Amanda McCracken: Mwanamke aliyekuwa na wapenzi wengi lakini akasalia bikira hadi umri wa miaka 41

Amanda McCracken akicheza densi na mumewe Dave wakati wa harusi yao

Chanzo cha picha, Zack Weinstein

Maelezo ya picha,

Amanda McCracken akicheza densi na mumewe Dave wakati wa harusi yao

Mwaka 2013, mwandishi wa Marekani Amanda McCracken alichapisha taarifa katika gazeti la New York times ambayo ilisambaa. Ilikuwa na jina la Je ubikra wangu unaweza kuishi?.

Wakati huo McCracken ambaye alikuwa na umri wa miaka 35 alitoa sababu kwa nini aliamua kutoshiriki ngono.

''Afadhali nihisi uchungu wa kutoshiriki ngono badala ya kusononeka na upweke baada ya kuwa na mtu asiye na hisia za mapenzi'', alielezea.

Pia alisema kwamba ubikra umekuwa kitambulisho chake , na kwamba hilo halijamzuia kuwa na uhusiano wa kihisia na makumi ya wanaume..

Katika mahojiano wiki hii na kipindi cha BBC cha NewsDay McCracken alifichua jinsi alivyokosolewa kwa uamuzi wake wa kusubiri hadi atakapopata mpenzi wa kweli kabla ya kushiriki tendo la ndoa..

''Wakosoaji walishangazwa sana, nilihisi kwamba wananiadhibu kwa kuwa mkweli'', alisema.

''Nilishambuliwa kwa kutofuata utamaduni uliopo. Na sasa nimegundua kwamba sikujua kwamba hadithi yangu itakubalika'', alisema.

Chanzo cha picha, New York Times

Maelezo ya picha,

Taarifa ya Armanda aliochapisha katika gazeti la New York Times

Kwa McCracken ukosoaji huo unafichua unafiki: Ninaishi katika maisha ya utamaduni endelevu ambapo wanawake hupewa motisha ya kufanya kile wanachotaka na miili yao, aliongezea.

Kama utaratibu maalum wa Chakula

Mwandishi ambaye pia ni mwalimu wa somo la Kiingereza mbali na kuwafunza wanariadha wa mbio ndefu anatumia mfano asilia kuelezea kwanini ubikra wake ulisababisha hasira kwa wengi.

''Ni kama utaratibu maalum wa chakula'', alielezea: Iwapo wanakukaribisha katika chakula cha jioni na kusema kwamba hutaki kula chakula fulani, kila mtu anafikiria kwamba hawafai kula chakula hicho nao.

''Pia inalinganishwa na unywaji wa pombe .Iwapo hutaki kunywa pombe inaonekana kama uamuzi mzuri wa kiafya ,Lakini hapo zamani uliulizwa kwa nini hunywi pombe? na jibu lilikuwa , Je mnadhani sifai kunywa?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kutoshiriki ngono ilikuwa njia ya kudhibiti maisha yangu, anasema mwandishi huyo

McCracken pia anasema alishambuliwa kutoka kona zote kutoka kwa wahafidhina hadi walio huru. Nadhani watu walikerwa na kwa nini sikuingiliana na pande zote. Hawakuweza kuniingilia.

Chukua udhibiti

Mbali na maoni ya wengine, McCracken anatambua kwamba mojawapo ya lengo lake la kutoshiriki ngono licha ya kushiriki katika mahusiano kadhaa - mengine na wanaume aliowapenda - alikuwa na wasiwasi wa kupoteza udhibiti.

Kwa wazo hilo kuwa bikra kwake ilikuwa njia ya kuchukua udhibiti wakati ambapo maisha yake yalikuwa yakikosa mwelekeo.

''Wapenzi wangu watatu wa kwanza niliokuwa nao waliniacha na kutafuta wasichana wengine na muongo mmoja baadaye nilikuwa naogopa vitu kama hivyo kunitokea tena'', alikiri. Nilifikiria kwamba iwapo wataniacha , nitasalia na ubikra wangu.

Pia alianza kuwa na wasiwasi kuhusu iwapo matarajio yake ya kupata mpenzi yalikuwa ya juu.

''Na iwapo uamuzi wako wa kutoshiriki ngono ulikuwa unakupunguzia fursa ya kupata mpenzi ambaye yuko tayari kuwajibika. Lakini baadaye niligundua kwamba hiyo si sababu'', alifichua.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Amanda alifanikiwa kuimarisha penzi alilolitaka

Penzi

Hadithi ya Amanda McCracken ilikuwa na mwisho mwema. Katika hadithi aliyoandika tarehe 14 mwezi Februari siku ya wapendanao kwenye jarida la mtandaoni la HuffPost , alisema jinsi alivyokutana na Dave , ambaye sasa ni mumewe.

Akizungumza na BBC kuhusu sababu zilizomfanya kusubiri kwa kipindi kirefu , mwanamke huyo mjamzito alisema: Wapenzi wangu wa kwanza waliniacha na kutafuta wanawake wengine hivyobasi muongo mmoja baada ya hayo nilikuwa nikiwa na mahusiano yaliyojaa hofu na kufikiria kwamba iwapo nitaachwa tena , kitu nitakachosalia nacho ni ubikra wangu.

''Ni suala la kuchukua udhibiti kwa kuwa nilihofia kana kwamba nitaachwa tena. Nisingesema kwamba ni kitu nilichotaka kupata''.

''Nilihisi kwamba nilianza kuwa na wasiwasi iwapo matarajio yangu ya mapenzi yalikuwa ya juu na iwapo kutoshiriki ngono kulikuwa kunanitenga na mpenzi niliyemtaka na nikabaini kwamba huo si ukweli''.

''Hilo linaacha swali kuu ambalo kila mtu angependa kujua. Je subira huvuta heri? Ni kweli huvuta heri, lakini sio jinsi watu wengi wangefikiria''.

''Tendo la ngono lilikuwa zuri, lakini safari hii haikuwa kuhusu tendo la ndoa. Sasa niko na mwanamume kwa jina Dave na niko katika uhusiano wa uwajibikaji naye''.

Lengo langu lilikuwa kusubiri na kuingia katika uhusiano na mtu ambaye angenipatia mapenzi na mimi niwe katika hali ya kuweza kulipokea penzi hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Badala ya kukataa chakula alikataa tendo la ndoa

"Mwisho wa msimu wa joto wa 2018 nilikutana na mwanajiolojia na mwanariadha wa milimani nilipokuwa nikinywa kinywaji changu na marafiki''.

Alikuwa amesitisha uhusiano na mwanaume mmoja ambaye alikuwa hapatikani mara kwa mara, Dave alikuwa ametalikiana miezi sita iliopita baada ya uhusiano wa miaka 18.

''Mwanaume huyu mwenye nywele ndefu kutoka kisiwa cha Long hakuwa chaguo langu, alinitumia ujumbe na kunipigia simu'' , anasema kwa kucheka.

Kando na imani potofu , Amanda hakuhisi wasiwasi tumboni mwake wakati alipokuwa na Dave.

''Sikuhisi kwamba nilikuwa katika mapenzi. nilihisi kana kwamba kila kitu kilikuwa kawaida, sikuwa na ule wasiwasi wowote wa kuwa na mpenzi? Sikuwa na hofu kwamba angeniacha'', aliandika.

Mwishowe - na kutokana na usaidizi wa washauri kadhaa, Amanda aligundua kwamba alikuwa akijikandamiza na kuishi maisha ya utabiri.

''Nilihisi mapenzi na wanaume ambao hawakuwepo , wanaume ambao nilijua sitashiriki nao ngono kwa kuwa hawangenipenda ama kujiwajibika kwangu.

Pia aligundua kwamba amezoea kukataa ngono badala ya kukataa chakula.