Dagmar alipiga fidla ili kuhakikisha kuwa sehemu muhimu ya ubongo wake haiharibiwi

Dagmar alipiga fidla ili kuhakikisha kuwa sehemu muhimu ya ubongo wake haiharibiwi

Dagmar Turner 53, aligundulika kuwa na uvimbe upande wa kulia wa ubongo wake. Wakati wa upasuaji katika hospitali ya chuo iitwayo King jijini London, aliamua kupiga fidla ili kuwezesha madaktari kuhakikisha kuwa wakati wa upasuaji hawaharibu sehemu muhimu inayomuwezesha kuchezesha mikono yake.