Nzige huenda wakasababisha ukosefu wa chakula na utapia mlo

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kwa siku moja tu, kundi la nzige Paris huenda likala kiwango cha chakula kinachoweza kuliwa na nusu idadi ya watu wote Ufaransa

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa usaidizi wa kimataifa kukabiliana na nzige wengi waliovamia maeneo ya Afrika mashariki.

Msemaji wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO), ametoa wito wa kutolewa kwa msaada ili kukabiliana na athari za nzige kama vile ukosefu wa chakula, utapiamlo na kuathirika kwa mfumo wa maisha ya kila siku.

Ethiopia, Kenya na Somalia zinapitia wakati mumu kukabiliana na na makundi ya nzige ambako hakujawahi kutokea hapo kabla kunakoathiri mazao ya kilimo, limesema shirika la FAO.

Shirika hilo linahofia kwamba idadi ya nzige hao huenda ikaongezeka mara 500 zaidi ifikapo Juni mwaka huu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nchi za Afrika mashariki hazijawahi kuingiliwa na nzige kwa miongo kadhaa

Ethiopia na Somalia hazijawahi kushuhudia nzige wa aina hiyo kwa kipindi cha miaka 25 huku Kenya ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 70, shirika la FAO limesema hivyo mapema wiki hii.

Sudani Kusini na Uganda pia zipo katika hatari ya kuingiliwa na nzige hao ambao wanaendelea kuongezeka na kusambaa.

"Kasi ya kusambaa kwa nzige hao na kiwango ambacho wanavamia maeneo siyo kawaida kiasi cha kuwa changamoto hata kwa mamlaka za eneo na za kitaifa," kulingana na FAO.

Chaguo pekee lililosalia kukabiliana na nzige hao ni kutumia ndege ambazo zinanyunyiza dawa ya kuua wadudu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umoja wa Mataifa yatoa wito wa kupatikana kwa mabilioni ya madola kukabiliana na nzige.

Nzige hao wamesambaa kuanzia Yemen hadi maeneo mengine ya Bahari ya Shamu. Kiwango kikubwa cha mvua mwishoni mwa 2019 kilitengeneza mazingira mazuri yanayochangia uwepo wa wadudu wao.

Tatizo hilo linaendelea kuwa kubwa zaidi kadiri siku zinavyoendelea. Mbali na nzige hao kuongezeka maeneo ya Afrika Mashariki, pia wamejitokza katika nchi za India, Iran na Pakistan, ambao huenda wakabadilika na kuanza kusambaa kwa makundi ifikapo msimu wa chipukizi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nzige wanaweza kuharibu mazao na kusababisha ukame Afrika Mashariki

Nzige wanaweza kusafiri umbali wa kilomita 150 (maili 93) kwa siku na kila nzige mkubwa anaweza kula chakula kiasi kikubwa tu cha chakula kwa siku.

Kundi la nzige kama hivyo mjini Paris linaweza kula kiasi sawa cha chakula kinachoweza kuliwa na nusu idadi ya watu wote Ufaransa kwa siku moja, kulingana taarifa za maelezo za FAO.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Nzige wametoka bahari ya Shamu hadi Yemen

Novemba mwaka jana, Umoja wa mataifa ilionya kwamba huenda nzige wakavamia baadhi ya ameno ya Ethiopia na kusema kuwa huenda wasambaa hadi Ethiopia na Kenya iwapo hawatakabiliwa. Baadhi ya wakulima ncini Ethiopia wa eneo la Amhara walipoteza mazao yao yote.

Mwezi jana, kundi la nzige lililazimisha ndege ya abiria nchini Ethiopia kubadili mkondo wake. Wadudu hao waliingia kwenye injini, kioo na sehemu ya mbele ya ndege, na kulazimika kutua katika uwanja wa ndege wa Addis Ababa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii