweza kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine na maafisa wanaonya kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi wakati wa sherehe za mwaka mpya wa China ambapo huenda ukasambaa zaidi na kuwa changamoto kuuzuia na kuudhibiti.
Corona: Maafisa wameonya 'huenda vikazaana na kusambaa mbali zaidi'
Mamlaka ya afya imethibitisha kuwa maambukizi ya virusi hivyo ni kupitia kwa binadamu.