Coronavirus: Je tunafaa kuwa na wasiwasi wa kiwango gani kuhusu virusi hivi?

Virusi hivyo vinauwezo wa kusababisha maradhi hatari ya mapafu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Virusi hivyo vinauwezo wa kusababisha maradhi hatari ya mapafu

Kirusi ambacho kilijulikana na wanasayansi pekee kwa sasa kinasababisha ugonjwa hatari wa mapafu nchini China na pia kimetambuliwa katika mataifa mengine.

Zaidi ya watu 100 wanadaiwa kufariki kutokana na virusi hivyo ambavyo vilipatikana katika mji wa Wuhan mwezi Disemba.

Tayari kuna zaidi ya visa 4,500 vilivyothibitishwa na wataalam wanatumai kwamba idadi hyo itaongezeka.

Kirusi kipya kinachowawacha wagonjwa na homa ya mapafu, ni kitu kinachotia wasiwasi na maafisa wa afya kote duniani wamepewa tahadhari.

Je mlipuko huu utadhibitiwa ama hiki ni kitu kilicho hatari zaidi?

Je ni kirusi gani hiki?

Maafisa nchini China wamethibitisha kwamba visa hivyo vinasababishwa navirusi vya Corona. Hii ni familia kubwa ya virusi , lakini ni aina sita pekee vinavyojulikana kuwaambukiza watu.

Kirusi cha SARS kinachosababishwa na Coronavirus, kiliwaua watu 774 kati ya 8098 walioambukizwa katika mlipuko wa ugonjwa huo ulioanza China 2002.

Kuna kumbukumbu kubwa za SARS , hapo ndipo kuna hofu kuu lakini tumejiandaa ya kutosha kukabiliana na aina ya ugonjwa huo, kulingana na Dkt Josie Golding , kutoka wakfu wa Wellcome Trust.

Je dalili zake ni hatari kiasi gani?

Huonekana kuanza na vipimo vya juu vya joto mwilini na kufuatiwa na kikohozi kikavu na baada ya wiki moja, kinasababisha tatizo la kupumua huku wagonjwa wakihitaji usaidizi wa hospitali.

Maambukizi hayo hatahivyo hayamfanyi mtu kutoa kamasi puani ama hata kupiga chafya. Kirusi cha Corona chenyewe kinaweza kusababisha homa mbaya itakaoendelea hadi mgonjwa kupoteza maisha yake.

''Wakati tunapokutana na kirusi kipya cha Corona , tunataka kujua je dalili zake zina hatari gani . Dalili zake ni zaidi ya zile za homa ya kawaida na hilo ndilo linalotia wasiwasi lakini sio hatari kama vile ugonjwa wa SARS'', alisema Profesa Mark Woolhouse , kutoka chuo kikuu cha Edinburgh.

Shirika la afya duniani WHO linasema kwamba ni janga la dharura nchini China , lakini likaamua kutotangaza hali hiyo ya kiafya kama ilivyofanywa na ugonjwa wa homa ya nguruwe na Ebola.

Je kinaweza kusababisha kifo?

Zaidi ya watu 100 wanajulikana kufariki kutokana na virusi hivyo - lakini licha ya kwamba idadi ya vifo miongoni mwa visa vilivyotambuliwa ikionekana kuwa chini , takwimu haziaminiki.

Ni rahisi mno kugawanya idadi ya vifo dhidi ya idadi ya visa vilivyogunduliwa ili kuweza kubaini kiwango cha vifo wakati huu wa mlipuko huo.

Lakini maambukizi yanaonekana kuchukua muda kabla ya kusababisha kifo, hivyobasi ni wagonjwa wengi ambao huenda wakafariki, na haijulikani ni visa vingapi ambavyo havijaripotiwa.

Je virusi hivyo vinatoka wapi?

Virusi vipya hugunduliwa mara kwa mara.

Hutoka katika spishi nyengine ambapo havikugunduliwa hadi kwa wanadamu.

''Iwapo tutafikiria kuhusu milipuko ya siku zilizopita , iwapo ni kirusi kipya cha Corona, huenda utakuwa umetoka kutoka katika hifadhi ya wanyama'', amesema Profesa Jonathan Ball, mtaalam wa virusi katika chuo kikuu cha Nottingham.

Virusi vingi vya ugonjwa wa Corona vilihusishwa na soko la chakula cha baharini kusini mwa China tarehe mosi mwezi Disemba.

Virusi vya SARS vilianza katika popo na baadaye kuwaambukiza paka ambao badala yake wakawaambukiza binadamu.

Na Ugonjwa wa mapafu wa eneo la mashariki ya kati MERS ambao uliwauawa watu 858 kati ya visa 2,494 vilivyorekodiwa tangu ulipozuka 2012, mara kwa mara umedaiwa kutoka kwa ngamia.

Ni mnyama gani?

Muda tu eneo linalohifadhi wanyama ambapo virusi hivyo vinapatikana litakapotambuliwa , tatizo hilo litakuwa rahisi kutatua.

Ijapokuwa baadhi ya viumbe vya baharini vinaweza kubeba virusi vya corona , soko la vyakula vinavyotoka katika bahari ya kusini mwa China pia lina wanyama wa mwituni , ikiwemo kuku, popo, sungura na nyoka ambao ndio vyanzo.

Watafiti wanasema kwamba virusi vipya vinahusishwa kwa ukaribu na vile vilivyopatikana katika popo.

Hatahivyo hatua hiyo haimanishi kwamba popo wa msituni ndio waliosababisha mlipuko huo.

Waliambukiza spishi nyengine iliokuwa ikiuzwa sokoni.

Kwa nini China?

Profesa Woolhouse anasema kwamba ni kutokana na kiwango na idadi ya watu na ukaribu wa watu na wanyama unaozuia ugonjwa huo kusambaa zaidi.

''Hakuna mtu ambaye ameshangazwa kwamba mlipuko mwengine utakuwa China ama katika eneo hilo la duniani,'' anasema.

Image caption Ramani ya China

Je unasambaa vipi kirahisi miongoni mwa wanadamu

Mwanzo wa mlipuko, mamlaka za China ilisema kwamba virusi hivyo havisambai kupitia mtu mmoja hadi mwingine, lakini sasa visa kama hivyo vimetambuliwa.

Wanasayansi sasa wamefichua kwamba kila mtu aliyeambukizwa anawaambukiza kati ya watu 1.4 na 2.5.

Tunajua kwamba hiki sio kirusi ambacho kitachoka na kupotea. Hatua zinazochukuliwa China ikiwemo kuifungia mjini mingine - inaweza kuizuia kusambaa.

Ijapkuwa takwimu hizo ni za mapema sana, zinweza virusi hivyo sawa na vile vya SARS.

Ni wakati gani ambapo walioambukizwa wanaweza kuambukiza wengine?

Wanasayansi wa China wanasema kwamba watu huambukiza kabla ya kuonyesha dalili za virusi hivyo. Muda kati ya maambukizi na dalili uwepo kwa siku 14.

SARS na Ebola unaweza kusambazwa tu mtu anapoanza kuonyesha dalili. Mlipuko kama huo huwa rahisi kuuzuia.

Watambue watu walioathirika na kuwatenga na baadaye kuchunguza wale waliokaribiana nao.

Homa hatahivyo ndio mfano maarufu wa virusi ambao husambaa kabla ya mtu kugundua kwamba ni mgonjwa.

Profesa Wendy Barclay kutoka kwa idara ya magonjwa ya kuambukiza katika taasisi ya Imperial mjini London alisema kwamba ni kawaida kwa magonjwa ya maambukizi ya mapafu kusambaa bila kuonyesha dalili.

''Virusi hivyo husambazwa hewani wakati mtu anapopumua na kuzungumza na mtu aliyeambukizwa'', alielezea.

Haitakuwa kitu cha kushangaza iwapo virusi vipya vya Corona vinafanya kazi hivi.

Hatujafikia kiwango ambacho watu wanasema kwamba huu unaweza kuwa mlipuko kama vile homa ya nguruwe.

Lakini tatizo la kuzuia maambukizi hayo yasio na dalili linafanya kazi ya serikali ya China kuwa ngumu.

Kile ambacho hakijulikani ni je waathiriwa wanaweza kuambukizwa kwa kiwango gani wanapokuwa katika kipindi ambapo ugonjwa huo haujaanza kuonyesha dalili.

Je virusi hivyo vinasambaa kwa kasi gani?

Inaweza kuonekana kana kwamba visa vimeongezeka. Lakini huenda sio la kweli. Visa vingi vinavyoripotiwa huenda vimejitokeza kutokana na uwezo wa China kutambua visa vipya.

Ukweli ni kwamba kuna habari chache kuhusu ongezeko la virusi hivyo.

Lakini wataalam wanasema kwamba idadi ya watu wanaokuwa wagonjwa inawezekana kuwa juu zaidi ya takwimu zilizoripotiwa

Wikendi iliopita, watafiti katika chuo kikuu cha Lancaster walikadiria idadi hiyo wakisema kwamba takriban visa 11,000 vimeripotiwa mwaka huu .

Iwapo ni kweli idadi hiyo itakuwa zaidi ya ile ya virusi vya SARS.

Je virusi hivyo vinaweza kuzaana mwilini?

Ndio , unafaa kutarajia virusi hivyo kuzaana kila mara. Lakini kinachoeleweka ni kwamba ni vigumu kuzungumzia.

Tume ya kitaifa ya afya nchini China imeonya kwamba maambukizi ya virusi vya Corona ynaendelea kuwa thabiti, lakini hawakuweza kuelezea hatari inayosababishwa na virusi hivyo kuzaana.

Hiki ni kitu ambacho wanasaynsi watakuwa wakitaza kwa karibu..

Je mlipuko huu unaweza kuzuiwa vipi?

Tunajua jinsi virusi vipya vitakavyoendelea kusababisha maambukizi na ni vitendo vya mamlaka ya China pekee ambavyo vinaweza kusitisha mlipuko huo.

Hatua nynegine ni kuwazuia watu ambao wameambukizwa kutosambaza virusi hivyo kwa wengine.

Hiyo inamaana kwamba:

  • Kuzuia ziara zinazofanywa na watu.
  • Kushinikiza kuusu kuosha mikono mara kwa mara
  • Kuwatibu wagonjwa katika maeneo yaliotengwa kwa kuvaa vifaa vinavyozuia maambukizi hayo.

Uchunguzi wa kiwango cha juu pia utafanywa ili kuwatambua watu ambao wagonjwa wamekaribiana nao ili kuona iwapo wana maambukizi hayo.

Je kuna chanjo ama tiba yoyote?

Hakuna...

Hatahivyo mpango wa kutengeneza chanjo unaendelea.

Ni matumaini kwamba utafiti kuhusu kutengeneza chanjo ya virusi vya Mers ambavyo pia ni virusi vya Corona itafanya kazi kuwa rahisi.

Na hospitali zinafanyia majaribio dawa za kukabiliana na virusi vya ukimwi kuona iwapo zina athari yoyote kwa waathiriwa.

Mchanganyiko wa dawa mbili - Lopinavir na Ritonavir - ulifanikiwa dhidi ya ugonjwa wa Sars na inafanyiwa majaribio nchini China wakati huu wa mlipuko

Je mamlaka ya China inasemaje kufikia sasa?

Haki miliki ya picha Getty Images

China imefanya kitu cha maajabu jushinda kokote kule duniani kwa kuitenga Wuhan. Vikwazo vya kusafiri pia vimewekwa katika makumi ya miji huku watu milioni 36 wakiathirika.

Makongamano yamepigwa marufuku na vivutio vya utalii ikiwemo sehemu moja ya ukuta mrefu duniani ikifungwa.

Pia marufuku ya uuzaji wa nyama mwituni , ikidaiwa kuwa chanzo cha maambukizi yamewekwa. Wuhan - chanzo cha mlipuko huo - inajenga hospitali mbili mpya zenye vitanda 2,300.

Je ulimwengu unasemaje?

Mataifa mengi ya bara Asia yameongeza uchunguzi dhidi ya abiria kutoa Wuhan na shirika la afya duniani WHO limeonya hospitali ulimwenguni kwamba kuna uwezekano wa mlipuko mkubwa kuripotiwa.

Singapore na Hong Kong zimekuwa zikichunguza abiria wanaotoka Wuhan na kwamba mamlaka za Marekani na Uingereza zimetangaza kuchukua hatua kama hizo.

Hatahivyo kuna maswali mengi kuhusu athari ya hatua kama hizo.

Je wataalam wana wasiwasi gani?

Dkt Golding anasema: Hadi tutakapopata habari zaidi, ni vigumu kujua wasiwasi tulionao.

''Hadi tutakapojua chanzo cha virusi hivi , vitaendelea kutupatia tumbo joto''.

Profesa Ball anasema: Lazima tuwe na wasiwasi kuhusu virusi vyovyote vinavyomuathiri binadamu kwa mara ya kwanza kwa kuwa vimepita vikwazo vya kwanza.

''Vinapokuwa ndani vinaweza kuzaana na kuruhusu kuenea na kuwa hatari zaidi.Hatutaki kupatia virusi hivi fursa''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii