Marufuku ya Manchester City: je ina maana gani kwa klabu hiyo?

Man City haijamailiza chini ya nafasi nne katika misimu tisa iliopita Haki miliki ya picha Empics
Image caption Man City haijamailiza chini ya nafasi nne katika misimu tisa iliopita

Manchester City imepigwa marufuku kushiriki katika ligi ya mabigwa Ulaya kwa misimu miwili ijayo baada ya kupatikana wamekiuka sheria za Uefa zinazoambatana na masuala ya fedha na leseni.

Mabingwa hao wa ligi ya Premier pia wamepigwa faini ya £25m.

Hata hivyo uamuzi huo unaweza kupingwa katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.

Manchester City imesema kwamba hatua hiyo ni jambo la kukatisha tamaa lakini halikuwashangaza na watakata rufaa.

Bod ya udhibiti wa masuala ya fedha imesema City imevunja sheria kwa kuweka kiwango cha juu zaidi cha fedha katika mapato yake ya ufadhili kwenye hesabu zake na katika ripoti ya fedha iliyowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 ikionesha kwamba hawakupata hasara wala faida", na kuongeza kwamba klabu hiyo haikushirikiana na wachunguzi".

Imesemekana kwamba City huenda pia ikapunguziwa pointi katika ligi ya Premier kwasababu sheria ya udhibiti wa masuala ya fedha katika ligi ya Premier kwa kiasi kikubwa inafanana na Uefa japo hazifanani moja kwa moja.

Hata hivyo, adhabu hiyo haitakuwa na athari zozote kwa timu ya wanawake ya City.

Kwanini Man City huenda isishiriki ligi ya mabingwa?

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Manchester City: "Klabu hiyo imekuwa ikifikiria umuhimu wa kuwa na bodi huru na kufuatwa kwa mchakato usiopendelea upande wowote kuangalia ushahidi wao ulio wazi.

"Disemba 2018, mchunguzi mkuu wa Uefa alisema wazi vikwazo ambavyo anataka City iwekewe hata kabla ya uchunguzi kuanza kufanywa.

"Kasoro na udhaifu uliopo katika mchakato wa Uefa kwenye uchunguzi alioongoza, hakukuwa na shaka na matokeo ya uchunguzi huu. Klabu hii awali ilikuwa imewasilisha malalamiko yake kwa bodi ya nidhamu ya Uefa, ambayo yaliidhinishwa na mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo.

"kwa maneno rahisi, hii ni kesi iliyowasilishwa na Uefa, ikashtakiwa na Uefa na aliyetoa uamuzi ni Uefa. Kwa mchakato wa kibaguzi aina hii ambao umemalizika, klabu hii sasa itatafuta hukumu isiyopendelea upande wowote haraka iwezekanavyo na hivyo basi, kwanza kabisa itaendelea na mchakato wake katika mahakama ya usuluhishi wa migogoro ya michezo bila kuchelewa."

City imepangwa kucheza na Real Madrid katika timu 16 za mchujo za ligi ya mabingwa huku mchuano wa kwanza ukiwa ni Februari 16 katika uwanja wa Bernabeu.

Rais wa La Liga Javier Tebas iliisifu Uefa kwa kuchukua hatua stahiki.

"Kuhakikisha utekelezaji wa sheria ya udhibiti wa fedha na kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria hiyo ni jambo la msingi kwa hatma ya mpira wa kandanda," amesema.

"kwa miaka mingi tumekuwa tukitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua muafaka dhidi ya Manchester City na Paris Saint-Germain, na hatimaye tumepata mfano bora na ni matumaini yetu kwamba hili litaendelezwa. Ni kheri kuchelewa kuliko kutochukuliwa kwa hatua kabisa."

Na Je wachezaji

Haki miliki ya picha Rex Features

Tayari tunajua kwamba kiungo wa kati wa miaka mingi David Silva atakuwa akiondoka mwisho wa msimu . Lakini idadi ya wachezaji ambao kandarasi zao zinakaribia kukamilika kabla ya City kurejea katika mechi za klabu bingwa inatia wasiwasi.

Mshambuliaji Sergio Aguero yupo katika orodha hiyo. Mkataba wake unakamilika 2021 . Mkataba wa Leroy Sane nao unakamilika wakati huohuo.

Kandarsi ya John Stones inakamilika mwaka huohuo. Mkataba pia utamuathiri Nicolas Otamendi.

Na je hatma ya nyota ambao kandarasi zao zinakamilika mwisho wa 2022 kama vile Kevin de Bryune Ederson, Bernado Silva , Raheem Sterling na Riyadh Mahrez? iwapo Guardiola ataondoka , ni rahisi kuona idadi kubwa ya wachezaji ikiondoka, ikimaanisha kwamba huenda City ikawachwa na kibarua kikubwa cha kuanza kujijenga upya.

Je hali ya kifedha ya City ikoje?

Haki miliki ya picha PA Media
Image caption Mmiliki wa klabu ya man City Sheikh mansour kushoto

Hiki ndicho kitu kisichoitia kiwewe City kwa kuwa kila mtu anajua kwamba klabu hiyo ni tajiri. Kila mtu pia anajua kwamba Manchester United imekuwa ikijaribu kushiriki katika ligi ya mabingwa katika siku za hivi katribuni.

