Hali ya watoto ya baadae ni ya utata, wataalamu waonya

A baby with a doctor

Chanzo cha picha, Getty Images

Hakuna nchi inayotoa fursa ya malezi ya kiafya na mazingira yanayofaa kwa ajili ya hali zao za baadae, linasema Shirika la afya Duniani (WHO).

Wataalamu wanasema mabadiliko ya hali ya hewa na matangazo ya kudhuru yanayoshawishi ulaji wa vyakula vinavyopatikana kwa urahisi na unywaji wa pombe wa watoto wadogo vinawaweka watoto katika hatari.

Uingereza iliwekwa katika nafasi ya 10 miongoni mwa nchi zenye afya na hali bora a maisha ya watoto.

Hata hivyo iliashindwa katika kuyalinda mazingira ya siku za usoni ya watoto .

Ripoti ya shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef na tume ya Lancet zilitaja nchi 180 katika uwezekano wa watoto kuweza "kushamiri ", kwa kuzingatia afya na maisha bora ya watoto kama vile kuwapatia elimu, vyakura vyenye virutubisho na kiwango cha vifo vya watoto.

Nchi hizo pia ziliwekwa katika viwango kwa kuzingatia uwezo wao wa utoaji wa hewa ya kaboni.

Wataalamu takriban 40 wa afya ya watoto walionya kuwa miongo miwili iliyopita "itakua ya madhara" ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa na serikali kote duniani.

"Kila mtoto kote duniani kwa sasa anakabiliwa na vitisho vilivyopo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na shinikizo za kibiashara,''alisema Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand, Helen Clark, ambaye ni mkuu msaidizi mwenza wa tume ya Unicet ya masuala ya watoto.

" Nchi zinapaswa kubadili nanama zinavyochukulia afya ya watoto wadogo na waliotimiza umri wa kubalehe ili kuilinda dunia watakayoirithi siku zijazo."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Matangazo ''yanayodhuru''yanawaweka watoto katika hatari ya kiafya, wataalamu wanasema

Wataalamu wanaonya juu ya kupanda wa kiwango cha nyuzi joto 4C katika viwango vya joto vya dunia ifikapo mwaka 2100, kwa kiwango cha makadirio ya sasa na kwamba kiwango hicho kinaweza kusababisha "athari mbaya za kiafya " kwa vizazi vijavyo - kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari, mawimbi ya joto, ongezeko kubwa la utapiamlo na kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa kama vile malaria.

"Zaidi ya watu bilioni mbili wanaishi katika nchi ambako maendeleo yanakwamishwa na mizozo ya kibinadamu, na majanga asilia , matatizo yanayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa ," alisema waziri Awa Coll-Seck, kutoka Senegal, ambaye ni mwenyekiti msaidizi wa tume hiyo.

Huku nchi maskini zaidi duniani zilibainika kuwa miongoni mwa nchi zinazotoa kiwango kidogo zaidi cha gesi chafu, zilionekana kuwa ndizo zenye uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa.

Unaweza pia kusoma:

"Kuboresha viwango bora kwa ajili ya watoto sana hakufai kuharibu hali za maisha za siku zijazo kwa watoto duniani ," aliongeza Bwana Coll-Seck.

Mnamo mwaka 2015, nchi za dunia zilikubaliana juu ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs),mkiwemo kutokomeza njaa, umaskini na kuchukua hatua za mabadiliko ya hali ya hewa, lakini baada ya miaka mitano kumekua na mafanikio machache sana katika kufikia malengo hayo.

Marekani na Australia zilikua miongoni mwa nchi zinazozalisha hewa chafu zaidi duniani.

'Makadirio'

Ripoti hiyo pia imeelezea tisho linalowakabili watoto kutoka kwa masoko hatari ya biashara.

Ilibaini kuwa wanaonyeshwa matangazo 30,000 ya televisheni kila mwaka, mkiwemo yale ya pombe, vyakula visivyo na virutubisho na vinywaji vyenye sukari nyingi.

Muandishi mmoja wa tume hiyo Anthony Costello, profesa wa chuko kikuu cha London wa masuala ya afya ya duniani ya kudumu, alionya kuwa ongezeko la matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa watoto na vinana waliofikia umri wa balehe linamaanisha hatari ya soko la bidhaa hzi hatari ni hata kubwa zaidi.

"Tuna taarifa chache na idadi juu ya kuongezeka zaidi kwa matangazo ya kibiashara ya mitandao ya kijamii na kiwango kinachowalenga watoto wetu ,"alisema.

Mnmo mwaka 2019 ripoti ilikadiria kuwa karibu watoto bilioni 2.2 na watiu wazima duniani walikua na uzito wa mwili wa kupita kiasi na zaidi ya watoto milioni 150 walidumaa katika ukuaji wao.

Nchi pekee uliyoongoza katika utoaji wa hewa ya oksijeni ifikapo mwaka 2030, huku pia zikifanya vema katika kuboesha afya ya watot na maisha bora zilikua ni Albania, Armenia, Grenada, Jordan, Moldova, Sri Lanka, Tunisia, Uruguay na Vietnam.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

kumekua na ongezeko la visa vya magonjwa ya sukari kutoka na lishe duni duniani, miongoni mwa waathiriwa wakiwa ni watoto

Ripoti hiyo iliyoa wito wa hatua mpya kuchukuliwa niongozi mwa wakazi wa dunia na kuongozwa na watoto kwa ajili ya watoto, ikiwa ni pamoja na :

  • Acha kutoa kumaliza hewa ya safi ya CO2 mara moja , ili kuhakikisha watoto wanakuwa na maisha ya baadae katika sayari hii.
  • Wekeni watoto na vijana walio katika umri wa barehe katika vituo vya juhudi zetu za kufikia maendeleo endelevu
  • Sera mpya na uwekezaji katika sekta zote zitekelezwa kwa kuzingatia afya na haki za mtoto
  • Jumuisha sauti za watoto katika sera za maamuzi
  • imarisha sheria na masharti juu ya utekelezwaji juu ya matangazo ya kibiashara yenye madhara ,zilingwa mkono na protokali mpya ya mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za mtoto.
Maelezo ya sauti,

Habari za Global Newsbeat 1100 31/01/2018