Daniel arap Moi: Maisha yake katika picha

Raisi mstaafu wa Kenya, Daniel arap Moi amefariki akiwa na miaka 95.

Aliiongoza Kenya kwa miaka 24, awali akikonga mioyo ya wananchi na kuungwa mkono na wananchi wake, lakini utawala wake pia ulikumbwa na hali ngumu ya kiuchumi na kashfa za rushwa.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Akiwa kama mjumbe wa baraza la kutunga sheria la Kenya, Daniel arap Moi na Michael Blundell walihudhuria mkutno wa pili wa Lancaster jijini London Februari 1962. Mkutano huo ulijadili uhuru wa Kenya kutoka kwa Uingereza.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Akateuliwa kuwa makamu wa rais wa Mzee Jomo Kenyatta mwaka 1967.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aliapishwa kuwa rais baada ya kifo cha Jomo Kenyatta mwaka 1978.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mzee Moi akikutana na Waziri Mkuu wa India Bi Indira Gandhi uwanja wa ndege Nairobi Septemba 1981.
Haki miliki ya picha PA Media
Image caption Malkia Elizabeth II akihutubia katika dhifa ya kitaifa pamoja na Rais Moi, katika ziara ya siku nne ya Malkia nchini Kenya mwaka 1983.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Akichoma moto shehena kubwa ya pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni 3 ili kuonesha msimamo wake juu ya vita dhidi ya ujangili mwaka 1989.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Akiwaambia maafisa wa chama tawala kipindi hicho Kenya African National Union (Kanu) kuwa mwisho wa siasa za chama kimoja Kenya zimefika tamati mwaka 1991. Mwaka uliofuata alishinda uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Akikagua gwaride la heshima kabla ya kufungua bunge jijini Nairobi mwaka Nairobi mwaka 1992.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Akipungia wafuasi wake baada ya kuapishwa kwa muhula wa mwisho madarakani mwaka 1998.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mzee Moi akikutana na Waziri Mkuu wa India Bi Indira Gandhi uwanja wa ndege Nairobi Septemba 1981.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Daniel arap Moi akiwa pembeni ya rais-mteule Mwai Kibaki wakati wa hafla ya kumuapisha Kibaki mwezi Disemba 2002, na huu ndio ulikuwa mwisho wa utawala wa miaka 24 ya Moi madarakani.