Je, ni nani nchini Sudan atakayefanya uamuzi wa kumwasilisha Omar el Bashir katika mahakama ya ICC?

Rais wa zamani wa Sudan Omar el Bashir Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waendesha mashtaka Sudan walimshtaki Omar al-Bashir kwa makosa ya kuwaua waandamanaji

Tangazo la maafisa wa Sudan kwamba washukiwa wanaosakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kuhusu uhalifu uliodaiwa kufanywa katika jimbo la Darfur wanafaa kuwasilishwa mbele ya mahakama hiyo limetoa matumani miongoni mwa wanaharakati wanaomtaka aliyekuwa rais wa taifa hilo kupelekwa katika mahakama hiyo , lakini kuna maswali mengi kuhusu lengo na maana ya hatua hiyo.

Bashir na wengine wanatuhumiwa na makossa mabaya ya uhalifu katika mzozo wa jimbo la magharibi la Darfur ambao ulianza 2003.

Takriban watu lakini 300,000 waliuawa katika ghasia hizo. Baada ya mazungumzo kati ya maafisa wa serikali na waasi wa Darfur , mwakiishi wa serikali Mohammed Haasan al -Taishi alisema kwamba pande zote mbili zilikubaliana kwamba ili haki kupatikana wale waliokuwa wakisakwa na ICC watalazimika kuwasilishwa mbele ya jopo la majaji hao.

Je maafisa hao waliyasikia maneno yake vizuri?

"Kulingana na stakhabadhi za haki na maridhiano, nitawaambia kwa uwazi wote kwamba tulikubaliana na taasisi inayoshughulikia kutafuta haki katika kipindi cha mpito'' , alisema al- Taishi katika runinga ya serikali.

''Tulikubaliana kuhusu maswala manne ili kupata haki katika kipindi cha mpito. Kwanza tulikubaliana kwamba wale ambao agizo la kuwakamata limetolewa wanapaswa kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC . Ninasema hili kwa uwazi wote'', alisema.

''Na pia tulikubaliana kuhusu mahakama maalum ya uhalifu ya Darfur''.

''Hii ni mahakama maalum iliopewa jukumu la kuchunguza na kufanyia kesi majaribio ikiwemo kesi za ICC'', aliongezea akizungumza kwa lugha ya Kiarabu.

Al- Taishi alitumia neno muthul{ kuhudhuria} na sio taslim{kuwasilishwa}.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walisema kwamba Taishi alitumia neno Muthul. Hatahivyo baadaye aliambia kipindi cha redio cha BBC focus ,kwa lugha ya kiingereza kwamba Bashir na wengine watawasilishwa mbele ya mahakama ya ICC.

Hiyo inamaanisha kwamba kwanza kesi ya Bashir italazimika kujaribiwa katika mahakama maalum nchini Sudan , kabla ya uwezekano wa kuwasilishwa katika mahakama ya ICC.

Haijulikani iwapo Taishi hakutaka kuwa wazi kwa makusudi.

Je ni nani atakayefanya uamuzi kuhusu Bashir?

Mnamo tarehe 20 mwezi Januari , waasi wa Darfur na serikali walikubaliana kuanzisha mahakama maalum ili kuchunguza na kuwashtaki wale waliohusika na uhalifu wa kivita mbali na uhalifu dhidi ya binadamu huko darfur.

Haijulikani iwapo makubaliano hayo ya hivi karibuni yalioafikiwa na pande hizo mbili yanahitaji kuidhinishwa na vyama vingine, hususan kile cha baraza kuu linalotawala. Taishi ni mwanachama wa baraza hilo.

Wakati alipochukua mamlaka mwaka uliopita Luteni Jenerali Abdel Fattah Burhan alisema kuwa uamuzi wa kumwasilisha Bashir katika mahakma ya ICC utakuwa uamuzi wa serikali iliochaguliwa na rais.

Baadaye alisema kwamba mahakama za Sudan zina uwezo wa kushtaki.

Serikali ya kiraia iliopo sasa inayoongozwa na waziri mkuu Abdala Hamdok ilichaguliwa baada ya makubaliano katika vyama vinavyoungwa mkono demokrasia na wanajeshi waliochukua mamlaka mnamo mwezi Aprili.

Hadi serikali iliochaguliwa na raia itakapochukua mamlaka , baraza kuu linalotawala kwa sasa ndilo litakaloamua maswala ya taifa hilo.

Siku chache zilizopita , bwana Hamdok alisema kwamba baraza lake la mawaziri halikuambiwa mapema kuhusu mkutano kati ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Burham.

Baada ya mazungumzo nchini Uganda, Netanyahu alisema kwamba makubaliano yaliafikiwa kuimarisha uhusiano kati ya Sudan na Israel - ikiwa na hatua kubwa.

Ni akina nani wengine wanaopaswa kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC

Waasi wa Darfur na vikosi vinavyopigania demokrasia vimemtaka rais huyo wa zamani kuwasilishwa katika mahakama ya ICC.

ICC ilitoa vibali viwili vya kukamatwa dhidi ya Bashir kwa madai ya kutekeleza uhalifu wa kivita, ule wa kibinadamu na baadaye mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.

Wengine wanaosakwa na mahakama ya ICC ni Ahmed Harun, aliyekuwa gavana wa jimbo la kusini la Kordofan, Abdel Rahim Mohammed Hussein,aliyekuwa waziri wa ulinzi; Ali Kushayb, kiongozi wa wapiganaji, na Abdallah Banda Abaker Nourain, aliyekuwa kamanda wa vuguvugu la waasi kuhusu usawa la Justice and Equality Movement (JEM) .

Kesi dhidi ya Bashir inaweza kumhusisha Burhan na naibu wake Luteni jenerali Mohammed Hamdan Dagalo maarufu Hemeti.

Wawili hao waliunga mkono kampeni za serikali dhidi ya waasi wa Darfur.

Huku ikiwa kuwasilishwa kwake katika mahakama ya ICC kutapongezwa na mataifa ya magharibi, kutaleta wasiwasi katika mataifa ya Ghuba na mataifa mengine ya Afrika, ambayo yanatilia shaka mahakama ya ICC .

Makubaliano hayo yanajiri wakati ambapo serikali hiyo ya mpito inakabiliwa na shinikizo kali za kiuchumi na kisiasa.

Makubaliano hayo yanaweza kutumiwa kupunguza hasira kali ambayo imesababisha maandamano madogo madogo katika siku zilizopita.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii