Barabara za Nigeria : 'Mwanangu wa kiume alikufa kwa ajali ya gari- na sasa ninaongoza magari barabarani'

Monica Dongban-Mensem controlling traffic
Image caption Monica Dongban-Mensem akiongoza magari barabarani

Wakati anapokuwa na muda wake wa ziada, hakimu wa Nigeria Monica Dongban-Mensem huongoza magari barabarani katika mji mkuu, Abuja, miaka minane baada ya mtoto wake wa kiume kuuawa katika ajali ya barabarani na gari lililomgonga kukimbia na kutoweka.

Alipokutana na mwanadishi wa BBC alikua akua amevalia fulana ya blu, miguu ikiwa upande, akitokwa na jasho akitumia mikona yake kwa ukakamavu, huku akiongoza magari katika hali ya hewa yenye kiwango cha nyuzijoto 38C inayochochewa na msongamano mkubwa wa magari katika maeneo ya mji huo mkuu.

Karibu nae alikua amezingirwa na vurugu za medani ya Berger iliyoko katikati mwa jiji la Abuja.

Magari ambayo yalikua yamemekwama kwenye msururu barabarani yalikua yakipiga honi, kutokana na madereva walioshindwa kuvumilia kusubiri aseme "nenda".

Alionekana wazi kuwa alikua anayadhibiti.

"Wanaigeria wengi huwa hawana subra na inaonekana katika uendeshaji wao wa magari ," Hakimu Dongban-Mensem aliiambia BBC.

Image caption Monica Dongban-Mensem (katikati) alipata mafunzo kutoka kwa mamlaka ili kupata ujuzi wa afisa wa usalama barabarani

Hajui ni nani aliyehusika na kifo cha mwanae, lakini anataka kukabiliana na baadhi ya uendeshaji mbaya wa magari anaoushuhudia.

Alianza kuenda kwenye vituo vya magari kuongea na madereva juu ya usalama barabarani nchini Nigeria.

Alichokibaini kilimshitua.

Wengi miongoni mwa madereva hawakua wamepata mafunzo yanayofaa juu ya sheria za barabarani.

Ujinga wa aina hiyo huenda ndio ulisababisha kifo cha mtoto wake na alioazimia kubadili hilo.

Akiwa na umri wa miaka 62- ameanzisha shirika lisilo na faida lililopewa jina la marehemu mtoto wake - Kwapda'as Road Safety Demand - kuwaelimisha madereva juu ya usalama na pia amepanga kuanzisha shule ya kuendesha magari kwa ajili ya madereva wanaoendesha magari ya kibiashara, ambako wanaweza kupat mafunzoya bure.

Accidents and road deaths in Nigeria

Showing data from 2012 - 2018

Source: Federal Road Safety Corps

Kutokana na kutoridhika na hilo, hakumu Dongban-Mensem alitaka kushiriki katika kudhibiti uendeshaji wa magari mwenyewe.

Baada ya wiki kadhaa za mafunzo ya tume ya usalama barabarani alipata ujuzi afisa usalama barabarani wa kuongoza magari.

Hadi ilipofika mwaka 2016, miaka mitano baada ya ajali , ndio alihisi kuweza kutembelea eneo alipofia kijana wake katika mji wa kati mwa Nigeria wa Jos.

"Lengo langu lilikua ni kumpata mtu ambae angalau angeniambia au kunielezea jinsi mwanangu alivyokufa."

Lakini alipofika, alipata uoga, huzuni na hasira kutokana na ghasia alizoziona.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption barabara nyingi za miji ya Nigeria ni maarufu kwa misururu ya magari ya barabarani

Makutano ya Miners, katika eneo la Tundun Wada mjini, ni moja ya maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari , ikiunganisha wilaya kadhaa za kibiashara katika eneo tambarare la mji mkuu Abuja

Aliona kuwa kwamba mpango wa barabara ulikua duni, aliona kuwa sehemu za barabara zinaharibika na hazina alama za barabarani.

'Mtoto wake alikua amelala barabarani'

Ilikua ni miundo mbinu hatari ambayo husababisha ajali mbali mbali kama vile moja ya sababu zilizomuua mtoto wake wa kiume aliyekua na umri wa miaka , 32- Kwapda'as Dongban, mwaka 2011.

"Kwa maoni ya mtu wa kawaida, ninaweza kusema muundo wenyewe wa barabara ni hatari na tuligundua kuwa watu wengi wameuawa katika maeno fulani ya barabara na hakuna serikali ambayo imeweza kutatua tatizo hilo ," alisema.

Unaweza pia kusoma:

Maafisa mjini Jos waliiambia BBC kuwa wanakarabati barabara na wakasema wanawahurumia wale waliowapoteza wapendwa wao katika ajali za barabarani. Lakini afisa mmoja alisema kuwa wanaotembea kwa miguu na madereva wanapaswa kuwajibika kuhusu namna wanavyotumia barabrara.

Watu katika eneo hilo walimwambia Jaji kwamba waliona mtoto wake akiwa amelala barabarani, lakini hawakuweza kumsaidia.

Monica Dongban-Mensem
BBC
I gave up sleep, hoping that my son will walk through the door and give me a big hug"
Monica Dongban-Mensem

"Miguu yake miwili ilivunjika na majirani katika eneo hilo waliangalia kando wakati mwanangu akipata maumivu, kuvuja damu iliyotiririka toka upande mmoja wa barabara hadi mwingine ," Hakimu Dongban-Mensem alisema kwa hasira.

"Alikata roho katika dimbwi la damu yakelakini nina uhakika angenusurika na kifa kama angekimbizwa hospitalini ."

Kijana wake alikua ndio tu amehitimu shahada ya sheria katika chuo kikuu cha jos na alikua amerejea mjini humo kwa ajili ya kuchukua cheti chake.

"Mwanangu alitaka kuwa mwendeshamashtaka bora duniani lakini alikufa kama kuku mtaani baada ya kugongwa na gari ."

Tangu Kwapda'as Dongban alipogongwa na gari, idadi ya watu ambao wameuawa katika barabara za Nigeria imesalia kuwa ni ile ile.

Juhudi za kutaka hukumu ya kifungo cha maisha

Haki miliki ya picha Monica Dongban-Mensem
Image caption Kwapda Samson Dongban alikua ndio amefuzu tu shahada ya sheria

Kwamujibu wa mamlaka ya shirikisho ya usalama wa barabarani nchini Nigeria (According to the Federal Road Safety Corps), idadi ya vofo ilishuka kidogo mwaka 2013, lakini tangu wakati huo kati ya watu 5,000 na 6,000 wamekua wakifa kila mwaka kutokana na ajali za barabarani.

Hii inamaanisha kuwa watu 13 hufa kila siku.

Nyingi kati ya ajali husababishwa na madereva walio na vibali, ambalo ni tatizo la mara kwa mara, maafisa wanasema. Mwezi Mei 2019, kwa mfano zaidi ya watu 60,000 mjini Lagos walikua wakiendesha gari bila vibali.

Zaidi ya hayo, hakuna taarifa za usajiri wa magari au kamera za kunasa utambulisha wa madereva wa magari yanayotoroka

Hii inaleta ugumu wa kufuatilia madereva wanaogonga watu na kukimbia, kama aliyemgonga mtoto wa hakimu Dongban-Mensem.

Ambulance on Nigerian road
BBC
Road safety in Nigeria

  • 200 millionpeople

  • 12.5 millionvehicles

  • 5,181deaths on the roads in 2018

  • 965accredited driving schools

Source: FRSC

Kama maderava wanaogonga watu na kukimbia wakikamatwa wanaweza kushitakiwa kwa kuua na kukabiliwa na kifungo cha miaka 14 jela , iwapo watapatikana na hatia.

Hakimu Dongban-Mensem anahisi hii haitoshi. Anasema wale wanaopatwa na hatia wanapaswa kufungwa kifungo cha maisha na familia za waliouawa wapewe fidia ya pesa.

Lakini hii bado huenda isitoshe kukabiliana na maumivu ya kumpoteza mpendwa wako.

"Nilishindwa kulala, nikiwa na matumaini kwamba kijana wangu atapita mlangoni na kunikumbatia.

"Pia niliacha sahani ya chakula mezani nikitumai atarejea nyumbani akiwa na njaa," alisema.

Hataki mama mwingine apitie haya na ameazimia kupeleka ujumbe wa usalama wa barabarani katika kila mtaa wa nchi ya Nigeria.

"Nitaridhika tu kama hakuna Mnigeria atakufa kutokana na ajali ya barabarani," alisema..

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii