Je ni kwanini asilimia 66 ya raia wa Nigeria hawatumii mipira ya kondomu?

Condom Haki miliki ya picha Getty Images

Asilimia 34 pekee ya raia wa Nigeria wanatumia mipira ya kondomu wakati wa kufanya mapenzi, kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la NOIPolls.

Shirika la NOIPolls limesema matokeo yanaonesha kwamba asilimia 28 pekee ya idadi yote ya watu wanaotumia kondomu hutumia mipira hiyo kila wakati wanaposhiriki mapenzi.

Hilo linajitokeza licha ya kwamba wengi waliohojiwa wana uwezo wa kununua mipira hiyo.

Chike Nwangwu, mkurugenzi mkuu wa NOIPolls, ameiambia BBC kwamba dini na wapenzi kukataa kutumia kondomu ni miongoni mwa sababu kuu za wapenzi kukataa kutumia mipira ya kondomu.

"Maono na mitazamo ya watu juu ya kondomu, asilimia 63 ya raia wa Nigeria walisema kwamba cha kwanza kinachowajia akilini ni kwamba wanaposikia neno kondomu mtu anataka kujifurahisha kingono, huku asilimia 45 wakisema kwamba wao moja kwa moja kinachowajia akilini wanapomuona mtu na kondomu ni usherati," amesema.

Akitangaza matoeko ya utafiti huo huko Abuja, Nwangwu alisema asilimia 83 ya raia wa Nigeria wanaamini kwamba mipira ya kondomu inastahili kutumiwa lakini ni asilimia 34 pekee waliokubali kwamba wanaitumia.

Aidha alisema kwamba asilimia 26 ya waliohojiwa wanatumia mipira ya kondomu kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa.

Bwana Nwangwu alisema kwamba utafiti huo ulifanywa kupitia maswali na kufasiriwa kwa lugha nne kuu nchini Nigeria, Pidgin, Yoruba, Hausa na Igbo.

Katika hotuba yake, mkurugenzi mkuu wa NACA, Gambo Aliyu, alisema matokeo ya utafiti huo yatawezesha serikali kubaini mianya iliyopo na kusaidia kukabiliana na virusi vya ukimwi.

Bwana Aliyu alisema kwamba uhamasishaji wa matumizi ya mipira ya kondomu siyo kuendeleza usherati miongoni mwa raia.

"Hatuendelezi usherati, bali kuhamasisha watu kuhusu kuzuia, maadili na tunataka watu kuwajibika.

"Tunahamisha watu kuwajibika lakini katika mchakato huo kuzuia ugonjwa wa Ukimwi ni jambo muhimu na ugonjwa huo unastahili kudhibitiwa ndani ya kipindi kifupi kabisa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii