Wanawake Nigeria wajiunga na darasa la ndondi ili kujihami
Huwezi kusikiliza tena

Nigeria ni miongoni mwa nchi zilizo hatari ulimwenguni kwa wanawake kuishi

Wanawake nchini Nigeria wanakabiliwa na hatari ya kudhalilishwa, kubakwa na hata kunyanyaswa kingono, hivyo wanawake jijini Lagos wameamua kuingia kwenye darasa la ndondi ili waweze kujifunza namna ya kujihami na kujilinda dhidi ya hatari itakayowakabili.