Benjamin Griveaux: Video ya ngono yamfanya mshirika wa Macron kujiuzulu

Former government spokesperson and La Republique en Marche (LREM) candidate for the upcoming Paris 2020 mayoral election Benjamin Griveaux on 14 Feb Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakati anajiuzulu, Bwana Griveaux alisema hakuna anayestahili kuharibiwa sifa

Video ya ngono imemaliza ndoto ya mgombea wa chama tawala cha Ufaransa Benjamin Griveaux ya kuwa meya wa mji wa Paris.

Aliyekuwa msemaji wa serikali ya Rais Emmanuel Macron, ambaye tayari alikuwa anayumba yumba kwenye kinyang'anyiro alilengwa na msanii wa Urusi aliyemshtumu kwa unafiki.

"Hakuna ambaye anastahili kupitia unyanyasaji huo," amesema Bwana Griveaux, 42.

Video hiyo inaonesha mwanamume akiwa katika hali tatanishi, ilisambaa kwa haraka katika mitandao ya kijamii Alhamisi jioni.

Petr Pavlensky, raia wa Urusi aliyeomba hifadhi ya ukimbizi, alisema kwamba ameweka video hiyo mtandaoni.

Wanasiasa Ufaransa wamesema nini?

Wapinzani kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa walionyesha hasira yao.

Meya wa sasa Anne Hidalgo alitoa wito wa kuheshimu maisha binafsi ya watu, huku kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon akishtumu tukio hilo na kulitaja kama la kuchukiza.

Kiongozi wa mrengo wa kulia Marine Le Pen alisema kwasababu ya demokrasia, Bwana Griveaux hakuwa na haja ya kujiuzulu.

Benjamin Griveaux
AFP
My family doesn't deserve this. I'm not prepared to expose my family and myself any more when all these attacks are allowed. This goes too far
Benjamin Griveaux
Ex-candidate for Paris mayor

Waziri Mkuu Edouard Philippe ameonesha kumuunga mkono aliyekuwa mfanyakazi mwenzake na waziri wa ndani Christophe Castaner na kuonya kwamba kuweka mtandaoni video kama hizo bila idhini ya mhusika ni kosa ambalo mtendaji anaweza kuadhibiwa na kutozwa faini kubwa na kifungo cha hadi miaka miwili jela.

Video hiyo ilionekana kwenye tovuti ambayo haifahamiki na wengi na kuandamana na wasifu wa Griveaux na malengo yake ya kisiasa pamoja na imani yake kali katika maadili ya familia.

Kisha makala iliyoandikwa iladai kwamba bwana Griveaux alikuwa amebadilishana ujumbe wa mapenzi kwa njia ya simu na mwanamke kijana na kumtumia video binafsi.

Kiunganishi cha kwenye mtandao ya kijamii kilisambazwa na mbunge ambaye alilazimika kujiuzulu kutoka kwa chama cha Macron mwishoni mwa mwaka 2018.

Bwana Griveaux amekiambia kituo cha BFMTV kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, yeye na familia yake wameharibiwa sifa, wamesemwa kwa maneno ya uwongo, uzushi, kushambuliwa na watu wasiowafahamu na hata kupata vitisho vya kifo.

"Uchafu huu umeniathiri mimi na zaidi kuumiza watu ambao ninawapenda."

Wakili wa Griveaux amesema kuwa atawasilisha mashtaka dhidi ya video iliyowekwa mtandaoni ambayo alisema inakiuka faragha ya mtu.

Petr Pavlensky ni nani?

Bwana Pavlensky ambaye anasema kwamba aliweka video hiyo mtandaoni, alikimbia Urusi na kuomba hifadhi Ufaransa alipokuwa anashutumiwa na serikali kwa kutenda unyanyasaji wa kingono madai ambayo anayakanusha.

Alihudumia kifungo ch amiaka saba jela kwa kuwasha lango la Shirika la Ujasusi Moscow. Na baadae akasababisha majeruhi kidogo katika jengo la Banque de France branch kwa sababu ya moto huo.

Aliliambia shirika la habari la Ufaransa la LCI, kwamba bwana Griveaux alikuwa mwanasiasa wa kwanza tu anayemlenga lakini ni wengi. Wanasiasa wanastahili kuwa wakweli na anasema kwamba ataendelea kupiga vita propaganda na wanasiasa wanaojifanya kuwa maadili makali".

Vyombo vya habari vya Ufaransa kawaida havina tabia ya kuchunguza maisha binafsi ya watu na watu maarufu kadhaa wameonesha kuchukia siasa zinazoonekana kuiga mkondo wa Marekani. "Sipendi watu kuchanganya maisha binafsi ya watu na siasa," amesema mbunge Alexis Corbière.

Wakili Marie-Anne Soubré amezungumza na kipidi kimoja cha runinga Ufaransa na kusema amekasirishwa kuona kule siasa za Ufaransa zilipofikia. "Tumetetereka vipi kiasi kwamba mtu yuko tayari kuchapisha taarifa kama hizi kuharibu siasa?"