Baadhi ya wakenya kunywa maziwa, soda na vitafunio katika mazishi ya Moi?

Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa vigezo kuhusu kauli ya kutolewa kwa kwa viburudisho vya bure kwa waombolezaji
Image caption Waombolezaji katika mazishi ya rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi wamehimizwa kuwahi mapema kwenye mazishi ili wapate maziwa na viburudisho vingine

Tahadhari picha utakayoiona huenda ikakutisha...

Serikali ya Kenya itatoa viburudisho kwa watu 30,000 wa kwanza kufika katika mazishi ya rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi siku ya Jumatano.

Mratibu wa jimbo la Rift Valley Regional George Natembeya amesema kuwa kutakuwa na viti, soda, maziwa na mikate pamoja na maji kwa watu 30,000 wa kwanza kufika kwenye mazishi na pia watakalishwa kwenye hema.

Bwana Natembeya amesema kuwa waombolezaji waliosalia watakaribishwa tu ndani ya eneo la makazi, lakini hawatapata mahala pa kukaa.

Amesema pia kwamba vitafunio kwa wale watakaohudhuria mazishi wa kwanza vitatolewa: "atakayefika kwanza ndiye atakayepewa wa kwanza ", amesema Bwana Matembeya huku akiwataka waombolezaji kufika mapema kilioni.

Usafiri utatolewa kuanzia mji wa Nakuru hadi katika makazi ya Moi ya Kabarak yapata kilomota 20 (sawa na maili 12.4) kutoka Nakuru mjini.

Baadhi ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa vigezo kauli hiyo ya serikali ya kutolewa kwa viburudisho vya bure kwa waombolezaji.

Kupitia ukurasa wa Twitter Modal realism@MozDefinitely amesema serikali inaogopa sana kuwa idadi ya watu watakaojitokeza kwenye mazishi itakua ya chini, kwa hiyo imelazimika kuwahonga wakenya wasio na ajira kuhudhuria mazishi?.

@kamau_wanjohi anasema njaa na kiu ni kichocheo cha kutosha cha kuwavutia watu kuhudhuiria mazishi:

Nae Kimathi @CounselKimathi anasema wakenya wanapaswa kuangaliwa kama wanaojua wanachokitaka. Tunachokihitaji sio mkate na soda ndogo.. tunaweza kujinunulia hizi wakati wote kwenye maduka. Tunataka kuona maendeleo, alisema kwenye ujumbe huu wa Twitter;

KEN MAPESA alikua na ushauri tofauti, ambapo alisema wangetoa maziwa badala ya soda wakati wa mazishi ndio wakumbuke maziwa aliyoyatoa Moi wakati wa utawala wake kwa watoto wa shule yaliyojulikana kama Maziwa ya Nyayo:

Marehemu Daniel Arap Moi aliaga dunia katika hospitali ya Nairobi Jumanne wiki iliyopita na wakenya mbalimbali wamekua wakipata fursa ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo aliyeliongoza taifa lao kwa muda wa miaka 27.

Image caption Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mkewe Bi Margareth Kenyatta wakitoa heshima zao kwa mwili wa rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi

Mwili wa Hayati Daniel arap Moi utazikwa katika makazi yake ya Kabarak eneo la Nakuru siku ya Jumanne.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii