737 Max: Vifusi vyapatikana kwenye tangi la mafuta ya ndege ya Boeing 737

A Boeing 737 MAX 8 airplane is pictured outside the company's factory.

Chanzo cha picha, Getty Images

Shirika la Boeing linakumbwa na hatari ya kukabiliwa tena na suala la usalama wa ndege zake baada ya vifusi kupatikana kwenye tengi za mafuta katika ndege kadhaa ambazo zilikuwa zinasubiri kuwasilishwa kwa wanunuzi.

Msimaizi wa ndege aina ya Boeing 737, amewaambia wafanyakazi wake kwamba ugunduzi huo ni jambo lisilokubalika.

Msemaji wa shirika la Boeing amesema kwamba kampuni hiyo haikugundua tatizo hilo na kusababisha ndege hizo kuchelewa zaidi kuanza tena huduma zake.

Hilo linawadia wakati ambapo ndege aina ya 737 Max bado hazijaidhinishwa kurejea kutoa huduma baada ya kusababisha ajali mbili mbaya ambapo abiria walipoteza maisha.

Shirika hilo la Marekani lilisema kwamba limegundua vifusi vilivyoachwa ndani kwenye matenki ya fueli kwa ndege kadhaa za 737 Max ambazo hazijawasilishwa kwa wateja.

Msemaji wa kampuni hiyo aliiambia BBC: "Wakati tunazikagua na kuchunguza ndege za 737 Max vile zilivyo kabla ya kuziwasilisha, tukagundua vifusi. Hilo likachangia kufanyika kwa ukaguzi upya tena wa kina na kufanyia mfumo wake marekebisho mara moja."

Vifusi hivyo ni kama vile uchafu, vifaa vya metali na vingine vilivyoacha na wafanyakazi wakati inaunganishwa.

Ugunduzi huo ni wa haivi karibuni zaidi katika msururu wa matatizo yanayokumba shirika hilo la ndege ambalo wakati fulani lilikuwa lina ndege za Boeing zenye mauzo mazuri zaidi.

Kwa sasa ndege hizo zimesitishwa kutoa huduma na wadhibiti kote duniani tangu Mwarch 2019.

Ndege hizo zilipigwa marufuku kusafiri baada ta ndege mbili kuanguka na kusababisha vifo vya watu 346.

Ajali zilizosababishwa na ndege za 737 Max

  • Oktoba 29, 2018: Ndege ya 737 Max 8 iliyokuwa inaendeshwa na Shirika la Lion Air ilianguka baada ya kuondoka Indonesia na kusababisha vifo vya watu 189 waliokuwemo.
  • Januari 31 2019: Shirika la Boeing lilisema kwamba limepata oda ya ndege zake aina ya Max kwa wateja 79
  • Machi 10, 2019: Ndege ya 737 Max 8 iliyokuwa inamilikiwa na shirika la ndege la Ethiopia, ilianguka na kusababisha vifo vya watu 157 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo
  • Machi 14 2019: Shirika la Boeing lilisistisha huduma ya ndege zake za 737 Max

Shirikisho la utawala wa safari za anga (FAA), liliiambia BBC kwamba linafuatilia hatua itakayochukuliwa na Boeing baada ya ndege zake kupata ajali: "Shirika la (FAA) linafahamu kwamba Boeing inafanya ukaguzi wa ndege ambazo hazijawasilishwa kwa wateja kama sehemu ya juhudi za kuhakikisha ubora wa ndege zak

"Shirika hilo liliongeza uchunguzi wake kwa kuzingatia ukaguzi wa awali na kuchukua hatua zaidi kulingana na matokeo," liliongeza.

Boeing ilisema kwamba haikuratajia vifusi hivyo kusababisha kuchelewa zaidi kwa kwa ndege za 737 Max kuanza tena kutoa huduma zake,

Kampuni imesema kwamba huenda ndege hizo zikaanza tena kusafiri kuanzia katikati ya mwaka huu.