Uvamizi wa nzige: Umoja wa Mataifa watoa tahadhari ya njaa katika Ethiopia, Kenya, Uganda, Tanzania na Somalia

Nzige Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kuna hofu ya mabilioni ya nzige-ambazo zinaweza kuongezeka

Kanda ya Afrika Mashariki inaweza kukumbwa na njaa kama wimbi la nzige wanaokula mimea kwa haraka na malisho ya mifugo hawatadhibitiwa, afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC.

Itasababisha mzozo wa chakula, Dominique Burgeon, mkurugenzi wa shughuli za dharura wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa(FAO), amesema.

Ethiopia, Somalia, Kenya, Tanzania na Uganda zimeathiriwa na nzige.

Unaweza pia kusoma:

Juhudi za kudhibiti wadudu hao hadi sasa hazijafanikiwa.

Unyunyiziaji wa dawa ya kuua wadudu ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na nzige lakini nchi katika kanda hiyo hazina raslimali zinazofaa kukabiliana nao.

Kuna hofu kwamba nzige - ambao tayari wamefikia mabilioni wanaweza kuongezeka zaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nzige hao wamesambaa kuanzia Yemen hadi maeneo mengine ya Bahari ya Shamu.

Shirika la chakula FAO linasema wadudu hao wanazaliana haraka sana kiasi kwamba idadi yao inaweza kuongezeka mara 500 kufikia mwezi Juni.

Umoja wa mataifa sasa unaitolea wito Jamii ya kimataifa itoe takriban dola milioni 76 kudhamini usambazaji wa dawa katika maeneo yaliyoathiriwa.

" Kama haitafanya hivyo, hali itakua mbaya zaidi, halafu mtahitaji kutoa msaada mkubwa wa chakula kwa ajili ya hali ya kibinadamu hali ambayo inaweza kudhibitiwa ," Bwana Burgeon amesema

Haki miliki ya picha FAO
Image caption Nzige hula tani za mazao kwa siku

Somalia imetangaza hali ya dharura kufuatia mzozo wa nzige.

Serikali ya Ethiopian imetoa wito wa kuchukuliwa kwa "hatua za mara moja" za kukabiliana na tatizo la nzige ambao wamevamia majimbo manne kati ya tisa ya nchi hiyo.

Kenya imetuma ndege kunyunyiza dawa katika mikoa kadhaa, huku Uganda ikipanga kutuma wanajeshi katika mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo kunyunyiza dawa ya kuua wadudu hao katika maeneo yaliyoathiriwa.

Nzige hao wanaaminiwa kutoka katika nchi ya Yemen miezi mitatu iliyopita. Uvamizi wa nzige ni mbaya kuwahi kushuhudiwa nchini Kenya kwa miaka 70 na mbaya kuwahi kushuhudiwa nchini Ethiopia kwa miaka 25.

Unaweza pia kutazama:.

Huwezi kusikiliza tena
Kundi la nzige latatiza ndege kutua

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii