Brexit: Uingereza haitatoa viza kwa wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi

Waitress

Chanzo cha picha, PA Media

Wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi hawatapata viza chini ya mpango mpya wa uhamiaji wa serikali baada ya Uingereza kujiondoa katika Muungano wa Ulaya.

Serikali inahamasiha waajiri kuacha kutegemea wafanyakazi wa kulipwa mshahara wa chini kutoka Ulaya na kuwekeza zaidi katika kudumisha wafanyakazi na kuendelezea teknolojia.

Wizara ya mambo ya ndani imesema Ulaya na raia wa nchi ambazo sio wanachama wa Muungano huo watakuwa wanachukuliwa walio katika daraja moja baada ya usafiri huru kati ya Uingereza na Muungano wa Ulaya kufikia ukomo wake Desemba 31.

Makampuni yanasema sheria kali kama hizo zitafanya iwe vigumu kuvutia wafanyakazi.

Lakini waziri wa mambo ya ndani Priti Patel amesema utekelezaji wa mfumo mpya kutamaanisha watu wenye weledi tu ndio watakaoingia Uingereza.

Serikali ambayo ilisema inalenga kupunguza wahamiaji kwa ujumla Uingereza, inataka kuanzisha mfumo wa uhamiaji wa kutumia alama ambazo mtu atakuwa anapata baada ya kutimiza vigezo kama ilivyo ahidi katika manifesto yake wakati wa uchaguzi.

Chini ya mfumo huo, wafanyakazi wa nchi za nje ya Uingereza ambao wangetaka kuingia Uingereza itakuwa lazima wawe na uwezo wa kuzungumza Kiingereza na mtaalam kwa kazi fulani baada ya kuidhinishwa na atakayemdhamini.

Wakati wa mchakato huo mhamiaji atakuwa anapewa alama 50 iwapo atatimiza vigezo hivyo.

'Kuendeleza na kukubali mabadiliko'

Kwa ujumla itakuwa lazima kwa mhamiaji kufikisha alama 70 ili aweze kufanya kazi Uingereza huku pia akipata alama kulingana na kiwango chake cha elimu, mshahara atakao kuwa anapokea na kufanyakazi katika sekta zenye upungufu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini serikali imesema haitaanzisha mfumo wa kuvutia wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi na kutaka makampuni kuendekeza na kukubali mabadiliko ili kumaliza usafiri huru wa watu kati ya nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya na Uingereza.

"Ni muhimu kwa wafanyakazi kuachana na utegemezi wa mfumo wa uhamiaji wa Uingereza kama njia mbadala ya kuwekeza katika kuendelea kuwa wafanyakazi, uzalishaji na uwekezaji mkubwa katika teknolojia," imesema.

Badala yake imesema raia wa Muungano wa Ulaya milioni 3.2 ambao wametuma maombi ya kutaka kuendelea kuishi Uingereza watasaidia kufikia kiwango cha wafanyakazi wanaohitajika Uingereza.

Serikali pia imegusia kuongeza mara nne wafanyakazi hadi 10,000 katika mfumo wake wa wafanyakazi wa muda katika sekta ya Ukulima pamoja na mipango ya kuvutia vijana ambao utaruhusu vijana 20,000 kuingia Uingereza kila mwaka.

Huku shirika la muungano wa makampuni Uingreza likiwa limekumbatia baadhi ya mapendekezo, limesema kwamba baadhi ya makampuni yatakuwa na wakati mgumu kuhusu namna ya kusajili watu wanaohitajika kuendeleza shughuli za biasha

Mkurugenzi wa shirika hilo Carolyn Fairbairn alisema, "Makampuni ambayo huajiri kutoka nchi za nje na kuwekeza katika kuwapa wafanyakazi ujuzi na teknolojia mpya hawana chaguo lolote kwa sababu vyote vinahitajika kusongeza mbele uchumi."

Chuo cha uuguzi cha Royal College of Nursing kilionyesha wasiwasi kwamba mapendekezo yaliyotolewa itakuwa vigumu kufikia mahitaji na huduma kwa raia", huku katibu mkuu akisema kwamba mipangi hiyo itaathiri pakubwa katika sekta ya afya.

Chama cha wafanyakazi wa majumbani Uingereza kimeelezea kukosekana kwa mpango makhususi kwa wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi ni kutowajibika na msemaji wa chama hicho akaongeza kuwa wameshangazwa na uamuzi wa serikali.

"Kuondoa usajili wa wafanyakazi wanaotoa hudumu za kawaida kwa wagonjwa chini ya mfumo mpya wa uhamiaji itakuwa moja ya sababu ya raia kuwa hospitali kwa muda mrefu wakisubiri hudumaa au hata kutopata huduma kabisa," wameongeza.

Wakati huohuo, rais wa vyama wa wakulima Minette Batters ameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu kushindwa kwa serikali kutambua mahitaji ya Ukulima na chakula nchini Uingereza katika mipango yao.

Aidha shirikisho la vinywaji na vyakula, pia limesikitishwa na hatua hiyo na kuonyesha wasiwasi wake juu ya wafanyakazi katika makampuni ya nyama, kuoka na wale wanaotengeneza vyakula kama jibini na tambi kwasababu hawafikishi viwango vilivyowekwa chini ya mfumo mpya wa uhamiaji.

Chanzo cha picha, PA Media

Chini ya mpango mpya, mhamiaji atapata tu mafao ya mshahara hadi wakati ambapo atakuwa ahitaji tena mdhamini kwa kawaida huwa ni miaka mitano.

Kwa sasa raia kutoka nchi za Muungano wa Ulaya Uingereza wanaweza kudai mafao iwapo wanafanyakazi.

Raia kutoka nchi ambazo si Muungano wa Ulaya wanaruhusiwa kihalali kupata mafao wanapopata vibali vya makazi ya kudumu ambavyo kawaida huwa ni miaka mitano baada ya kuishi Uingereza kihalali.

Kufuatia ushauri wa kamati wa uhamiaji, mshahara kwa wafanyakazi wenye ujuzi wanaotaka kuingia Uingereza utapunguzwa kutoka £30,000 hadi £25,600.

Bodi huru ya ushauri ilisema kwamba kupunguza mshahara kutasidia kusajili walimu na wahudumu wa afya wenye ujuzi.

Tofauti na mfumo wa sasa, wanaotuma maombi wataweza kushiriki katika biashara ya hisa.

Wale wanaopata mshahara wa chini ya £25,600, lakini zaidi ya £20,480, bado wanaweza kuomba viza kama walikuwa na kazi katika sekta yenye upungufu, au kama wana shahada ya uzamivu yenye uhusiano na kazi anayofanya.

Orodha ya sekta zenye upungufu itakuwa inapitiwa na kamati ya ushauri ya uhamiaji, serikali imesema.

Kazi ambazo kwa sasa zina upungufu wa wafanyakazi kulingana na kamati hiyo ni pamoja na uhandisi, madaktari, wauguzi, wanasaikolojia na wacheazaji densi ya bale.

Pia inasemekana kwamba vipengele vingi vitaondolewa kwenye mshahara kwa wahudumu wa afya wanaotunza jamii na sehemu kubwa tu ya sekta ya kibinafsi kiasi kwamba itakosa maana na kufanya iwe vigumu kuvutia watu wenye ujuzi mbalimbali katika mazingira ya kikazi ambayo si rafiki.