Arsenal imekosa kushiriki misimu mitatu mfululizo. Chelsea ilishindwa kushiriki msimu uliopita. Liverpool ilishindwa kufuzi mwaka 2015.

Ni kweli kwamba watakosa mamilioni ya fedha lakini hilo halitaiathiri sana klabu hiyo. Pengine ugumu mkubwa utakuwa kukosa fursa ya kupata alama ikimaanisha kwamba hata iwapo watarudi , klabu hiyo itakuwa klabu ya chini zaidi ya walivyotarajia kuwa na hivyobasi kupata ugumu kufika katika awamu za mwisho za mashindano hayo.

Je huu ndio mwisho wa Guardiola?

Image caption Pep Guradiola amekuwa akichezea Man City tangu 2016

Na Simon Stone, mwanahabari wa BBC Michezo

Kwa wakati mwengine katika kipindi cha wiki chache zilizopita, mkufunzi wa City Pep Guradiolaamejibu kuhusu hatama yake kwa kuelezea malengo yake ya kuhakikisha kuwa kandarasi yake inakamilika 2021.

Pia amesema kwamba anaamini uongozi wa City uliomkakikishia kwamba hakuna ukweli wowote kuhusu madai yanayochunguzw ana Uefa. Je Guardiola anahisi kusalittiwa na matokoe hayo? na anashindwa kusema.

Hatahivyo ni sawa kufikiria kwamba baada ya kushinda mechi nyingi katika ligi ya Premia mbali na kuwa klabu ya kwanza kushinda mataji matatu kwa mpigo , Guradiola huenda akapoteza motisha aliokuwa nayo.

Iwapo City itashinda kombe la ligi ya mabingwa, Guradiola anaweza kuondoka hatahivyo.

Sasa sio rahisi kufikiria kwamba atasalia huku kukiwa na uvumi kwamba Juventus inamnyatia, ndhini kwamba uwepo wake katika klabu hiyo kutategemea iwapo rufa iliokatwa na klabu hyo itafanikiwa.

Je kinyang'anyi cha timu nne bora kitakuwa cha timu tano bora?

Katika mechi za wikendi hii , Chelsea ilikuwa na pointi mbili mbele ya Sheffiled katika shindano la kuwania nafasi ya nne ya ligi ya Uingereza.

Hatahivyo haijulikani kile kitakachotokea iwapo City itaondolewa lakini iwapo Uefa itaamua kuchukua timu nne za England na timu iliopo katika nafsi ya tano kuchukuliwa, kutakuwa na makabiliano makali katika hatua hiyo.

Kutoka Sheffiled United iliopo katika nafasi ya tano hadi Crystal Palace iliopo katika nafasi ya 14, kuna alama tisa zinazozitawanya timu 10.

Kutoka kuona kwamba huenda isifuzu katika ligi ya mabingwa . Arsenal huenda ikarudi kwa goli moja.

Nini ambacho City inadaiwa kufanya?

Uefa ilianzisha uchunguzi baada ya gazeti la Ujerumani Der Spiegel kuchapisha nyaraka za siri zilizovuja Novemba 2018 zilizodai kwamba City iliweka kiwango kikubwa cha makubaliano ya ufadhili wao na kupotosha bodi ya soka ya Ulaya.

Taarifa hiyo ilidai kwamba City - ambayo kila wakati imekuwa ikikanusha kufanya makosa - ilipotosha Uefa kwa kukusudia ili iweze kutimiza sheria ya FFP inayotaka vilabu kufikia kiwango cha fedha ambacho siyo kuwa na hasara wala faida.

City ilipigwa faini ya £ milioni 49 mwaka 2014 kwasababu ya kosa la awali la kukiuka sheria.

Sheria za FFP zinasemaje?

Sheria ya udhibiti wa fedha ilianzishwa na Uefa kuzuia vilabu kutumia fedha nyingi kuliko uwezo wao katika msindano wanayoshiriki na kukomesha kile ambacho wakati huo rais Michel Platini alikiita udanganyifu wa kifedha ndani ya mpira wa kandakanda.

Chini ya sheria hizo, uwezekano wa vilabu kupata hasara unakuwa mdogo mno na pia vinajukmu la kuhakikisha kwamba wanaweza kugharamia pesa wanazotumia wakati wa usajili wa wachezaji na kulipa wafanyakazi wao kama inavyotakikana.

Vilabu vinahitajika kuwa na uwiano- wenye kuhusishwa na matumizi - usajili na mishahara - pesa wanazopata kutokana na tiketi za mechi wanazouza, pamoja na mapato mengine yanayopatikana na idara zao za biashara. Pesa zinazotumika katika viwanja, vituo vya kufanyia mazoezi, miradi ya uendelezaji wa vijana au jamii huondolewa katika hilo.

Bodi ya udhibiti wa fedha iliyoanzishwa na Uefa, ina uwezo wa kupiga marufuku vilabu kushiriki mashindano ya Uefa pamoja na adhabu zingine ikiwemo kutoa onyo, kutoza faini, kuzuilia pesa zilizokuwa zitolewe kama zawadi, marufuku ya usajili, kupunguza pointi, kupiga marufuku usajili wa wachezaji wapya na masharti ya idadi ya wachezaji ambao wanaweza kusajiliwa katika mashindano ya Uefa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii