Nzige wahofiwa kusababisha uhaba wa chakula Afrika mashariki

A tourist guide holds a handful of dead locusts in northern Kenya Haki miliki ya picha EPA

Somalia imetangaza hali ya dharura kutokana na kuenea kwa kundi kubwa la nzige katika eneo la Afrika Mashariki.

Waziri wa kilimo nchini humo amesema kuwa wadudu hao wameonekana kuwa tishio kwa kuwa tayari wameshambulia mimea mingi ya chakula na kufanya hali ya usalama wa cha chakula Somali kuwa hatarini.

Kuna hofu kuwa hali hii inaweza kushindwa kudhibitiwa kabla ya muda wa mavuno mwezi Aprili.

Umoja wa mataifa umesema kuwa uvamizi wa nzige wengi kiasi hiki haujawahi kutokea Somalia na Ethiopia kwa miaka 25.

Huku nchi jirani ya Kenya, haijawahi kukutana mashambulizi ya nzige kiasi hiki kwa kipindi cha miaka 70 iliyopita, kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO).

Ingawa Somalia imekuwa nchi ya kwanza kutangaza kuwa na hali ya dharura.

Somalia ambayo imekuwa katika changamoto za hali ya kiusalama haiwezi kutumia dawa ya kunyunyizia kwa kutumia ndege ili kuuwa wadudu hao.

Huwezi kusikiliza tena
Kundi la nzige latatiza ndege kutua

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa usaidizi wa kimataifa kukabiliana na nzige wengi waliovamia maeneo ya Afrika mashariki.

Msemaji wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO), ametoa wito wa kutolewa kwa msaada ili kukabiliana na athari za nzige kama vile ukosefu wa chakula, utapiamlo na kuathirika kwa mfumo wa maisha ya kila siku.

Ethiopia, Kenya na Somalia zinapitia wakati mgumu kukabiliana na na makundi ya nzige ambako hakujawahi kutokea hapo kabla kunakoathiri mazao ya kilimo, limesema shirika la FAO.

Shirika hilo linahofia kwamba idadi ya nzige hao huenda ikaongezeka mara 500 zaidi ifikapo Juni mwaka huu.

Haki miliki ya picha Reuters

Nzige hao wamesambaa kuanzia Yemen hadi maeneo mengine ya Bahari ya Shamu.

Kiwango kikubwa cha mvua mwishoni mwa 2019 kilitengeneza mazingira mazuri yanayochangia uwepo wa wadudu wao.

Tatizo hilo linaendelea kuwa kubwa zaidi kadiri siku zinavyoendelea. Mbali na nzige hao kuongezeka maeneo ya Afrika Mashariki, pia wamejitokza katika nchi za India, Iran na Pakistan, ambao huenda wakabadilika na kuanza kusambaa kwa makundi ifikapo msimu wa chipukizi.

Nzige wanaweza kusafiri umbali wa kilomita 150 (maili 93) kwa siku na kila nzige mkubwa anaweza kula chakula kiasi kikubwa tu cha chakula kwa siku.

Kundi la nzige kama hivyo mjini Paris linaweza kula kiasi sawa cha chakula kinachoweza kuliwa na nusu idadi ya watu wote Ufaransa kwa siku moja, kulingana taarifa za maelezo za FAO.

Haki miliki ya picha Reuters

Novemba mwaka jana, Umoja wa mataifa ilionya kwamba huenda nzige wakavamia baadhi ya ameno ya Ethiopia na kusema kuwa huenda wasambaa hadi Ethiopia na Kenya iwapo hawatakabiliwa. Baadhi ya wakulima ncini Ethiopia wa eneo la Amhara walipoteza mazao yao yote.

Mwezi jana, kundi la nzige lililazimisha ndege ya abiria nchini Ethiopia kubadili mkondo wake. Wadudu hao waliingia kwenye injini, kioo na sehemu ya mbele ya ndege, na kulazimika kutua katika uwanja wa ndege wa Addis Ababa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii