'Tunahofia kulima mashamba yetu upande wa Uganda'

'Tunahofia kulima mashamba yetu upande wa Uganda'

Mkutano wa rais wa Rwanda Paul Kagame na Yoweri Museveni wa Uganda kumaliza tofauti baina ya nchi zao unatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa kwenye mpaka wa Gatuna baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huu unachukuliwa kama hatua ya mwisho ya kutathmini utekelezwaji wa makubaliano yaliyosainiwa na marais hao mwaka jana mjini Luanda –Angola chini ya upatanishi wa rais wa Angola na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa Rwanda wanaoishi maeneo ya mpakani bado wana kilio kwa kuwa wamekuwa wakiitegemea Uganda kwa huduma nyingi na sasa hawaruhusiwi na serikali ya Rwanda kukanyaga kwenye ardhi ya Uganda.

Wengi wana mashamba nchini Uganda na hulazimika kutumia njia haramu kwenda nchini Uganda.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana ametembelea wananchi hao kwenye mpaka wa Cyanika na kutuletea taarifa ifwatayo