Je umewahi kuona nyani na simba pamoja?

Nyani akimlinda mwaka wa simba Haki miliki ya picha Kurt Safari
Image caption Nyani akimlinda mwaka wa simba

Afisa mmoja wa utalii nchini Afriika Kusini ambaye alifanikiwa kupata picha isio ya kawaida ya nyani akimbeba mwana wa simba katika mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Kruger, amesema kwamba hajawaona tena wanyama hao tangu alipowapiga picha hiyo wiki iliopita.

Katika taarifa kwa BBC, mkurugenzi wa Kurt Safari , alisema kwamba msimu wa mvua umefanya kuwa vigumu kuwaona wanyama hao.

''Ni msimu wa mvua katika mbuga ya Kruger na miti imekuwa mikubwa huku nyasi zikiwa ndefu. Wakati nyani wanapoondoka katika barabara na kuingia katika nyasi , sio rahisi kuwaona''.

Picha hiyo ilileta shauku kubwa huku wengine wakisema kwamba ulikuwa ukweli wa filamu ya rafiki na simba.

Haki miliki ya picha Kurt Safari
Image caption Nyani akimbeba mwana wa simba katika mbuga ya Kruger Afrika kusini

Bwana Schultz alisema kwamba mwana huyo wa simba ambaye alikuwa amebebwa na nyani huyo alikuwa hatarini pengine.

''Nyani huyo wa kiume aliruka kutoka tawi moja hadi jingine akimbeba simba huyo mdogo kwa muda mrefu. Mwana huyo wa simba alionekana kuchoka na ijapokuwa hakuonekana kuwa na jeraha huenda alikua ameumia''.

''Nimeshuhudia nyani wakiwashambulia watoto wa chui na nimesikia nyani wakiwaua watoto wa simba lakini sijawahi kuona jinsi nyani anavyomlea vizuri mwana wa simba''.

Bwana Schultz aliongezea kwamba hadhani kwamba mwana huyo wa simba ataendelea kuishi.