Kinamama Tanzania wanavyowaosha watu miguu kujikimu kimaisha

Msimu wa mvua maeneo mbalimbaili ya Afrika mashariki umekuja na adhabu kwa baadhi ya watu huku wengine wakiona fursa. Nchini Tanzania baadhi ya kina mama wameanza biashara ya kuosha watu miguu pindi wanapotoka sokoni kama sehemu ya kujipatia kipato. Biashara hii imeshamiri hasa wakati huu mvua na ikichangiwa na miundombinu mibovu ya masoko inayosababisha matope mengi.