Makubaliano kati ya Kagame na Museveni: Serikali ya Uganda yawaachilia raia 13 wa Rwanda

  • Isaac Mumena
  • BBC Swahili
Serikali ya Uganda imewaachia huru raia wengine 13 wa Rwanda waliokuwa wamezuiliwa katika korokoro zake wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali.
Maelezo ya picha,

Serikali ya Uganda imewaachia huru raia wengine 13 wa Rwanda waliokuwa wamezuiliwa katika korokoro zake wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Serikali ya Uganda imewaachia huru raia wengine 13 wa Rwanda waliokuwa wamezuiliwa katika mahabusu zake wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Raia hao ikiwemo wanawake watatu wamekabidhiwa kwa maafisa wa uhamiaji wa Uganda mbele ya mwakilishi wa ubalozi wa Rwanda nchini Uganda.

Hili ni kundi la pili baada ya Wanyarwanda wengine kukabidhiwa mapema mwezi wa Januari mwaka 2020, katika hatua ya kumaliza uhasama uliopo kati ya mataifa hayo.

Hatua hiyo inajiri baada ya rais Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake Yoweri Museveni wa Uganda kukutana na kuafikiana kuhusu kuimarisha uhusiano kati yao ili kumaliza uhasama uliopo.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uganda Sam Kutesa amewakabidhi Wanyarwanda hao leo mchana katika hoteli ya Serena mjini Kampala mbele ya wandishi wa habari pamoja na mwakilishi wa ubalozi wa Rwanda nchini Uganda Noel Mukyo.

Kwa mjibu wa waziri huyo rai hao wa Rwanda ni wale waliokamatwa mwaka 2019 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya kukutwa na silaha

''Serikali ya Uganda imeamua kuwaachia huru raia wengine 13 wa Rwanda ukiongeza kwa wale tisa tuliyowachia mwezi jana tarehe 9 2020. Waliochiwa leo wameachiwa katika makundi tofauti kundi A wale walirudishwa kwao kwa vitisho vya usalama mwaka 2019 na kurudi tena nchini Uganda na kukamatwa. Nafikiri waliobaki jela wakitumikia vifungo ni 39.

Kutesa ameongeza kwamba kuondolewa kwa makosa raia hao wa Rwanda ni kutokna na mkutano wao wa juzi mjini Kigali Rwanda, ambapo Uganda imekubali kutekeleza yaliyotiwa saini na viongozi wa mataifa hayo mawili mwaka jana mwezi Agosti mjini Luanda Angola, Ili kumaliza uhasama uliopo :

Chanzo cha picha, IKULU YA RWANDA

Maelezo ya picha,

Yoweri Museveni na Paul Kagame wa Rwanda walipoweka MOU ya kumaliza uhasama kati yao

Mbali na makubaliano ya viongozi hao wawili pia waliunda jopo linalohusisha utekelezaji wa makubaliano hayo.

Jopo hilo linahusisha mawaziri wa masuala ya kigeni wale wa masuala ya ndani na wanasheria wakuu kutoka mataifa yote mawili

Hatahivyo ripoti hiyo imesema kwamba kuondolewa mashtaka dhidi ya raia hao 13 hakumaanishi kwamba hawana hatia na kwamba pia Rwanda inatarajiwa kuangazia maswala kuhusu raia wa Uganda wanaozuiliwa nchini humo.

Kutesa amewafahamisha rai hao wa Rwanda walioachiwa huru kwamba ni matarajio ya Uganda kuwa hawatarudi tena nchini Uganda kutekeleza vitendo vilivyowafanya kukamatwa.

Alitoa wito kwa serikali ya Rwanda kuonyesha ishara ya nia njema kuwachilia Waganda walioko kizuizini nchini Rwanda, na kutowauwa ovyo Waganda.

Lakini mwakilishi wa ubalozi wa Rwanda nchini Uganda Noel Mukyo alijibu tuhuma za kuwauwa Waganda akisema:

''Serikali ya Rwanda imekuwa wazi juu ya vifo vya raia wa Uganda katika ardhi ya Rwanda, wale waliouwawa ni wafanya magendo waliokuwa wakipitia Uganda kuingia Rwanda, na serikali ya Rwanda imeshatowa matamshi rasmi kuhusu vifo hivyo.

Tukio hili limefanyika siku chache kabla ya rais wa Uganda Yoweri Museveni na Paul Kagame wa Rwanda wakitarajiwa kukutana siku ya Ijumaa wiki hii katika mpaka wa Uganda na Rwanda wa Katuna.

Raia wa pande zote mbili wanatarajia marais hao watafungua mpaka wa Gatuna uliofungwa mwezi wa February mwaka jana na kurudisisha uhusiano mwema wa mataifa hayo

Maelezo ya picha,

Raia hao ikiwemo wanawake watatu wamekabidhiwa kwa maafisa wa uhamiaji wa Uganda mbele ya mwakilishi wa ubalozi wa Rwanda nchini Uganda.

Jopo hilo pia liliandaa vikao vyake mjini Kampala na Kigali ambapo masuala yanayohusu mataifa yote mawili yalijadiliwa kwa kina.

Katika kikao chao cha mwisho kilichofanyika tarehe 14 mwezi Februari 2020 , hatua kubwa zilipigwa katika kubaini masuala muhimu ambayo yanahitaji kuangaziwa na pande zote mbili kwa lengo la kuimarisha uhusiano bora kama ilivyoafikiwa katika makubaliano hayo.