Kijana anayetumia uchafu kutengeneza spika Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Wilgrand Lubida: Mvumbuzi anayetumia uchafu kutengeneza spika Tanzania

Wilgrand Lubida ambaye ana umri wa miaka 27 alianza kufanya hivi miaka 12 iliopita wakati alipokuwa mwanafunzi wa shule ya upili.

Alikuwa akizunguka kila mahali akiokota vifaa vichafu vya kielektroniki ili kutengeneza bidhaa mpya. Mwanzo alikua akijitengenezea bidhaa zake, baadaye marafiki zake na familia na baada ya muda mfupi alianza kupata maombi kutoka kwa watu wengine.

Na sasa soko lake limepanuka hadi maeneo mengine na mara nyingine mahitaji yanazidi uwezo wake wa kutengeneza.

Picha na habari: Eagan Salla

Mada zinazohusiana